Mambo 6 ya kuzingatia wanandoa kuhusu fedha

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,906
22,017
Zipo Ndoa ambazo mke na mume wanaishi tu kwa sababu ya watoto, au kuogopa kupoteza nyumba, au mali kwani utamu na raha ya Ndoa imetoweka, hata hivyo kila kitu kina chanzo na ni muhimu kujua chanzo ili uweze kutatua tatizo kabla halijakumaliza na kujikuta umechelewa.
wahenga walisema
"Heri Kinga Kuliko Kuponya". Unahisi huyo mwanamke anamwambia nini Mume wake hapo kwenye picha?

Tafiti nyingi zinaonesha kwamba migogoro mingi ya wanandoa hutokana na mambo yanayohusu pesa.
Pia mfumo wetu dume katika jamii umeongeza tatizo kuwa kubwa zaidi kwani suala la pesa ameachiwa mume bila mke kuwajibika, kujua au kuchangia lolote, hata wanawake wenyewe wengi wamejiweka katika kundi la kuwaachia wanaume kuwajibika kwa kila kitu kinachohusu pesa katika na kutoa maamuzi yote yanayohusu pesa katika ndoa.
Na kuna maamuzi mengine yameangamiza familia kwa sababu ni mtu mmoja tu katika ndoa ndo hutoa maamuzi linapokuja suala la pesa yaani baba au mume.

Sasa ulimwengu umebadilika wanawake nao wana uwezo, wanafanya kazi, wanaingiza pato katika familia na ndoa.
Pia kuna familia ambazo mke ndiye mwenye kipato kikubwa kuliko mume, na kuna ndoa ambazo kila mmoja akipata pesa hutumia anavyotaka yeye bila kukaa pamoja na kupanga nini kifanyike na matokeo yake kumekuwa na migogoro ya hapa na pale na kusuguana kwa hapa na pale.
mambo yafuatayo ni muhimu sana kuwekwa wazi kwa wanandoa kwa ajili ya kuimarisha ndoa hasa linapokuja suala la fedha.

Kuwa na Account Moja:
Kitu kikubwa ambacho wana ndoa wapya hukupamba nacho mara wakishaanza maisha pamoja ni jinsi ya kupangilia matumizi ya pesa.
Kama wote mnafanya kazi, je ni muhimu kuwa na account moja ya pesa? au kila mmoja kuwa na account yake then wote kuwa na account ya tatu ya pamoja?

Asilimia kubwa ya wanandoa wapya hufungua Account ya pamoja wakishaoana .

Kitu cha msingi ni kuhakikisha mmekuwa kitu kimoja si katika mwili mmoja tu, bali hata katika pesa.
Kuwa na account moja ni sawa, pia kuwa na account tofauti ni sawa.
Kitu cha msingi ni kuwaelewana juu mapato na matumizi ya pesa zenu na pia malengo ya kiuchumi ya muda mrefu na muda mfupi, kama kuwekeza na akiba kwa pamoja.
Pia kujua aina ya matumizi ya pesa kwa kila mmoja kwani kama mmoja ni mtumiaji na mwingine ni mtu wa kuweka akiba, mnahitaji kujuana ili kusiwe na kinyongo kwa mmoja.

Pia kama mmoja wenu ameingia kwenye ndoa huku anadaiwa na Bank ni vizuri kumjuulisha mwenzake kwani kuoana ni pamoja na hilo deni mnakuwa kitu kimoja.
Kuna wengine wanaingia kwenye ndoa huku tayari walishawekeza kwa ajili ya mke/mume na watoto aliokuwa anatarajia.
Kitu muhimu ni kuwa wazi kuhakikisha mke wako au mume wako anajua.

Jinsi ya Kupambana na Madeni
Katika mambo yote ya pesa katika ndoa, madeni ni jambo linaloongoza kuleta zogo mwenye ndoa na kama hamjafahamishana vizuri inaweza kuleta maafa.
Pia mara nyingi wana ndoa huwa wanatofautiana katika mtazamo kujua lipi ni deni kubwa au dogo hasa kutokana na elimu ya fedha ya kila mmoja.

Hilo ni deni lenu wote hivyo lazima muweke mikakati ya kuondokana nalo kwa pamoja.
Mara nyingi wengi hujiingiza katika deni bila upande mwingine kujua hali ikiwa mbaya ndiyo mtu anaanza kutoa taarifa kwamba ilikuwa hivi na vile huku nyumba inataka kuuzwa au kufukuzwa kazi.
Hapo ndiyo zogo huanza na ndoa huanza kuyumba kwani upande mwingine hujiona hauthaminiwi.

Mmoja kuwa Mtumiaji wa Pesa zaidi ya Mwenzake.
Wanandoa wengi hulaumiana kwamba "wewe ni mtumiaji mbaya kuliko mimi" au kumtuhumu mwenzake kwamba anatumia pesa katika kununua vitu visivyo muhimu katika maisha.

