Mama Shelukindo atimuliwe CCM mara moja

Kilichopelekea mpaka baraza la mawaziri kuvunjwa na kuundwa jipya ni nani kama si wapinzani??? CCM ni bendera fuata upepo! Alichoonyesha muheshimiwa Shelukindo ndio demokrasia ya ukweli na sio ile ya wabunge wa CCM kila hoja inayotolewa na wapinzani kwao hawaitaki halafu saa ya mwisho yule bibi akishaanza kusema wanaounga hoja? CCM ndioooooooooo!!! Shame on you MAKUPA!
 
Wabunge wote wa CCM wangekuwa kama mama Shelukindo, tungekua na bunge zuri sana na maendeleo yangekuja kwa haraka.
 
Kitendo cha Mama shelukindo kusifia wapinzani bungeni na kukosea heshima chama kilichompeleka bungeni, hivyo anastahili kutimuliwa sio siri hawa ndio wale waasi tulionao ndani ya chama

Hili nalo ni kosa la kumfukuzisha mtu chamani? Kweli wanaCCM DHAIFU.
 
Kitendo cha Mama shelukindo kusifia wapinzani bungeni na kukosea heshima chama kilichompeleka bungeni, hivyo anastahili kutimuliwa sio siri hawa ndio wale waasi tulionao ndani ya chama


Hizo siasa ndio zimetufikisha hapa tulipo.kama watu wanasema mambo ya msingi kwa nini asiwasifie?kwenye ukweli acha watu awaseme.magamba mezowea kuukataa ukweli siku zote zama hizo zilishaisha siku nyingi.kama hujui hiyo ndiyo ilivyo mkuu.
 
Naomba nifafanuliwe maana ya neno DHAIFU,maana linanichanganya sana,kila nikiangalia kuanzia ngazi za juu serikalini,kwenye mashirika ya umma naona mambo hayaendi ,je kuna kozi fulani viongozi hawa wanaichukua inayoitwa DHAIFU au ni nini? maana mambo yanafana fanana????????????????????????????????????
 
Mama shelukindo anafanya booking mapema ya kuhamia basi kubwa koz amechoshwa na hilo lori la uchafu wa manispaa (CCM).
 
Kwa kusema ukweli ndo ufukuzwe chamani? Mfukuzeni muone. Kama anaongelea maendelo ya wananchi halafu chama kimwajibishe, wapiga kura watamrejesha tu bungeni. Hongera Mh Shelukindo na wabunge wengine wa CCM kwa kuthubutu kusema ukweli mnao amini kuliko wale wanaponda BAJETI yote halafu mwisho wanamalizia kuunga mkono 100% huu sio wakati wa Chama kushika hatamu, tunataka wabunge watetee maslahi ya umma siyo ya watu wachache.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom