Mama wa Watoto 18 Ana Mimba ya Mtoto wa 19

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125


2991294.jpg

Michelle akiwa na mumewe na watoto wao 18
Friday, September 04, 2009 2:27 AM
Mama mwenye watoto 18 ambao wote amewapa majina yanayoanzia na herufi 'J' anategemea kuzaa mtoto wa 19 hivi karibuni. Mama wa watoto 18 Michelle Duggar kutoka Tontitown, Arkansas, Marekani anategemea kupata mtoto wake wa 19 mwezi machi mwakani ikiwa ni wiki chache baada ya kupata mjukuu kwa mara kwanza.

Mama huyo mwenye umri wa miaka 42 pamoja na mumewe Jim Bob ambaye anafanya biashara ya majumba wametengenezewa kipindi maalumu kwenye luninga kinachoelezea maisha yao na watoto wao 18 kinachoenda kwa jina la "18 Kids And Counting".

Bi Duggar alisema kwamba alishuku kuwa ana mimba nyingine baada ya mtoto wake wa 18 mwenye umri wa miezi nane kuanza kukataa kataa maziwa yake wakati alipokuwa akimnyonyesha.

Kwa kutumia uzoefu wa mimba zake zilizopita, alijua kuwa hii ni dalili ya ujauzito na alipofanya vipimo vya ujauzito alirukaruka kwa furaha baada ya kugundua ni kweli ana mimba.

"Tuna furaha kubwa sana" alisema Michelle na kuongeza "Tunasubiria kwa hamu kumuona mtoto wetu wa 19 na mjukuu wetu wa kwanza".

Mtoto wa kwanza wa kiume wa Michelle mwenye umri wa miaka 21, Josh na mkewe Anna, 21, wanategemea kupata mtoto wa kike hivi karibuni.

"Namshukuru mungu, nina miaka 42 wakati nikifikiria kuwa siwezi kupata mtoto tena , mungu ametubariki kwa mtoto mwingine" alisema Michelle.

Michelle na mumewe hivi sasa wanafikiria jina la kumpa mtoto wao wa 19 ambaye atajiunga na familia ya watoto 10 wa kiume na nane wa kike ambapo watoto wote wana majina yanayoanzia na herufi "J".

Ukianzia kwa mtoto wao wa kwanza Josh mwenye umri wa miaka 21, watoto wao wengine majina yao ni Jordyn-Grace mwenye umri wa miezi nane, mapacha Jana na John-David wenye umri wa miaka 19, Jill, 18, Jessa, 16, Jinger, 15, Joseph, 14, Josiah, 13, Joy-Anna, 11, mapacha Jeremiah na Jedidiah, 10, Jason, 9, James, 8, Justin, 6, Jackson, 5, Johannah, 3, na Jennifer, 2.

Matumizi ya chakula na mahitaji mengine ya lazima huigharimu familia hiyo kiasi cha Tsh. Mil. 2.5 kwa mwezi.

Wakati walipofunga ndoa, Michelle na mumewe walikuwa wakifikiria kuwa na watoto wawili au watatu tu.

Lakini baadae kutokana na imani yao ya kikristo waliona ni bora wamuachie Mungu aamue wawe wana watoto wangapi.

Habari Zaidi bonyeza hapa Website ya huo Mama >http://www.duggarfamily.com/photos.html
 
Huyu mama na mumewe wamebarikiwa na wanatimiza kivitendo ule mstali unaosema:

"Mungu akawabarikia, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi..."
Mw1:28
 
As long as wanaweza kuwatunza watoto wao bila kutegemea misaada, waacheni wapet watoto. hata mimi nilitaka niwe na watoto 20plus lakini uwezo unanibana na kuniacha niwe na watatu tu. Hebu angalia jumba lao: externally simple, but internally beautiful.


Nyumba yao kwa nje

14662_225.jpg


14662_211.jpg




Jikoni:
14662_156.jpg



14662_024.jpg

(b) Living Room

14662_157.jpg



(c) Sehemu ya Makulaji

14662_161.jpg



14662_164.jpg


14662_021.jpg


14662_172.jpg


(d) Sehemu za burudani

14662_197.jpg


14662_203.jpg


14662_046.jpg


14662_038.jpg



14662_143.jpg


14662_054.jpg



Chumba cha kulala wavulana

14662_064.jpg




Chumba cha kulala wasichana

14662_076.jpg



Chumba cha wazazi

14662_129.jpg





Chumba cha kufulia nguo

14662_011.jpg




Chumba cha kutunzia nguo (closet) Familia nzima inatumia closet moja:

14662_136.jpg



Halafu wanapata muda wa kuwa na good time kama family:

14662_214.jpg



Acha jamaa wajidai. Hata wakifikisha watito hamsini, as long as wanaweza kuwalea vizuri kama picha hizo zinavyoonyesha, basi hiyo itakuwa ni tahawabu kubwa sana.
 
Dah! inafurahisha kwa kweli!wamebarikiwa sana,ni wachache wanaweza kufikia achievement kama hiyo hasa kiuchumi na uwezo wa mama kiafya kuhimili hiyo mikiki ya watoto 18 na mwingine anakuja.
 
Back
Top Bottom