Jinsi ya kutumia pesa huleta maneno katika ndoa nyingi, wapo wanaume akipata pesa tu ni kwenda kununua TV kubwa, Music System na vitu vingi vya starehe wakati mke anataka Pesa ya kununua kiwanja amechoka kukaa nyumba ya kupanga, au mwanamke yeye ni kununua nguo za fasheni mpya iliyoingia mjini hata kama ni gharama kubwa wakati mtoto anahitaji ada ya shule.
Kitu cha msingi ni kuwa na malengo ya muda mrefu na muda mfupi na kwamba kuwa na uelewano wa kujua nini kinunuliwe (bajeti).
Kuvaa ni muhimu na pia kuwa na vitu vya starehe ndani ya nyumba ni muhimu ila kupanga malengo na kuwa na mawasiliano mazuri hilo ndiyo jambo la kwanza.
Kaa pamoja, panga vitu vya msingi,
Tununue nini na kwa nini?
Tuwekeze wapi? na kwa nini?
Tuweke akiba kiasi gani kila mwezi na kwa nini?

Panga pamoja kila mmoja aelewe kwa nini hiki kinafanywa Badala ya hiki.

Kuwekeza kwa Busara na Hekima:
Mustakhabali wa maisha yenu ya miaka 5, 10, 20. 30, 50 ijayo ni sasa na jinsi mnavyotimia pesa na kupanga malengo.
Kuwekeza pesa katika business mara nyingi huwa na risk na risk ikitokea mara nyingi mmoja huanza kumlaumu mwenzake kwamba wewe ndo ulilazimisha tufanye hivyo.

Ni muhimu kushirikiana katika kuweka uamuzi wa pamoja mnapowekeza pesa kwenye miradi au business pamoja.
na piakukubaliana risk yoyote ikitokea pamoja kwani kama ni faida ni yenu wote na kama hasara ni yenu wote.
Katika hali ya kawaida katika ndoa inaonesha kwamba wanaume ndo wanaongoza kwa kujitosa kufanya kitu chochote (business) hata kama kuna risk kubwa baadae na wanawake huogopa sana kuwekeza katika kitu ambacho hawana uhakika.

Kitu cha msingi ukitaka kufanikiwa katika business au maisha lazima uwe risk taker kwani ukifanikiwa unaweza kubadilisha uwezo wa kifehda wa familia yako, ingawa unahitaji kufanya utafiti mkubwa kabla ya kuwekeza pesa zako na uwe na njia ya kupunguza risk inapotokea au Usibebe mayai yote kwenye kikapu kimoja kwani kikidondoka umeumia.

Kutunza Siri zinazohusu pesa
Wengine wanaamini siri za pesa walizonazo bila mume au mke kujuahazina ubaya sana kwenye ndoa.
Ukweli ni kwamba unahatarisha sana ndoa yako kwa kuficha siri za pesa ulizonazo au business unazofanya bila mke au mume kujua.
Wengine wameficha wake au waume fedha walizonazo katika Account walizonazo
Wengine hata wakinunua vitu hudanganya bei waliyonunulia vitu.
Na wengine hujiingiza katika business ambazo mke au mume hajui na huko ikitokea hasara au tatizo ndo hurudi kusema kwa mke au mume, hapo ndo zogo linaanza.

Wengine huwapa ndugu zao au marafiki zao pesa nyingi bila mke au mume kujua na siku mke au mume akijua kwamba mmoja alitoa pesa bila kuambiwa hapo tena moto unalipuka.
Ni muhimu kutoficha siri zozote kwa mke au mume wako kwani lolote linaweza kutokea wakati mwingine hata kifo, utatesa watoto bure kwa kuficha siri muhimu kama hizo ambazo si siri bali jambo muhimu kwa mke au mume wako.

Kupanga kwa ajili ya fedha ya dharura
Wengi hudhani haina haja kuwa na pesa ya dharura
Na wengine hupanga fedha ya dharura kwani chochote kinaweza kutokea, anaweza mtoto kuugua au ninyi wenyewe mmoja kuugua ghafla pia kunaweza kutokea mchango wa dharura bila kujua.
Hata kama una kazi nzuri kama hujajipanga vizuri kwa ajili ya mambo ya dharura unaweza kushangaza mke au mume kwani lolote laweza kutokea.

Matatizo hayataisha hadi tuwe tumekufa, kupangilia vizuri masuala ya pesa kutawezesha ndoa yako kuwa yenye afya na imara.

(1 Timotheo 6:10)
 
Pesa ni kuweka na kuchukua, je wewe ni mtu makini Kuweka au Kuchukua? Hakuna mtu ambaye huwa anaingia kwenye Ndoa huku anajua hiyo ndoa Haitafika mbali.
"Wahenga Walisema Kinga ni Bora kuliko Kuponya".
Jinsi Unavyokuwa na Ufahamu mkubwa wa nini kinaweza kutokea baada ya kuoana hiyo itakuwezesha Kuzuia na Kujiandaa kukabiliana na changamoto zitakazotokea mbele ya safari ya Ndoa.
Matatizo yanayohusiana na pesa yamekuwa chanzo kikubwa cha migogoro ya ndoa nyingi. Matatizo haya huhusika moja kwa moja na jinsi ya kusimiamia na uaminifu katika pesa.

