Mama Rwakatare, Meya Kimbisa, Sofia Simba...

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Meya Kimbisa na Sofia Simba sasa wameamua kuokoka na wanasali kanisa la Mama Rwakatare, hivi hii ni serious issue au kuna issue nyuma ya pazia?
 
Meya Kimbisa na Sofia Simba sasa wameamua kuokoka na wanasali kanisa la Mama Rwakatare, hivi hii ni serious issue au kuna issue nyuma ya pazia?

Tell us Pimbi, what do you think and who can think on their behalf?
 
Jicho leo hii limeshuhudia Mh Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Utawala Bora Mh Sophia Simba katika ibada ya maombezi pale Mikocheni B Ass of God kwa Mch Rwakatare,

Mh Simba alipata maombi ya nguvu toka kwa waumini wote yakiongozwa na Mch Dk Rwakatare na mara baada ya kuombewa alijumjuika na wakristo ama walokole katika ibada ya kusifu na kuabudu ambapo alikuwa akifuatisha vyema nyimbo zote pamoja na kunesanesa ama kucheza kama wafanyavyo waumuni wengine wa makanisa haya ya pentekoste.

Hapana shaka hii haitakuwa mwisho kwa Mh Simba kuudhuria ibada mahali pale kwani ameoneshwa kukunwa sana na maombezi yale, ingawa sina hakika kama atakubali kumpokea Bwana na kuwa Mwokozi wa maisha yake.

Ubarikiwe sana Mh Simba.

Unajua, Ndugu yangu, RMashauri Huyu mama Rwakatare na Sophia Simba wanawaangusha sana wanawake Tanzania na dunia nzima. Si Rwakatare wala Sophia Simba anaweza kujigamba kuwa ni mfano bora wa mwanamke wa Afrika. Tunahitaji sura nyingine kabisa za wanawake ambazo ndizo zitakuwa mfano wa bara letu, ambalo wanawake bado wako nyuma.

Rwakatare na Sophia Simba wanaitumia nafasi hiyo vibaya sana, wakielewa wazi kuwa kuna pengo kubwa hasa katika nyanja hizo, Dini na Siasa.

Tukirudi kwa Rwakatare, huyu si mtumishi wa Yesu wala Mungu, kwa hili ninahakika kabisa. Huyu mama anatafuta pesa, na amezipata kwa kutumia jina la Yesu. Na amini usiamini, lakini wateja wake anaowaota usiku ni hawa wenye pesa kama Sophia Simba na si wale wenzangu walala hoi wanaokwenda kwake bila pesa. Hao huwatumia kujaza kanisa na kujitangaza tu. Sikiliza maneno yake yalivyojaa vishawishi vya kiuchumi.

Sophia Simba ni Msema ovyo, aliyebahatika kupata vyeo zaidi ya uwezo wake kwa kubahatisha kutumia ukichaa wake kugusa hisia za watu waliochoshwa na mafisadi wanaume. Swali linalotawala hapa ni MARA NGAPI ATAWEZA KUBAHATISHA KUCHAGUA NAMBA 6 KATIKA NDOO ILIYOJA VIKARATASI VYENYE NAMBA 35 MILIONI.

Jibu la swali hilo ni ngumu, na wengi wanadhani ni MLEMBE au Rwakatare. Well, time will tell!

Tupe chanzo cha habari yako hii?
Malila, as quoted above, issue ya Mama Sofia haikuwa ngeni, lakini jana nilimwona hata Kimbisa kanisani akitoa ushuhuda. Sina tatizo na kuwa muumini wa kanisa hilo na wengine wengi (wanasiasa) niliowaona ambao walikuwa wakitoa shuhuda zao na kupewa fursa za kunena mbele za madhabahu, wasiwasi wangu ni kama wamedhamiria kweli toka kwenye mioyo yao, kama ni kutoka moyoni basi watenda vema, kama wanacheza deal wajue wanacheza mchezo wa hatari ambao kinyume chake wanaweza kukabiliana na balaa kubwa hapo mbeleni na sishauri wala sitamani kuona wengine wakifanya usanii kupitia njia ya imani/dini.

Mkuu Ibra, kama nimekosea basi samahani mkuu wangu. Naomba kama topic inakugusa kwa namna moja ama nyingine au imekukera wafahamishe mods wafute kabisa. Nimeianzisha kwa wema kabisa mkuu wangu
 
Meya Kimbisa.....eamua kuokoka na wanasali kanisa la Mama Rwakatare, hivi hii ni serious issue au kuna issue nyuma ya pazia?

hivi unawajua vizuri wanasiasa wewe? makamba hujawahi kumuona makanisani?

kwa taarifa yako, inawezekana hakuna aliyeokoka hapo, hata rwakatare mwenyewe. we subiri tu utaona
 
Wanasiasa ni viumbe wa ajabu sana, wanaweza kufanya vituko ilimradi vinawapatia kura!! Juzi juzi nimensikia Lyatonga Mrema akiwa anahojiwa pale TBC wakiwa na Lipumba ananukuu aya za Q'oran tukufu kwa kiarabu; Lipumba alishindwa kujizuia ikabidi acheke !!

