Mama Tibaijuka, naongeza ushauri wangu kuhusu uboreshwaji wa jiji la Dar

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Nilibahatika siku moja kumsikiliza mama Tibaijuka katika kipingi cha dk 45 cha ITV. Kwa kweli alipoelezea mpango wa 'kuifumua' Dar na kujenga mji wa kisasa wa 'magorofa', niliona kama alikuwepo kwenye mawazo yangu. Kama kweli kama alivyosema mama huyu kuwa mpango huo utapelekea kujenga nyumba za magorofa kwa ajili ya makazi wakianza na maeneo yaliyo mjini zaidi kama Magomeni, Manzese, Ubungo, Tabata n.k. then hilo ni wazo zuri sana. Siku zote ambazo mi niliwahi kuwaza juu ya kufanyiaka kitu kama hicho, niliwaza kipangiliwe kama ifuatavyo;

1. Kabla ya kuwahamisha wakazi wa maeneo hayo, serikali ijenge kama 'stabilization houses' maeneo fulani pembeni na mjini, ambapo ardhi itapatikana. Maeneo haya yawe na uwezo wa ku-accommodate angalau watu elfu 5 kwa wakati mmoja. Idadi hii ya watu, itafanya huduma zozote za kijamii zitakazoambatana na eneo hilo ziwe economically viable. Nyumba hizi zitatumika kwa ajili ya kuwahamishia kwa muda wakazi wanaoishi eneo linalotakiwa kushughulikiwa kwa wakati huo. Wazo la kuwafidia then, kuwataka wakatafute makazi sehemu nyingine, litazua mdahalo na hali ya kutokukubaliana, tena litawapa mafisadi chance ya kuchakachua fidia.

2. Wamiliki wa nyumba na wakazi waliohamishwa kutoka eneo fulani, ndo watakaokuwa wa kwanza kupewa nyumba na vyumba miongoni mwa zitakazojengwa baada ya kukamilika

3. Suala la sewage channels, Barabara, rest places, breathing spaces, public areas kama viwanja, shule n.k vipewe kipaumbele sana. ninaamini kama mpango wa kujenga utakuwa mzuri, kwa kujenga magorofa, then idadi ya watu wanao-occupy eneo moja kwa sasa inaweza kuongezwa hata kwa ratio ya 1:10. Kwa maana hiyo maeneo yatakuwa makubwa na yatatosha kwa matumizi mbalimbali

Najua kuwa kama kweli serikali imedhamiria kuboresha miji yake, then watakuwa na mipango mizuri katika kuyafanya hayo...
 
Kwa sababu jamii nzima imeoza na kila mtu anataka kufanya yake, no matter how good huyu prof yupo, hawezi kufanikiwa. Atakosa support kutoka kwa watu muhimu since almost all of them ni 10 percenters!
 
Kwa sababu jamii nzima imeoza na kila mtu anataka kufanya yake, no matter how good huyu prof yupo, hawezi kufanikiwa. Atakosa support kutoka kwa watu muhimu since almost all of them ni 10 percenters!

mkuu hilo ni kweli kabisa, hapo kila mtu atafikiria atapataje cha juu na sio wananchi watanufaika vipi!!:twitch:
 
Namkubali Sana huyu mama me naona anafaa kuwa rais was Tanzania abomoe vijumba vyote vya kijingajinga tujenge mijengo ya maana
 
Back
Top Bottom