Mama wa Taifa Hili ni Nani?

Fredrick Sanga

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
3,153
697
Nasikia kuna issue ya mababa wa mataifa, lakini sijawahi kusikia ma-Mama wa mataifa, Mbona hakuna Gender Balance. Mama wa taifa hili ni nani?:spy:

Samahani kama nimewaudhi, akina mama
 
hiki siyo cheo/nafasi iliyotajwa kikatibali bali ni jinsi anavyokubalika katka jamii kwa ujumla.
 
Hivi kukiwa na baba wa taifa lazima kuwe na mama wa taifa? Sidhani! Baba wa taifa ni mwanzilishi wa taifa (founder of the nation). Ni wazi founder akiwa mwanaume ataitwa baba wa taifa; na iwapo ni mwanamke basi ndo atapewa heshima ya Mama wa taifa.

Kumbe si busara kuichukulia hiyo expression "kindoa-ndoa" kwamba kwa kuwa kuna baba wa taifa lazima awepo pia mama wa taifa. Haya ni mawazo yangu tu mazee.
 
Nasikia kuna issue ya mababa wa mataifa, lakini sijawahi kusikia ma-Mama wa mataifa, Mbona hakuna Gender Balance. Mama wa taifa hili ni nani?:spy:Samahani kama nimewaudhi, akina mama

Tukifanya kama unavyotaka wewe na wengine wataanza kuuliza Bibi wa Taifa, Babu wa Taifa, Kaka wa Taifa, Dada wa Taifa, Mama mkwe wa Taifa, Baba Mkwe wa Taifa, Shemeji wa Taifa, Wifi wa Taifa etc. Je haya ndiyo unayo advocate?! Kweli akili nyingi huondoa Maarifa.
 
Kama Baba wa taifa ni Mwl nyerere mama wa Taifa ni Mama Maria Nyerere si ndio alikuwa mke wa baba wa Taifa.
 
Mwishoni utauliza mjomba wa taifa; shangazi wa taifa n.k. Iwapo hujui falsafa ya mtu kutambuliwa kitaifa na kupewa heshima si uliza kwanza? Kuitwa baba wa taifa sio Cheo hadi utake gender balance!!! Bado tuna safari ndefu!!
 
Back
Top Bottom