Mama Terry yuko wapi?

JituParaTupu

Member
Nov 20, 2008
92
9
Wakuu,
Nisaidieni kujua huyu mama Terry kwa sasa hivi yuko wapi? Na nini kilitokea mpaka akapotea kabisa kwenye publicity.
Nawasilisha...
 
Nadhani Joyce Mhavile wa ITV anajua kilichomsibu na alipo sasa huyu mama.
 
Nadhani Joyce Mhavile wa ITV anajua kilichomsibu na alipo sasa huyu mama.

MSANII, NA DMAUJANJA,
Kwani Joyce na Misanya wanahusikaje na maisha ya binafsi ya Mama Terry?

Hata mimi ninashauku kujua aliko mama Terry na kulikoni ukimya huu.
 
Alikuwa Marekani kwa muda mrefu akarudi kama miezi miwili iliyopita. Nilimwona karibu na nyumbani kwake maeneo ya Bahari Beach kipindi hicho.
 
’’nitajitahidi katika wiki mbili zijazo kuchapisha ratiba inayoonyesha namna nzuri ya kula chakula kwa mtu aliyeathirika na ukimwi,’’ mama terry gbemudu (2005) http://www.habaritanzania.com/new/articles/273/1/msiwanyanyapae-wanaoishi-na-( vvu--mengi (08/1/2005)
" wa kwanza kunasa katika mtego huo ni mama terry gbemudu ambaye alikuwa mmoja wa wagombea ubunge katika jimbo la kigamboni.

mama huyo ilikuwa aitwe kwenye kikao maalum na kuwekwa kitimoto lakini bahati yake akili ikawa imemcheza mapema na kuandika barua ya kuiangukia ccm kutokana na maneno aliyoyatoa". (mike williams, 2005http://www.habaritanzania.com/new/articles/359/1/zengwe-jipya-laibuka-ccm )






jamani wapi huyu mama aliyekuwa makini enzi zile za itv na redio wani ya akina mishanya bingi???.

 
yadaiwa hyu mama ni wa ta, (waondoka leo waja leo) ni wale wa "korogwe girls!!"

alipata kuolewa na mnaigeria fulani aitwae gbemudu na miaka ya kati 1990's hivi huyu mnaigeria aliondoka tz. Haileweki what went wrong on the family na kama bado mahusiano yapo.

umahiri wa huyu mama kwenye vita dhidi ya "ngoma" na ujasilimali ulikuwa kiboko!!!.

wapi mama terry????
 
nakumbuka akiongelea matunda yaliyobakwa! du alikuwa mkali kweli...
wadau, kapotelea wapi kweli!??
 
Eliachim simpasa,

Mbunge wa zamani wa jimbo la mbozi mashariki alikuwa ni mwenyekiti wa kamati ya maadili ya bunge. Mama terry alisema kuwa dodoma huwa kunajaa machanguadoa kipindi cha vikao vya bunge, na baada ya bunge kumalizika machangu wanarudi jijini. Hakusema kuwa wabunge wanatembea na machangudoa.

Aliachim Simpasa, kwa madaraka aliyokuwa nayo alimwita Mhavile na Mama Terry na kuwahoji kwa zaidi ya masaa matano. Aliwatuhumu kuwa mhavile amemruhusu Mama Terry kuitumia Radio 1, kulidhalilisha bunge na wabunge.. Mama terry alituhumiwa kuwatukana wabunge na kuwakosea heshima.

Baada ya hapo Mhavile aliambiwa mama terry asiguse tena radio 1.. Na sauti yake ikisikika tu... Ndio ungekuwa mwisho wa kituo hicho cha radio.
Kuanzia hapo mama terry hatukusikia tena...

Kuna wakati zikaja taarifa zake kupitia magazeti kuwa mtoto wake amewakamatishia watu mbwa... Mbwa wa mama terry wameng'ata na kujeruhi....
Kesi ikawa kesi......

Hadi leo tunajiuliza muelimisha rika wetu huyu wa juisi za maganda ya viazi yuko wapi??Mwenye jibu atumwagie uwanjani..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom