Mlalahoi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2006
- 2,182
- 883
Ndugu Wana chama wa Chadema,kwa hoja hii ni mhimu viongozi wakuu wa Chadema na Wajumbe wa kamati Kuu wayafanyie kazi. Sote tuna tambua kua Uchaguzi wa Mwaka 2010 ulikua na changamoto nyingi hasa kwa Chadema kuonekana ni Chama ambacho kinaelea juu tu ngazi ya Taifa! Hili limetokea kwa Chadema kuto kusimamisha Wagombea wa Ubunge baadhi ya Majimbo! Wito wangu ni sasa kujielekeza zaidi katika maeneo ya wilaya na hasa yale ambayo Chadema haikusimamisha wagombea katika majimbo hayo! Lakini jambo jingine ni mhimu kujitenga na mahusiano ya moja kwa moja na Kanisa Katoliki iwe mahusiano na Baraza la Maaskofu TEC iwe kwa wao kupenda kutoa ushauri kwa Chadema au Chadema kuomba Ushirikiano na TEC,pia Kadinal Pengo aache kutoa matamko pale tu anapo ona viongozi wa Chadema wanaongelea jambo fulani! Tatu,utaratibu uliotumiwa wa kutumia formula kupata Wabunge wa Viti Maalumu uangaliwe kwani unawapa zaidi nafasi wabunge wengi watoke Kilimanjaro! Nne,Imefika wakati sasa Chadema imulipe fidia Mzee Edwin Mtei kwa kuanzisha Chadema ili Chadema itoke kwenye mfumo wa Kampuni Binafsi na sasa kuwa Chama cha Wanachama! Tano,Mheshimiwa Freeman Mbowe sasa kuwapa nafasi wanachama wengine kugombea nafasi ya Uenyekiti na kuondoa taswira ya kuwa chama cha Ukoo. Mwisho, Matumizi ya Ruzuku ndani ya Chadema ni mhimu yaelekezwe Wilayani,Dr Slaa kulipwa 12 milioni kwa mwezi ni ufisadi ndani ya Chama.
How stupid!Kabla ya kukurupukia mambo yanayokikwamisha chama cha siasa-ambacho ni mjumuko wa watu-kwanini usianze kwanza na mambo yanayoukwamisha ubongo wako kufanya kazi yake ipasavyo?Chadema haihitaji ushauri wa kiendawazimu.
Get a life!