mambo sasa yamenichanganya

MUGUNDA

Member
Aug 11, 2011
69
62
ndugu wanajf ni jana tu nimepost mawazo ya mwanaume aliyokuja anyasema kwangu kwa kuomba ushauri nashukuru kwa waliochangia. Sasa kikubwa zaidi leo hii hasubui mwanamke wa yule jamaa nimekutana naye nikiwa nakwenda kazin akanisimamisha, akadai mume wake hamuon kama mwenye thaman make anakunywa pombe kila siku na anakuja anajirusha kitandandan tu hata hajafanya chochote kile even hata kuoga. akadai anasubiri ajifungue ili amuachie nyumba yake aendelee kukaa kwake kule ankofanya kazi maana amechoka kwa hili.
mwanamke akiwa analia amedai kuwa mara nyingine mwanaume anakuwa anachati na wanawake live kwenye simu wakiwa sebulen.sasa nimeshindwa la kumwambia hapo lakin nikamsihi avumilie ili tuonane kwanza na mwanaume tuongee hili make nayeye alinifuata kama rafiki yake kunieleza hayo na mke ameniona kama rafiki wa mke wake akaniambia ili abadilike. wana jf hebu nipe ushauri niwafanyeje hawa wanandoa?
 
Mkuu, wote wawili wanakuomba ushauri mtu mmoja, ni hatari. Wakipatana utakuja kubaki na lawama. Washauri wafikishe matatizo yao kwa ndugu au viongozi wa dini na wewe ubaki neutral, labda hapo utasalimika.
 
waambie ndoa ni watu wawili, wakae mume na mke wazungumze matatizo yao wayamalize wenyewe
 
Huyu mwanamke anaekwambia wewe kama mumewe haogi kaanza wakatu gani hiyo tabia sababu kama ni mke yeye ni wajibu wake
kuhakikisha mumewe hatoki bila kuoga nguo iwe safi mbona kama anakumbuka shuka kumeshakucha? asijidai bure kosa ni lakwake la mumekua mchafu loh haoni hata aibu kukwambia haoni kama anajitukana mwenyewe?
mwanamme ana Chat atafute ubunifu wakumueka mumewe ajue nini mumewe anapenda...jengine wambie wote wakae chini waongee
wayamalize....
 
Nimetoka kapa,
Hata siielewi story yenyewe,
Weka link ya hiyo story iliyopita kutusaidia ambao hatujaelewa connection yake na hii ya leo!!
 
ndugu wanajf ni jana tu nimepost mawazo ya mwanaume aliyokuja anyasema kwangu kwa kuomba ushauri nashukuru kwa waliochangia. Sasa kikubwa zaidi leo hii hasubui mwanamke wa yule jamaa nimekutana naye nikiwa nakwenda kazin akanisimamisha, akadai mume wake hamuon kama mwenye thaman make anakunywa pombe kila siku na anakuja anajirusha kitandandan tu hata hajafanya chochote kile even hata kuoga. akadai anasubiri ajifungue ili amuachie nyumba yake aendelee kukaa kwake kule ankofanya kazi maana amechoka kwa hili.
mwanamke akiwa analia amedai kuwa mara nyingine mwanaume anakuwa anachati na wanawake live kwenye simu wakiwa sebulen.sasa nimeshindwa la kumwambia hapo lakin nikamsihi avumilie ili tuonane kwanza na mwanaume tuongee hili make nayeye alinifuata kama rafiki yake kunieleza hayo na mke ameniona kama rafiki wa mke wake akaniambia ili abadilike. wana jf hebu nipe ushauri niwafanyeje hawa wanandoa?

Kaka kwani we ndiye uliekua bestman kwny harusi? Kama ndio kaa na wanandoa hao uwasikilize kwa makini kisha utapata ufumbuzi wa matatzo vngnevyo waambie wawatafute wahucka sahihi kwan wale hawakuwepo pale kula keki tu na kunywa bali kusaidia kutatua matatzo yatakayowakabili wanandoa hao
 
Nimejitahidi kuisoma sijui ni njaa imaniuma! sijakusoma kabisa
 
Utajijua mwaka huu,kama unajidai ww ndio middle men wa ndoa za watu subiri siku wenye ndoa yao wangudue utatafuta pa kujificha,endelea tu kujidai mama ushauri,
Achana na hiyo kesi waambie wakaongee na washenga wao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom