mama Mungu na akunyime akili kama hii..............lol!

sasa Mtambuzi kama wewe umeletewa shauri hili ili uwashauri wewe ungemwambia huyo mama afanye nini na huyu baba je? ok najua mama na mtoto wamekosea lkn je baba kafanya sahihi kumlaani mwanae?
gfsonwin, umeniwahi ndio na-type ushauri wangu, bado sijamaliza nitaweka sasa hivi mtazamo wangu.............
Subiri bi dada............
 
Last edited by a moderator:
kufanikiwa kwa mwanaume mara nyingi huwa kuna efforts za mwanamke! na anguko lake pia ni huyo huyo MWANAMKE! pole kwa huyo baba! ila kweli ujinga unatofautiana viwango!
cacico wewe umesema kweli kabisa lkn sasa hivi huyu baba kamkomoa nani? siyo yy mweneywe kajikomoa?
 
Last edited by a moderator:
cacico wewe umesema kweli kabisa lkn sasa hivi huyu baba kamkomoa nani? siyo yy mweneywe kajikomoa?
gfsonwin hivi unajua wakati huo hata kama ungekuwa wewe, ungekasirika sana! tena ukute ungechukua maamuzi mabaya kuliko hayo! majuto yatakuja baadaye kwa huyo baba! ila sijui wamama wengine wakoje jamani?? lol!
 
Last edited by a moderator:
lakin sasa mkuu utafanyaje ili kuinusuru hii familia na laana?
nothing sadly! :( Broken trust from a wife and son is too much for us men. nasema hivi maana kuna watu wawili kwenye familia yangu hawaelewani kwa miaka 10+ sasa; licha ya juhudi za wasuluhishaji. solution ni kumuomba Mungu ampe moyo wa kusamehe lakini hii itachukua muda.
 
gfsonwin hivi unajua wakati huo hata kama ungekuwa wewe, ungekasirika sana! tena ukute ungechukua maamuzi mabaya kuliko hayo! majuto yatakuja baadaye kwa huyo baba! ila sijui wamama wengine wakoje jamani?? lol!
cacico ni kweli kabisa wakati wa hasira waweza fanya jambo baya sana, ila sasa je hili wewe ungeishauri nini hii familia? ukijua kuwa yule kijana ndo keshalaaaniwa na baba anahasira na mama anahofu ya alichokitenda?
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin naomba ujibu maswali ya fuatayo kwanza.....................

Baba mmoja mjeda ana ndoa yapata 25 yrs sasa, kwa bahati nzuri sana ana watoto wakubwa ambao ni college students. maisha ya familia za kijeda nafikir wengi tunayajua so huko sitaki kwenda ila haya ndiyo yalyotokea kwenye familia yake.

Je wana watoto wangapi na Je wote ni wa mama na baba mmoja, yaani hakuna wa nje ya ndoa?

Mkewe mjeda kwa siri kaamua kuuza mali za familia ambazo baba ndiye aliyezichuma kwasababu ya kuwa yeye ndio source of income nyumban na mama alikuwa ni goli kipa kitu. Mama huyu kauza nyumba maeneo fulan ambayo baba aliijenga ili atakapo staafu akapate mahalia pa kuish kuliko kubanana na watoto mjini, pia kauza kiwanja kingine kikubwa cha familia. Ha yote huyu mama anayafanya akishirikiana na watoto pasi kumwambia baba chochote. na pia aliuza wakati baba huyu alipopelekwa masomon na jeshi so akawa mbali na familia kwa wakati huo.
Je watoto wote wali-conspire kuuza mali za baba bila kumshirikisha ili mmoja wao akasome nje?
je baba alipokuwa masomoni alikaa kwa muda gani?
je ni kweli baba ni muasherati?
maana lazima tuangalie upande wa pili wa shilingi pia, isije ikawa baba alikuwa ameandikisha hiyo nyumba na kiwanja kwa jina la nyumba ndogo............

Kwanza nijibu hayo maswali ili nijue pa kuanzia.........​
 
Hiyo ni laana kubwa sana kwa huyo mtoto! Huwezi toa maneno ya kashfa kwa baba yako no matter what!! Huyo mtoto na mamake watabeba hizo laana, unless wamrudie huyo baba na kuomba masamaha wa kweli!
 
gfsonwin naomba ujibu maswali ya fuatayo kwanza.....................

Je wana watoto wangapi na Je wote ni wa mama na baba mmoja, yaani hakuna wa nje ya ndoa?

Je watoto wote wali-conspire kuuza mali za baba bila kumshirikisha ili mmoja wao akasome nje?
je baba alipokuwa masomoni alikaa kwa muda gani?
je ni kweli baba ni muasherati?
maana lazima tuangalie upande wa pili wa shilingi pia, isije ikawa baba alikuwa ameandikisha hiyo nyumba na kiwanja kwa jina la nyumba ndogo............

Kwanza nijibu hayo maswali ili nijue pa kuanzia.........​

huyu mjeda anawatoto 4 mkubwa ambaye ni binti yy anasoma hapa bongo kwenye vyuo vyetu vya kawaida.

siyo watoto wote wawili bali anayemtuhumu ni huyu wa kiume ambaye ndiye kaka mkubwa ingawa

alipokwenda kusoma alikaa miezi 6 short course za kijeda,

baba kwa maelezo ya familia ni kwamba kuna wakati aliwah kuwa na mahusiano ya nje ya ndoa na binti fulan na hii ilileta mtafaruku sana kwan mkewe na mwanae wa kiume walikwenda kumfanyia fujo huyu binti hadi watu kujeruhiwa.

ingekuwa huyu baba ameandika chochote kwa jina la nyumba ndogo definately huyu mama asingeweza kuuza manke kisingekuwa mali yake. hivi vyote vilikuwa vimesajiliwa kwa jina la baba mwenye familia. ni hayo tu kiongozi
 
Hiyo ni laana kubwa sana kwa huyo mtoto! Huwezi toa maneno ya kashfa kwa baba yako no matter what!! Huyo mtoto na mamake watabeba hizo laana, unless wamrudie huyo baba na kuomba masamaha wa kweli!

sasa kiongozi WALIMWEUSI, ukiwa wewe utashari nini hii familia? na utamconvice huyu baba hadi arudishe moyo wake nyuma? manake kumbuka mtoto wa kiume ndo keshaondoka na mzee haongei na mtu ndani kwake zaid ya watoto wake wawili wadogo. hali msosi hime zaid ya kuoga na kulala basi
 
Hizo huwa ni hasira tu, hata kama ungekuwa ni wewe. Cha muhimu ni huyo mama atambue kuwa amemkosea mumewe na ajshushe ajutie hilo kosa lake kwa Mungu wake na kwa mumewe. Ajaribu kumuomba msamaha mumewe na ikishindikana basi awafuate watu wazima wenye busara na hata watu wa dini (padri au shekhe), awaeleze ***** alioufanya then wao ndo wajaribu kuwasuluhisha. Ninaamini mzee atarudisha moyo nyuma na kumsamehe mwanae na mkewe pia ila HII KITU NI NGUMU KWA HALI YA KIBINAADAMU! Hapa MUNGU ashirikishwe sana otherwise laana itawatafuna!

Pia kwa upande mwingine wazazi wajitaidi kutokutoa maneno ya laana kwa watotot wao, sio vizuri kabisa! Ujue mzazi ni Mungu wa duniani so you need to love your children kama vile Mungu anavyotupenda. Ebu fikiria ni mara ngapi tunamkosea Mungu tena makosa makubwa zaidi ya hayo, lakini ANATUSAMEHE na bado anatupenda!! Naamini huyo baba akisamehe atapata thawabu kubwa kwa Mungu.
 
