Mambo vipi washikaji?

Gabriel3266

New Member
Aug 2, 2010
4
0
Habari zenu wenzangu wa JF. Naitwa Gabriel, natoka Marekani. Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu huko Marekani lakini niko TZ siku hizi. Nimejitolea kama mwalimu, lakini kwa sasa najaribu kutengeneza mradi wa kuwatetea wafungwa wa kike, hasa hasa wafungwa wajawazito na watoto wao. Nataka kujifunza zaidi kuhusu uhusiano wa haki za wanawake na haki za uhalifu na nafasi za kupata michango, na kadhalika. Kwa hivyo, ningependa sana kuwasiliana na wanaJF kuhusu mambo hayo. Asanteni sana na kwa heri. Nangoja kwa hamu kuzungumza na ninyi. Nawatakia kila la heri.

Wasalaam,
Gabriel Maeck

PS. Nimehariri ujumbe huu kwani najua kuandika lugha ya kitaa sio ya heshimu. Nisameheni.
 
Karibu lakini jaribu kuwa neutral na lugha zako za mitaani, nani mshikaji wako?

Wengine humu ni babu zako kiumri!!
 
Duh sijui uko kitaa gani mshkaji? Hiyo style uliyokuja nayo ni babu kubwa. Karibu jamvini
 
Back
Top Bottom