Kama hujaoa/olewa bado unaweza kukaa partner wako mkaongea masuala ya pesa na pia ukapata ufahamu wake kuhusu suala zima la pesa ili mkiingia kwenye ndoa unajua kabisa mwenzangu ni mtu wa aina gani lipokuja suala la pesa na uchumi kwa ujumla.

Na kama upo kwenye ndoa naamini umemchunguza mwenzako na kujua ana tabia ipi likja suala la pesa.
Hapa chini kuna maswali ambayo kama mwongozo tu hasa pale ynapojibiwa kwa ukweli na uaminifu ambayo inaweza kukusaidia kujua mtazamo wa mwenzako kuhusu pesa.

1. Wakati unafanya shopping huwa unafikiria kitu gani hasa?
(a) Vitu unavyonunua.
(b) Pesa unayotumia kununua hivyo vitu


2. Ikitokea mwisho wa mwezi ukapungukiwa pesa hata kama una mahitaji muhimu?
(a) Nafikiria Kukopa
(b) Sinunue kitu chochote


3. Huna Fedha (cash) na unataka kununua vitu na upo mbali na Bank yako utatoa uamuzi gani?
a) Nitatumia ATM card niliyonayo kwenye ATM machine iliyojirani
b) Sitanunua kitu kwani sipendi kutumia ATM card kwani kuna gharama za kutumia kadi


4. Huwa unajisikia una uwezo kifedha pale ikiwa?
(a) Una nunua kile kitu umekuwa unahitaji.
(b) Unapoiweka fedha kama mali (save).


5. Kwa jinsi unvyowekeza sasa na kuweka akiba.
(a) Hujui kabisa ni kiasi gani utakuwa nacho siku ukistaafu kazi.
(b) Unajua kiwango halisi cha pesa utakuwa nayo utakapostaafu kazi.


6. Unapoweka pesa bank kwa ajili ya akiba.
(a) Unajisikia ni wajibu (inaumiza kidogo)
(b) Unajisikia ni raha sana


7. Ukiwa na rafiki zako, unapoongelea masuala ya pesa huwa hukosi kutaja kipi ?
(a) Punguzo la bei uliyopata
(b) Punguzo la mali uliyonunua


8. Kama umepandishwa cheo utasherehekea vipi?
(a) Kwa kununua kitu maalumu kwa ajili yako mwenyewe
(b) Utaruka hewani na kushangilia "waoooooo"

Kama Amejibu kwa kuchagua (a) nyingi basi ni Mtumiaji mzuri wa pesa (Spender) na kama amejibu kwa kuchagua (b) nyingi basi ni mweka akiba mzuri (Saver)


Kama kuna tofauti kubwa yaani mmoja ni mtumiaji na mwingine anapenda kuweka akiba basi uwezekano wa kuwa na migogoro inayotokana na fedha ni kubwa, lakini haina maana kwamba itakuwa migogoro bali changamoto kamili inayokukabili mbele ya safari na unabidi ujiweke sawa jinsi ya kushughulikia Tatizo la pesa ndani ya ndoa.


Na kama partners wote ni Watumiaji; maana yake hakuna atakayekuwa na break ya kuzuia matumizi na matokeo yake mwisho wa njia kunakuwa zogo na matatizo ya fedha kwani mnatumia bila kuwake akiba.
Madeni huumiza ndoa, uwe mwangalifu.

Na kama wote ni watu wa kuweka akiba; hiyo ni nzuri ila mnahitaji wakati mwingine kufurahi kwa kutumia pesa kwa ajili ya just for fun.
Maana mnaweza kujikuta ni mabahiri wa ajabu kiasi kwamba hata raha ya kutumia pesa hakuna.

Kitu cha msingi ni kuhakikisha kila mmoja anamsoma mwenzake kujua mwenzake ana mtazamo gani kuhusu suala la pesa.
na pia kujua ni jinsi gani mnaweza kuhakikisha mnafurahia maisha ya sasa na wakati huo huo mnawekeza fedha na miradi ambayo mbele ya safari mtakuwa na fedha kwa ajili ya kusomesha watoto na hata wakati mkiwa wazee.
Wakati ni sasa usisubiri ukiwa mzee ndo unapanga mipango mikubwa ya kuwekeza anza hata kabla hujaoa au kuolewa.
Kama umeolewa au umeoa; panga malengo, timiza ndoto zako.
Kuwa na ndoa imara yenye afya ni pamoja na kuwa na mafanikio katika Creation of Wealth kwa ajili ya maisha yenu miaka 5, 10, 20, 50 au 100 ijayo
.

 
Back
Top Bottom