Mama'ake anapodandia bili ya mwanawe!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Kazi nzuri tuliifanya mimi na maama'ake
Matunda yake si khaba na mwana tukajaliwa
Ndoa kati yetu tuliiogopa kwani ni ndoana
Mwafaka ukafikiwa wa mgawanyo wa majukumu
Lakini matunzo ni ya mtoto na mama'ake atoka wapi?

Mie jukumu langu lawa ni kubeba gharama
Mzazi mwenzangu kazi yake ni malezi tu..
Baada ya kipindi mwenzangu somo kageuza!
Akidai bila kumbeba na yeye malezi hayawezekani!
Lakini matunzo ni ya mtoto na mama'ake atoka wapi?

Bili ya mtoto yabebeka lakini kero za mama'ake zatisha!
Kwani mtoto hana makuu lakini mama'ake ataka mengi!
Mtoto yeye ni wa kulamba celerac lakini ya mama'ake!
Mama'ake ataka atunzwe akidai bila yeye hakuna malezi!
Lakini matunzo ni ya mtoto na mama'ake atoka wapi?

Baada ya purukushani na kasheshe kibao sasa..
Siri sasa yafichuka na mama'ake kashindwa uteja!
Kumbe mwenzangu ana dongo aona kadhulumiwa!
Anipasha khabari kuwa mtoto ni wa kwangu tu!
Lakini matunzo ni ya mtoto na mama'ake atoka wapi?

Mama'ake apasua jipu kuwa jasho langu ni lake pia!
Adai kama tumeweza kuzaa kwanini tusile wote?
Mie simwelewi kwani mwafaka tuliweka sote.
Yawaje sasa anigeuzie kibao bila ya sababu?
Lakini matunzo ni ya mtoto na mama'ake atoka wapi?

hahahaah yaaan hii kali ,, mama ana taka mbeleko na haki sawa kwa wote? still baada ya muafaka wanawake wengine bana ruta , mkimbieee mtoto niletee mm nitamlea hahaha
 
Mhhh Rutashubanyuma
Wakati sio ukuta
Kujua kuwa moja lahitaji kuisha
Hebu muangalie mamake
Kama unalompa afikisha kunakohusika
Gharama nyingi utabeba
Kama usipokuwa makini
Kujua kuwa malezi nani alea na gharama nani atoa
Na kama gharama ziko kwenye uhalisia
Au zaongezwa kusudi mfuko wako utobboke
 
hahahaah yaaan hii kali ,, mama ana taka mbeleko na haki sawa kwa wote? still baada ya muafaka wanawake wengine bana ruta , mkimbieee mtoto niletee mm nitamlea hahaha

wahida, hilo haliwezekani kwa sababu mtoto amekuwa ni mtaji kwake na hata kazi hataki kufanya tena......................iko shida na kizungumkuti................................na hata akiisoma hii....................i really don't care because I am really fed up with her...................
 
Last edited by a moderator:
Msaidie mwenzako. . .kama hutaki mchukue mtoto umlee wewe.

Lizzy......la kuachia mtoto hataki hata kusikia anachotaka abebwe kwenye mbeleko za mtoto au mtoto atamtesa..................just imagine..............
 
Last edited by a moderator:
Iwe mlienda mahakamani,
au japo mashahidi jirani.
Ikiwa karatasi alisaini
kuwa utampa kiasi gani,
sasa iweje leo azue tafrani?

Mshauri afungue kesi nyengine,
ikiwa ni lazima kile mlichochuma mgawane
lakini sio leo hivi kesho vile. Lazima mkubaliane.
Vyenginevyo, atakuchuna huyo mpaka ukome.

Lakini kabla ya hapo, mburuze mkapime DNA,
isijekuwa anakuchuna kumbe mtoto ni wa mwengine.

Anecdote:
Kuna jamaa alilazimishwa kumlipia mtoto hadi atakapotimia miaka 18.
Siku ya malipo ya mwisho, alimkabidhi "bintiye" kimemo akampe mama yake.
"Hatimaye, haya ni malipo ya mwisho," kimemo kilisema.
Mama akamrejeshea kimemo pia, "Nakushukuru, kwani huyu mtoto hata si wako".