Huyo mama ni basua kichwa.kama alihitaji hela kwa lengo zuri tu la kumsomesha mwanae why asimshirikishe mzazi mwenzake? Sasa hapo kuna umuhim gani wa kuwa na baba(kichwa) cha familia?
 
Laaana imemfika kijana mdogo lazima hawe kizibo.

Mwanamke huyo kaibomoa familia yake kwa mikono yake mwenyewe
 
sion mahali ambapo wewe umeshirikishwa hili jambo na umeombwa kusaidia na hii familia mbali na kuelezwa na huyo binti wa kwenye hiyo nyumba....kingine baba amekataa mtu yeyote ampe ushauri na ndio maana ametumia neno ''padre''......endelea na kazi zako (mwagilia mboga mboga,lisha kuku au ng'ombe kama zipo la hazipo kaa ufume vitambaa vyako) hili halikuhusu..kwani huyo aliyekweleza amesema wameachana hao wanandoa? ....baba kamlaani kijana huku mama aliyeuza mali akiwa hajaambiwa lolote(kwa mujibu wa thread).....maneno aliyoyatoa mtoto kwa baba yake ni nauli (malezi) waliyokuwa wakimpa wazazi wake..na hayo ndio malipo...

halafu kingine...mama aliuza nyumba na kiwanja baba akiwa nje ya nchi masomoni na taarifa za kuwa nyumba imeuzwa alizipata wiki moja kabla ....umeendelea kusema pia kuwa baba alimlaani mtoto wake kwa kumuonyesha utupu wake!!! sasa hapa alikuwa kesharudi toka huko nje ya nch huyu baba ??!!...hii habari bado ina inaacha maswali mengi!! maana kuanzia heading yake haiko sawa..
 
Aisee wonders shall never end!
gfsonwin hii habari utaniambia vizuri personally baadaye...
 
Last edited by a moderator:
duh ama kweli mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba kwa mikono yake mwenyewe.......

Tatizo huyo mwanamke hajui uchungu wakutafuta, na kiukweli ni moja ya matatizo ya baadhi ya magolikipa, kulikuwa na umuhimu gani huyo mtoto akasome nje?

Huyo mwanamke anajua kesho na keshokutwa ikoje? Mume akirip anajua atatunzaje familia?

Kazi kweli kweli....
Mie nimekosa chakushauri kwa kweli....
 
sion mahali ambapo wewe umeshirikishwa hili jambo na umeombwa kusaidia na hii familia mbali na kuelezwa na huyo binti wa kwenye hiyo nyumba....kingine baba amekataa mtu yeyote ampe ushauri na ndio maana ametumia neno ''padre''......endelea na kazi zako (mwagilia mboga mboga,lisha kuku au ng'ombe kama zipo la hazipo kaa ufume vitambaa vyako) hili halikuhusu..kwani huyo aliyekweleza amesema wameachana hao wanandoa? ....baba kamlaani kijana huku mama aliyeuza mali akiwa hajaambiwa lolote(kwa mujibu wa thread).....maneno aliyoyatoa mtoto kwa baba yake ni nauli (malezi) waliyokuwa wakimpa wazazi wake..na hayo ndio malipo...

halafu kingine...mama aliuza nyumba na kiwanja baba akiwa nje ya nchi masomoni na taarifa za kuwa nyumba imeuzwa alizipata wiki moja kabla ....umeendelea kusema pia kuwa baba alimlaani mtoto wake kwa kumuonyesha utupu wake!!! sasa hapa alikuwa kesharudi toka huko nje ya nch huyu baba ??!!...hii habari bado ina inaacha maswali mengi!! maana kuanzia heading yake haiko sawa..
Edson nafikir hujanielewa na ni ngumu pia kuelewa nilichokimaanisha. so naona pia wewe huna msaada so sikuhitaji kwa wakati huu. mind your own business man
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom