Mama Shelukindo atimuliwe CCM mara moja

Mh. Beatrice Shellukindo amepelekwa Bungeni na wananchi wa Kilindi na siyo CCM. Waliopelekwa Bungeni na CCM ni kama Zakhia Meghi, James Mbatia, Easter Bulaya, Wanawake na Maendeleo (jina limenitika) na wengineo

Ha ha ha,eti wanawake na maendeleo! Anaitwa ViCky Kamata!
 
Tatizo la CCM haipendi kuambia ukweli hata pale inapoona kuwa tunachokifanya sicho cha manufaa kwa wananchi, na sikuzote ukweli huwa unauuma, na penye uongo ukweli hujitenga?

Alichokifanya huyu mama ni kitend cha ushujaa hasa kwa magamba ambao huwa hawataki kukosolewa, amesoma alama za nyakati na ameona mbele. Anajua wazi kuwa chama chake kimepotoka na wanaopata tabu ni mabosi zake (wananchi waliomchagua kuingia bungeni) huko vijijini bajeti ya mwaka huu haiwanufaishi kwa chochote. Ameelewa bajeti ya mwaka huu 2012/13 ni bajeti ya waishio mjini na yenye kuongeza matabaka ya wenyenao na wasiyonayo.

Ushauri wangu wabunge wakiwa ndani ya bunge wakumbuke kuwa mabosi zao ndio wanataabika vijijini waacha ushabiki usiokuwa na tija wala maendeleo kwa wanachi wao.
 
Kitendo cha Mama shelukindo kusifia wapinzani bungeni na kukosea heshima chama kilichompeleka bungeni, hivyo anastahili kutimuliwa sio siri hawa ndio wale waasi tulionao ndani ya chama

....kwli watz bado fikra ni mgando!kweli kijana na akili zako timamu unaweza kuongea huu ujinga?i wonder!
 
mama sherukindo anafaa kucheza timu nyingine CCM hatakiwi...........kusema rahisi kutawala sio rahisi.

Lowassa at work.........
 
Kwa kile kisicho tegemewa na wengi bungeni katika uchangiaji wa bajeti ya serikali 2012/2013.

BEATRICE SHELUKINDO( CCM) alitumia muda huo kuwapongeza wapinzani kwa bajeti nzuri na yenye malengo ya kuirekebishe serikali.
Nukuu " Nawapongeza wapinzani kwa kuandaa bajeti yenye malengo ya kuikosoa na kuirekebisha serikali,lazima tukubali tumefika hapa tulipo kwa ajili ya watu wachache, ni nani aliye ruhusu nyumba za serikali kuuzwa?"

Aliendelea kuwafunda wabunge wa ccm(dhaifu) kwa kuwambia wapinzani wanawatakia mema ndio maana wanawambia ukweli ili wajirekebishe.

Na hii iliendelea kuupamba ukweli wa mnyika kwamba " jk ni dhaifu" ndio maana mbunge huyo mzalendo aliwataka ccm(dhaifu) wakubali kuambiwa ukweli. Kwani yeye alikubali ukweli huo.

Shelukindo aliendelea kuwapa ukweli wabunge wa ccm(dhaifu) kuwa waweke maslai ya taifa mbele siyo chama kwani wananchi wanataka maendeleo.

Kwa maneno ya mbunge huyu mzalendo alionekana kukerwa na kitendo mwigulu nchemba( mzee wa fumanizi) kuchana bajeti ya upinzani, kwani alisema nchi hii ina wachumi anawaomba watusaidie kuliokoa taifa, na hili lili kuwa dongo kwani alikuwa anajua nchemba hana mchango wowote kwa taifa pamoja na kujiita mchumi.

Kweli shelukindo alionesha uzalendo wa hali ya juu ambao haukutegemewa na mafisadi wa chama dhaifu hasa Ngeleja alio lipa taifa zawadi ya giza kwa muda mrefu.

"WATANZANIA WA LEO SIO WATANZIA WA ENZI ZA ASP"
 
Mawazo Mgando Hivyo ndiyo vitisho mnavyowapa wabunge wenu hivi wanawakilisha chama au wananchi waliowachagua?Ndiyo Maaana Mwenyekiti yupo Dodoma Kuwatisha ili wapitishe bajeti?
 
Kitendo cha Mama shelukindo kusifia wapinzani bungeni na kukosea heshima chama kilichompeleka bungeni, hivyo anastahili kutimuliwa sio siri hawa ndio wale waasi tulionao ndani ya chama

Hivi na wewe unajua kazi za Mbunge???. Hivi kazi za mbunge ni kusifia chama?? Umesoma chuo gani we mwenzetu.??
 
