Mama watoto kila siku anaota anafanya mapenzi na watu tofautitofauti

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,066
4,085
Mke wangu ana ujauzito wa miezi mitatu, lakini tangu amekuwa na mimba
amekuwa akiendelea kupata hedhi, Pia anaota anafanya mapenzi na watu tofautitofauti kila siku.
Na kuanzia amekuwa mjamzito, nimepoteza kabisa uwezo wangu wa kiume, jogoo hawiki kabisa
 
Atakuwa ana jini mahaba mpeleke kwa Mchungaji/mtumishi wa Mungu anayeamini katika nguvu ya maombi akaombewe. Ni lazima aharibu kotekote kwako na kwa mkeo.
 
Big problem!

Kama hamuamini ktk maombi huu ndo wakati wenyewe, msiende kwa wapunga pepo.
 
Mmeshawahi kuomba kuhusu hilo?? Ur wife needs deliverance from those demons.wanandoa wanatakiwa waombe sana hasa kipindi cha ujauzito maana shetani anatafuta kuharibu kwa kila njia. Mnahitaji kuomba sana otherwise mtampoteza mtoto na ndio itakuwa mmefungua mlango wa matatizo ktk ndoa.
 
Mpeleke kwa gyeno mahiri hilo tatizo la hedhi hutokea sometimes kwa wajawazito. Hizo ndoto mwambie asali kama hajalala bwana, pili acheni kula mivyakula mizigo usiku saa nyingine inamiletea mandoto ya kiaina.

Jogoo hawiki labda unapychological issue, are you sure huna stress. Anza kufanya tizi it helps!
 
Nendeni kwa mganga especially mtoto wa sheikh Yahya Hussein hapo Magomeni bila hivyo matatizo yataendelea kwani si kwa kelele za maombi wala usanii wa kulia na ngoma kwa wingi

Nashauri hata uwe mbali wahi hapo kwa huyo mtoto wa Magomeni ili umaliziwe tatizo lako usidanganywe kwa maombi kwa waombaji wenyewe ni mamluki na wezi na hawana tena nguvu za imani toka kwa Mungu
 
Navyo fahamu mimi kuna wanawake wengine hata kama wana mimba wanapata siku zao, inategema na mimba.

Kuhusu kuota mke wako ana fanya sex na wanaume tofouti, hapo sijui...inawezekana mke wako ana hitajia PSYCHIATRIST EXPERTS.

Kuhusu wewe nadhani unajitisha tu, ondoa wasi wasi vitu vitapiga tu kwenye target...Hata messi jana hakuweza kufunga goli, na ameanza kupata hayo matatizo toka last week, match inayo kuja lazima afunge magoli tu.
 
acha ujinga nenda kwa gyno haraka, hasa hilo la kutoka damu wakati mja mzito sio dalili nzuri, anaweza poteza ujauzito huo.

Japo kuna baadhi ya wanawake wachache ambao hupata hedhi hadi miezi 5 au 6 ya ujauzito.

Kuhusu kuota anafanya mapenzi na watu tofauti inaweza tokana na wewe kushindwa kumkuna kisawa sawa sababu jogoo wako hawiki. Sambamba na jogoo wako kutowika, kuna baadhi ya wanawake hamu ya ngono huongezeka maradufu wakati wa ujauzito au akishajifungua. Inawezekana hivyo vyote viwili vinapelekea mke kuwaza ngono muda mwingi mwishowe anaota.

Ukishaenda hospitali, uchanganye na sala utafanikiwa. Hata tunapokuwa waumini wazuri tutumie na akili za hospitali hata hao madaktari wanatimiza mipango ya Mungu.

Wewe kaka kuhusu jogoo kutokuwika, inawezekana umejijaza hofu ya majini mahaba, hedhi ya mkeo na mimba, utawikaje sasa?
 
Kaka Maombi tu Ndo soln hata Kama mmesali Mara million hakuna kilochotokea, I still say Maombi tu will do, but first advice is, go and have all the hospital answer kuhusu Kupata hedhi etc, jiridhishe kabisa na utaalam Wa kisayansi, baada ya hapo ni Maombi.

Baada ya hapo sasa je waenda ombewa wapi? Wachumgaji Wengi ni wasanii, sijui UPI wapi ila Dar Ni tabu, mapasta Wengi Wa sanii, ila kuna mapasta Wengi Pia Wa ukweli.

Kwepa haya makanisa mapya ya kisanii, mapasta wanajisifu mwanzo mwisho, mchungaji anajiita mheshimiwa , nabii na mtume, huu ni ujinga.

Kupunguza shida na Wasiwasi nenda mkanisa Kama TAG, EAGT, etc, me sipo dar but one the church that I real trust can be of help to you is TAG ubungo.

Pole but I tell you Unaweza kuuamaliza yote hayo na kuishi na Amani na mke wako, na Unaweza haribu Ndoa yako na ukapoteza mtoto wako kabisa na mke wako.

Ahsante.
 
Mwenzangu hivi una chele na hirizi ngapi vile???
Nendeni kwa mganga especially mtoto wa sheikh Yahya Hussein hapo Magomeni bila hivyo matatizo yataendelea kwani si kwa kelele za maombi wala usanii wa kulia na ngoma kwa wingi

Nashauri hata uwe mbali wahi hapo kwa huyo mtoto wa Magomeni ili umaliziwe tatizo lako usidanganywe kwa maombi kwa waombaji wenyewe ni mamluki na wezi na hawana tena nguvu za imani toka kwa Mungu
 
Tumekuwa tukikemea sana na kusali sana, bado ngoma nzito

Unaweza ukawa unasali ila unakuwa hujajenga imani ya kuamini sala yako itaondoa matatizo hayo, kama ulivyoshauriwa nenda kwa mchungaji, kama unaweza na ukienda kuwa na imani kuwa matatizo yenu yataondoka.

hili jini limekasirika labda mkeo kupata mimba na linawaadhibu na msipoangalia atapoteza mimba, cha muhimu kuweni na amani kuwa mtamshinda shetani huyo.

Salini, wekeni biblia kwenye kitanda msali na msali Zaburi ya 91 nayo itawasaidia, kuna nyingi zaidi muhimu kujenga imani ya kuamini kuwa ni Mungu awezaye na all will come to pass.
 
naona umeshauriwa kwenda kwa mganga ila angalia sana waganga nao wanafanya kazi na mashetani, hivyo wanakuonyesha tatizo hili limetoka huku wanakuongezea lingine bila kujijua, na huwa wanasaidiana na kusikiliza mashetani yenye nguvu zaidi yao.

hiyo ndivyo nijuavyo mie.
 
Nendeni kwa mganga especially mtoto wa sheikh Yahya Hussein hapo Magomeni bila hivyo matatizo yataendelea kwani si kwa kelele za maombi wala usanii wa kulia na ngoma kwa wingi

Nashauri hata uwe mbali wahi hapo kwa huyo mtoto wa Magomeni ili umaliziwe tatizo lako usidanganywe kwa maombi kwa waombaji wenyewe ni mamluki na wezi na hawana tena nguvu za imani toka kwa Mungu


Niko confused kabisa, sasa mtu utafute wapi salvation?
 
je unawajua anaoota kalala nao? Na anavyokuhadithia jana nimeota namegwa na fulani unajisikiaje?
 
Back
Top Bottom