huyu mama huwa simuelewi kabisa
hivi kweli imegusa maeneo yote? Rasimu hii na ya tume ya warioba ipi imegusa maeneo mengi?
Kwani lazima rais aongee kwa niaba ya chama? Makamu m/kiti, katibu mkuu, katibu mwenezi na viongozi wengine wa chama wasio na madaraka yeyote wana kazi gani? Yeye kama mwenyekiti tunakubali akae kwenye vikao vya chama wakubaliane watakavyokubaliana ila hizi kazi za PR awaachie hao wengine.Watu wahamasishwe tu kujitiokeza kwa wingi kupiga kura na viongozi watendaji wa serikali na dini.
Lakini viongozi wa vyama vya siasa akiwemo huyu mama ruksa kueleza wanataka watu wapige upande gani.Huyu mama si kiongozi mtendaji wa serikali au dini ni mwana CCM na kiongozi katika chama cha mapinduzi ana haki kuongea hivyo.
Ila nadhani kuna tatizo la viongozi hasa wa dini kuchanganya mambo kisa eti wamemsikia raisi kasema watu wapige kura ya ndiyo.Raisi ni mwenyekiti wa CCM taifa.Akiongea mambo ya kutaka watu wapige kura ya ndiyo anaongea msimamo wa chama chake yeye akiwa kiongozi wa chama.
Lakini inapofika askofu ambaye anaongoza kanisa lenye wanachama wa UKAWA ,CCM na wasio na vyama naye akajitosa eti kupigia debe eti kura ya ndiyo au hapana hapo anakuwa hajui vizuri kazi yake kama kiongozi wa dini kwa waumini wake wenye vyama tofauti na misimamo tofauti ya kisiasa.Maaskofu ni vizuri wabakie kwenye majoho yao siasa wawaachie waumini.Askofu awaambie tu waende kupiga kura kwa kadri ya dhamiri zao kisha aendelee kuwaswalisha wakishatoka kupiga hiyo kura sawasawa na dhamiri zao.