Mama Tibaijuka,Unamjua Bush Mdogo?

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
51,603
68,511
Umofia kwako mama Tibaijuka,nakumbuka ulisisitiza sheria ya kuendeleza makazi ambayo inasema mtu asipoendeleza shamba ndani ya miaka mi3 basi huyo mtu atanyang'anywa shamba/kiwanja!
:focus:
Kuna mtu anaitwa Akbaru(Bush Mdogo),kwanini anaitwa bush mtoto? Huyu jamaa(Muhindi) anamiliki karibia kigamboni nzima(Zaidi ya 50%) cha kushangaza sehemu kubwa huyu bwana ameacha mapori kuanzia kisarawe,lengato,luguruni,lugwadu,mwasonga kote huko anamiliki mapori tena alinunua laki1 na nusu kwa heka! Mama Tibaijuka ebu mfatilie huyu mtu kama hana mpango nayo ayagawe kwa serikali ili waweze kugawa viwanja!! Hawa watu ndio wanaopandisha bei za viwanja kwa kuhold maeneo makubwa wao na kuacha tugombanie vipande vidogo kwa hela nyingi mfano viwanja vya geza viwanja 1800 waombaji 120,000.

Nawasilisha.
 
ccm na sera ya MWENYE PESA KWANZA!usitegemee mwananchi maskini kupata kiwanja kwa bei nafuu wakati KUNA MTU AMESHATANGULIZA PESA KWANZA!!
 
Mama Prof Anna Tibaijuka na Dr.Faustine Ndungulile mmefikia wapi kuhusu huyo jamaa? Kumiliki sio dhambi tatizo hayaendelezi kila sehemu ukitafuta kashamba ka kulima mihogo unaambiwa ni la Akbaru,sasa sie wajasiliamali wa ukulima tuende wapi? Kama hayaendelezi agawe kwa wananchi walime.
 
Mh. Lukuvi na Makonda,Eneo mliopewa/mliomnyang'anya Akbaru vipi? Mshagawa maeneo ya wajasiliamli kujenga viwanda vidogo vidogo?
 
Kule Lugwadu na Magodani kuna Mgogoro mkubwa sana,Serikali ya Kijiji iliamua kuchukua Pori la huyu jamaa na kugawia Wananchi ambalo halijaendelezwa tangu alipolinunua 1980s sababu hili Pori lilikuwa kitisho cha Usalama kwa Wakazi wa maeneo yale maana watu wengi walikuwa wanauawa na kubakwa. Cha kushangaza hili swala limefikishwa sehemu husika mpaka leo wanapiga danadana sababu kuu jamaa kila sehemu kamwaga mpunga wa kutosha na hutaweza kumsikia Lukuvi akitia neno.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom