JokaKuu
Platinum Member
- Jul 31, 2006
- 30,441
- 55,018
Chifu Ihunyo,
maana yangu ni kwamba mumetumbukia katika mtego wa wana-mtandao. mtego wa kulaumu wengine kwa uzembe na ubadhirifu wa Jakaya Kikwete.
Ninavyoelewa mimi, Mama Kikwete hawezi kutumia hiyo ndege bila ruhusa ya JK. Gharama za first lady ziko chini ya mfuko wa ikulu, ambao mdhibiti wake ni JK.
Kuna maana kubwa sana kuwa kiongozi wa kuchaguliwa. Maana yake ni kwamba unawajibika moja kwa moja kwa wananchi na kulinda maslahi yao.
Mara nyingi nimeona watu wakiwahifadhi mawaziri na kutaka watendaji wa chini yao mf.,makatibu wakuu wawajibike badala yao. Ubadhirifu umefanywa na ofisi ya Raisi na anayepaswa kubeba lawama ni Raisi.
Mwisho, nilipinga vikali ziara hiyo kwamba maudhui yake yanaathari kubwa kwa maendeleo ya mtoto wa kike. Kwa ujumla kilichoendelea pale ni mila potofu.
Wako wale walionipinga na kudai ngoma zile ni moja ya jadi zetu hapa tanzania na tunapaswa kuzitukuza. Ukichunguza Tanzania maeneo yanayoendekeza sana unyago na watoto wa kike kuchezwa ngoma yamebobea katika utoro watoto wa kike shuleni.
Raisi Mkapa aliumbuka alipopewa takwimu za watoto walioachishwa masomo na kufungishwa ndoa Mtwara ambao ni mkoa kinara wa ngoma za unyango.