Ruta, chunga sana.
 
Ujumbe huu kwa kweli uwafikie wanawake wote!

Bondpost......popote pale walipo..........................ajue mtoto awe mtoto na mama akae mbali na hilo....................LOL.....tumechoka kubeba mizigo kibao.............
 
Last edited by a moderator:
Iwe mlienda mahakamani,
au japo mashahidi jirani.
Ikiwa karatasi alisaini
kuwa utampa kiasi gani,
sasa iweje leo azue tafrani?

Mshauri afungue kesi nyengine,
ikiwa ni lazima kile mlichochuma mgawane
lakini sio leo hivi kesho vile. Lazima mkubaliane.
Vyenginevyo, atakuchuna huyo mpaka ukome.

Lakini kabla ya hapo, mburuze mkapime DNA,
isijekuwa anakuchuna kumbe mtoto ni wa mwengine.

Anecdote:
Kuna jamaa alilazimishwa kumlipia mtoto hadi atakapotimia miaka 18.
Siku ya malipo ya mwisho, alimkabidhi "bintiye" kimemo akampe mama yake.
"Hatimaye, haya ni malipo ya mwisho," kimemo kilisema.
Mama akamrejeshea kimemo pia, "Nakushukuru, kwani huyu mtoto hata si wako".

Ruta, chunga sana.

MAMMAMIA hawa watu wanajua kututesa...............sasa kama hata mtoto alikuwa akijua siyo wa kwake hiyo dhuluma yote ya nini?................itabidi tuwe tunaenda kufanya DNA kujithibitishia ya kuwa hatubebeshwi mizigo ya watu wengineo...............
 
Last edited by a moderator:
hahahahahaha ,yaaan unanichekesha ile mbayaaa , yaan sijui niseme nn? kwan yumo humu? ktk jf unajua hizo system za ki ulaya mwanamke kuwa more poweful ,,?
 
sasa mtoto akilamba cerelac na maziwa ya kunyonya yatoke wapi!??

Orodha niliyokabidhiwa na mama'ake yadai cerelac, disposable diapers, lactogen........na vikorombezo kibao.............najua vyote hivyo mwanangu hapewi..............lakini vingine nimerundikiwa kukomolewa tu.................just imagine Tshs 700,000/=...................a month and she is still hungry for more........................
 
hahahahahaha ,yaaan unanichekesha ile mbayaaa , yaan sijui niseme nn? kwan yumo humu? ktk jf unajua hizo system za ki ulaya mwanamke kuwa more poweful ,,?

wahida anajua sitaki kufika mahakamani...................naogopa utandawazi na kadamnasi ya macho miamia..........kwa hiyo naye khilo alijua ndiyo maana aja na vitisho kuwa kama hakuna mwafaka wa pili basi atatinga mahakamani.................LOL.............sipati usingizi siku hizi..........
 
Last edited by a moderator:
na mama mtu plzzzzzzz aangaliwe, akiumwa je mtoto akakosa mama, kisa tu hukumhudumia,? jitahidi ruta hudumia wote for the sake of the child.

cacico................huyu mama ni bedui kabisa.......................kwa mwezi anakunja laki saba hivi naye hazimtoshi kweli...................adai mie nakula zaidi lakini jasho langu si ni langu tu?
 
Last edited by a moderator:
ooh so sad ,, jitahidi ,kila kitu kitakuwa sawa mapenz gani hayo sasa , ya pesa kukandamizana kila kitu kina end iko siku maybe ata elewa kuwa sio issue kufanya hivyo
 
Hapo sasa!!
ruta. . .
Ukilea mama ujue ndio umelea mtoto, ila tu asiwe anakulazimisha au anakutumia kupitiliza.

[MENTION]Lizzy [/MENTION]nampa laki saba hivi kweli huyu si ana lake jambo.......................hayo maziwa hawezi kuyapata humo?
 
Back
Top Bottom