Thi is the extent politicians can go in search of votes.
 
Malila, as quoted above, issue ya Mama Sofia haikuwa ngeni, lakini jana nilimwona hata Kimbisa kanisani akitoa ushuhuda. Sina tatizo na kuwa muumini wa kanisa hilo na wengine wengi (wanasiasa) niliowaona ambao walikuwa wakitoa shuhuda zao na kupewa fursa za kunena mbele za madhabahu, wasiwasi wangu ni kama wamedhamiria kweli toka kwenye mioyo yao, kama ni kutoka moyoni basi watenda vema, kama wanacheza deal wajue wanacheza mchezo wa hatari ambao kinyume chake wanaweza kukabiliana na balaa kubwa hapo mbeleni na sishauri wala sitamani kuona wengine wakifanya usanii kupitia njia ya imani/dini.

Mkuu Ibra, kama nimekosea basi samahani mkuu wangu. Naomba kama topic inakugusa kwa namna moja ama nyingine au imekukera wafahamishe mods wafute kabisa. Nimeianzisha kwa wema kabisa mkuu wangu

dr. wewe umeokoka? kwa maelezo yako hapo juu ni kwamba nawe ulikuwemo kwenye kadamnasi hiyo. kama ni hivyo basi wape moyo wahusika utakuwa umefanya jambo la maana sana utashiriki katika kuwasaidia wahusika katika hilo.
 
Politicians like to manipulate the true sons of God! Just be aware! It could be the strategy to use that church as the platform to excel in their political agendas
 
Sasa hivi imekuwa ni kasumba kubwa ya watu kuweza kujipatia utajiri ama kuendesha maisha yao kwa nji za imani za kidini.

Kwa mfano, imekuwa ni kawaida kwa wahubiri wengi sasa hivi kutumia matatizo aliyo nayo mwanadamu kumvuta aende akajisalimishe mahali hapo na mataizo mengi ni yale ya kiuchumi. Matangazo yo husheheni mambo kama huna gari njoo Mikocheni B, unaishi kwenye nyumba ya kupanga njoo kwa Nguruo upate upako, una madeni sugu njoo kwa Mzee wa Upako n.k na wengine hujiita serikali za mbinguni. Ili uyapate haya yote ni lazima uingie mfukoni ndipo ubaikiwe na baraka wanazozitoa zinafuatana na kiwango cha pesa unachotoa. Kwa mwenye laki moja hawezi kupewa upako sawasawa na mwenye elfu kumi.

Kwa hiyo Sophia simba yamkini amefuta kupata upako na si kumuungamia BWANA awe mwokozi wa maisha yake.
 
hivi unawajua vizuri wanasiasa wewe? makamba hujawahi kumuona makanisani?

kwa taarifa yako, inawezekana hakuna aliyeokoka hapo, hata rwakatare mwenyewe. we subiri tu utaona
Hivi mnamkumbuka yule kijana aliyekamatwa na kichwa cha mtu pale Muhimbili?

Kabla ya hapo Rwakatare alikuwa amedai kuwa alimtungua akiwa anaruka kwa ungo na kumdondosha kwenye paa la kanisa lake. Sasa baada ya kumuombea na kumuokoa ilitokeaje mpaka akaenda kuua mtu? Au alifanya hivyo kwa msaada wa Rwakatare?

Hawa manabii, maaskofu wa kujisimika wenyewe, nk. ni watu hatari sana. Wote ni wafanyabiashara, hakuna dini wala imani. Wachunguze wote, Rwakatare, Kakobe, Mwingira,etc. They have one thing in common. UTAJIRI. At the expense of their poor congregations.
 
Wanasiasa ni viumbe wa ajabu sana, wanaweza kufanya vituko ilimradi vinawapatia kura!! Juzi juzi nimensikia Lyatonga Mrema akiwa anahojiwa pale TBC wakiwa na Lipumba ananukuu aya za Q'oran tukufu kwa kiarabu; Lipumba alishindwa kujizuia ikabidi acheke !!

Thi is the extent politicians can go in search of votes.

Kumbuka methali isemayo"UKITAKA CHA UVUNGUNI NI SHARTI UINAME"
 
huyu mama ananikera sana (mh ma' Dk Rwakatare aka mtumishi wa bwana) nilitegemea kuteuliwa kushika kiti cha ubunge kupitia viti maalumu angestaarabika ,kwa kuweka sound proof kwenye kanisa lake ilikuondoa kero ya kalele inayotoka kanisani kwake na kusababisha kero kwa majirani wanao mzunguka.

fikiria kuna watoto wadogo wa shule wanatoka mashuleni jioni wanaitaji mapumziko wanakutana na sebene zito toka kanisani humo, wanafanyeje home works zao na pia wanasomaje katika mazingira yenye kelele kama zile, ? na hua kuna mkesha kanisani hapo, ni balaaa....!!!!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom