MAMBO HAYA NI BAADHIi YA CHANZO CHA MATATIZO YA UONGOZIi TANZANIA, TUFANYE NINI KUJIREKEBISHA?

milimo

Member
Nov 29, 2012
61
32
Tusema ukweli kwamba, tuna msingi mbaya wa uongozi toka huko
nyuma, tatizo kubwa zaidi ni kwamba tunaendelea na mtindo huo
kwa kasi zaidi kwa sababu hutajapata kiongozi jasiri wa kurekebisha
mapungufu haya; Haya ni miongoni mwa vitu vinavyosababisha
Ombwe la uongozi tulilonalo.


Moja; Bendara fuata upepo ndio wanapata uongozi badala kuwa
waongozwa:

Tuseme ukweli, kiongozi mzuri anatakiwa awe mtu mwenye msimamo
kwa mamuzi yake na anayeweza kushirikiana na walio chini yake
kufanya maamuzi yanahusu eneo lao la kazi. Lakini siku hizi viongozi
wengi iwe kwenye siasa au maeneo ya utendaji ni wale wanao soma
nyuso za walio juu yao. Bila kuwa mtu wa "YES SIR/MADAM" kwa kila
kitu unachoambiwa na wakubwa ni vigumu kupata uongozi au cheo.
Hata wale ambao walikua na uwezo wa ‘ku-argue' kwa manufaa ya
nchi wameacha kwa sababu hailipi tena. Kwa mtindo huo wale wenye
tabia za kuwa wafuasi ndio wanakuwa viongozi, uongozi wao ni
kusikiliza nini wakubwa wake wanasema bila yeye kulitawala
eneo lake la kazi. Hata kikohozi cha mkubwa wake ni kitu ambacho
atakitafakari na kukifanyia kazi. Tuombe tupate utaratibu ambao
viongozi wanatokana na uwezo wao wa kupambanua mambo na
wenye ujasiri wa kusimamia sheria kwa maslahi ya taifa.


Pili; Kuchafua wale wanaonekana ni wadilifu na wenye misimamo:
Tumefikia hatua ambayo ni vigumu kupata mtanzania mwaminifu na
mwenye msimamo kwa maslahi ya nchi iwe kwenye siasa au utendaji.
Sio kwamba watu hao hatuna, Lahasha, wapo wa kutosha, ila tatizo ni
kwamba, akijitokeza mtu mwenye uzalendo wa taifa hili kuna kikundi/vikundi
cha watu ambao kwa kutumia fedha za kifisadi na makusudi kabisa kinafanya
juu chini aidha kuwachomekea madudu hao wadilifu na wao bila kujua wanaingia kichwakichwa na kunasya, wakisha nasya wanafumbwa midomo kwa kuhofia
siri zao kuwekwa hadharani. Na ikishindikana kuwanasa, huwa zinafanyika
mbinu zingine za kuwachafua kwa kutumia vyombo vya habari na kampeni za propaganda za mtu kwa mtu, wakishindwa hapo, kinachofuata ni kuwadhuru
wahusika kimwili na kisaikolojia. Hivyo tumefikia ambapo tumechanganyikiwa
kwa sababu wale ambao wanajaribu kujitokeza kutetea maslahi ya nchi ghafla
wanachafuliwa ili kuwanyamazisha na matokeo yake sisi wananchi tunabaki tumechanganyikiwa kwa sababu ni vigumu kutofautisha mchele na pumba.
Tuombe tupate viongozi wadilifu wenye kumcha Mwenyezi Mungu ambao kwa
makusudi watawalinda kuwathamini watu waminifu na kuwapa uongozi kwa
manufaa ya nchi.



Tatu; Tumekosa watu wenye ujasiri;
Kila kitu kina faida na hasara. Kupata Uhuru kirahisi bila
mapambano ya nguvu kubwa na wakoloni bila kumwaga
damu kulikuwa ni faida kubwa kwa Tanzania. Lakini kutokana
na faida kubwa hiyo bahati mbaya tumekosa kupata watu wenye
ujasiri wa kusimama na kusema hapana kwa mambo ya kifisadi
yanayofanyika, maana dhuluma yoyote ile ni mbaya zaidi ya ukoloni.
Tuanahitaji kuwa na majasiri wengi (wapo wachache) ambao
wataweza kusema hapana kwa ufisadi na uonevu kwa wanyonge
bila kupepesa macho. Tunahitaji watu wa kusema hapana kwa maonevu
wanayofanyiwa wanyonge kwenye kupata huduma za jamii kama elimu,
afya, pembejeo nk.


Mwenyezi Mungu tunakuomba Ibariki Tanzania na watu wake.
Tunakuomba uwalinda wale wenye ujasiri wa kusimamia kwa
uadilifu maslahi ya nchi, Amen.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom