Mama wa mtoto aliyedungwa sindano tata aijia juu Muhimbili

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Mama wa mtoto aliyedungwa sindano tata aijia juu Muhimbili
Send to a friend
Wednesday, 15 February 2012 20:59
0digg

James Magai na Geofrey Nyang’oro
SIKU moja baada ya uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), kusema kwamba hauna taarifa yoyote kuhusiana na madai ya mtoto Imrani Iddy kudungwa sindano na kupoteza fahamu kwa miezi sita akiwa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), mama wa mtoto huyo amejitokeza na kupinga madai hayo.
Juzi, uongozi wa Muhimbili ulisema unafanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo na kuahidi kutoa taarifa jana. Hata hivyo, haukufanya hivyo.

Mama huyo, Amina Mwerangi alisema jana kwamba alishatoa taarifa ya maandishi kwa uongozi wa hospitali hiyo na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii lakini anashangaa kwamba hadi sasa imeshindwa kuchukua hatua.
Alisema aliwasilisha barua ya malalamiko kwa Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili na kutuma nakala yake wizarani tangu Januari 10 mwaka huu akielezea tukio la mtoto huyo kudungwa sindano na mwili wake kupooza kwa muda wa miezi sita sasa, lakini hajapata jibu lolote.

Mtoto Imrani amelazwa hospitalini hapo katika chumba cha hicho cha ICU tangu Julai 28, mwaka jana.
Alisema licha ya barua hiyo kuwa ya malalamiko, aliomba msaada wa mtoto huyo kupatiwa rufaa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi, maombi aliyoyafanya kwa muda mrefu bila mafanikio.

“Mimi kama nitakuwa sijapata taarifa zozote kutoka uongozi wa MNH hadi kesho (leo), nitakwenda kumuona Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto anisaidie. Nimefikia uamuzi wa kwenda huko sababu nilishaandika barua kwa uongozi wa MNH na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii lakini sijapata msaada wowote,” alisema.

Alisema kwa sasa hali ya mwanaye bado ni mbaya huku akisisitiza kuwa tukio la kuchomwa sindano kwa mtoto huyo limemuongezea tatizo la pili la kupooza badala ya lile la awali la kuota nyama kwenye njia ya hewa.

Muhimbili, Wizara
Februari 15, mwaka huu Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa MNH, Aminiel Aligaesha alisema tayari uchunguzi wa tukio hilo umeanza na kuahidi kutoa taarifa jana.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda alipoulizwa kuhusu taarifa hizo, alimtaka mwandishi kumtumia swali hilo kwa njia ya mtandao wa wizara ili aweze kuelewa vizuri na kulitolea majibu.

“Swali lako ni zuri sana, unafuatilia kutaka kujua hali ya mtoto na kuokoa maisha yake. Sasa nitumie swali hilo kwenye barua pepe ya wizara ili nilielewe vizuri na nitakupatia majibu,” alisema Dk Mponda.

Afya ya mtoto
Uamuzi wa familia ya mtoto huyo kuitaka hospitali hiyo kutoa maelezo ya kuridhisha, ulitokana na madai kwamba baadhi ya madaktari na wahudumu wa hospitali hiyo walitaka kumrejesha nyumbani mtoto huyo kimyakimya licha ya hali yake hiyo.

Ingawa hadi sasa aina ya sindano aliyodungwa na wala mhudumu aliyemdunga sindano hiyo havijajulikana, inadaiwa kuwa taarifa ya awali ya kitabibu zinaonyesha kuwa mtoto huyo amepatwa na tatizo la mtindio wa ubongo.
Mtoto huyo alifikishwa na kupokewa hospitalini hapo Julai 28, 2011 kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa nyama zilizoota puani na kufunguliwa jalada namba IP.No.A586301.

“Kabla ya upasuaji huo alipatwa na matatizo ya mshtuko wa moyo na tangu wakati huo amekuwa chumba cha uangalizi maalumu hadi sasa,” alisema mama huyo na kuongeza: “Oktoba 3, 2011 tulipokea taarifa ya kitabibu ambayo inaeleza tatizo hilo jipya la mtoto.”

Mama huyo alieleza kuwa mbali na tatizo hilo la kuota vinyama puani, mtoto huyo alifika hospitalini hapo akiwa na afya njema, mwenye uwezo wa kucheka, kutembea, kula mwenyewe na akiwa na fahamu kamili... “Leo hii mtoto hawezi kula mwenyewe, mikono na miguu yake havifanyi kazi ipasavyo
 
Back
Top Bottom