Ukweli unaumiza, ccm inabidi kujenga utaratibu wa kukubali kuambiwa ukweli
Kitendo cha Mama shelukindo kusifia wapinzani bungeni na kukosea heshima chama kilichompeleka bungeni, hivyo anastahili kutimuliwa sio siri hawa ndio wale waasi tulionao ndani ya chama
 
Kitendo cha Mama shelukindo kusifia wapinzani bungeni na kukosea heshima chama kilichompeleka bungeni, hivyo anastahili kutimuliwa sio siri hawa ndio wale waasi tulionao ndani ya chama

Makupa kumbe huna akili kiasi kikubwa kama hiki ? Membe kasema Wapinzani ni kwa mujibu wa sheria nawe wajua .Membe hivi vyama ni vyetu sisi wote maana viko Tanzania .Vyama hivi vyote vinaililia Tanzania tofauti na nyie CCM .Ujinga huu wa mawazo ya juzi umeutoa wapi ?
 
atimuliwe livingstone lusinde, yeye hana hoja ni kuiaibisha ccm kwa kutoa matusi tu. Mama Shelukindo kaza mwendo achana na makanga boya
 
Yeah i think makupa hakuwa na cha kusema,but since you are free to air your views then yuko sahihi kabisa,kwendana na fikra zake nadhani umenena bwana Makupa
Keep it up
 
atimuliwe livingstone lusinde, yeye hana hoja ni kuiaibisha ccm kwa kutoa matusi tu. Mama Shelukindo kaza mwendo achana na makanga boya
 
Kama alivyosema Chinua Achebe "hamkani si shwari tena" - no longer at ease. Bila shaka kuwa ndani ya CCM nyakati hizi ni changamoto kubwa sana kwa makada hasa wenye upeo mkubwa wa kufikiri na kutafakari. Wana machaguo matatu tu yafuatayo:

  1. Kutetea chama kinachoendeshwa na viongozi waliodhamiria kugeuza nchi shamba la bibi na kutumia kila aina ya ulaghai kupumbaza wananchi - uonekane ama mnafiki au mwendawazimu
  2. Kukosoa mwelekeo huo unaoliangamiza taifa waziwazi - upewe nembo ya msaliti (aka kinyago, oil chafu, n.k.)
  3. Kukaa kimya na kuisotesha dhamiri yako na kufanya hadhi yako ihojiwe na jamii ya watu makini

Hakika, huu si wakati muwafaka kuwa kada wa CCM. Sishangai wakongwe wengi ndani ya chama (toa Wassira) wakiamua kuwa kimya kabisa au kutoa kauli za kisisasa kwa tahadhari kubwa.
 
Kitendo cha Mama shelukindo kusifia wapinzani bungeni na kukosea heshima chama kilichompeleka bungeni, hivyo anastahili kutimuliwa sio siri hawa ndio wale waasi tulionao ndani ya chama

Tatizo Chama chenu Kumepeleka wabunge wengi Wa Kuzomea na kushangilia tu!! Sasa huyu mama amejipambanua kuwa yeye sio mtu wa type Hiyo!! Hivyo Yuko tayari kwa lolote!! Na hakika nakwambia Hamwezi kumfanya lolote!! Pia ungekuwa na busara wewe mleta Hoja Ungependekeza Badwell - Bahi ndio afukuzwe kwani ndio ameabisha Chama Hadi Aibu!!

Mama Shellukindo Kanyaga Twende!!
 
Ndo maana chama chenu kinazidi kudidimia kwa sababu ya kukumbatia uongo na majungu,mama Shelukindo hawajibiki kwa chama,anawajibika kwa watanzania waliompa dhamana,hataki kuwa mmoja wa wachafu,hana udhaifu na upuuzi wa ki CCM! yatawabana sana magamba hayo!
Zidumu fikra dhaifu za kikwete. zidumu
 
Kitendo cha Mama shelukindo kusifia wapinzani bungeni na kukosea heshima chama kilichompeleka bungeni, hivyo anastahili kutimuliwa sio siri hawa ndio wale waasi tulionao ndani ya chama

Tofauti baina yako wewe na kina Nchemba; Ngelenja, Anne kilango and other psycophants and praise singers ni kwamba Mh. Beatrice Shelukindo yuko objective, chepeo analiita chepeo na wala sio kijiko kikubwa kama nyie wengine. yeye amejipambanua na wana CCM wengine kwamba haichukulii siasa kama proffesion bali utumishi wa umma. nonetheless if the likes of you can not change, then change will change you, and beleive me you; it is just around the corne.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom