Mama mkwe amegeuka kero kwenye ndoa yangu

hebu subiri, sina hakika kama nimeelewa viizuri. Yaani umuache mumeo mjini alafu wewe uende Machame? Hivi kumbe hizi mambo bado zipo uchagani? Huwa zinaboa ile mbaya.. yani unaolewa halafu unakaa na wakwe, mumeo atakuja desemba kwa desemba. Usikubali kuacha kazi, wala kwenda huko, tumia busara kutatua hili. Wewe uliliolewa ili uishi na mumeo na si ukaishi na wakwe...!

cha ajabu mama mkwe anaishi na mumewe ila anataka binti wa watu amuache mumewe akakae na wakwe. wanawake jamani mnapokua na wakwe zenu msiwafanyie hayo loh
 
cha ajabu mama mkwe anaishi na mumewe ila anataka binti wa watu amuache mumewe akakae na wakwe. wanawake jamani mnapokua na wakwe zenu msiwafanyie hayo loh

Hii tabia kwa wachaga ilikuwepo toka enzi, but nimeshangaa sana kumbe hadi leo hii inaendelea. You can imagine: yeye na uzee wake hataki kumwacha wa Ubavu wake, halafu anataka mwali wake (ndoa ndo kwanza imenoga) amwache mumewe, haiingii akilini kabisaaaa.
 
huyo mama mkwe muharibifu tu........
 
Huyo anataka akufanye ushitakiwe na dhamira na ujione mkosaji,mpuuze halafu jaribu kuongea na mwanae(mumeo)ili amkanye tabia yake hiyo!
 
Huyu mama ananifanyia visa vingi sana na kwakweli najiskia hasira sn na kisa cha kunifanyia yote hayo ni MIMI KUKATAA KUACHA KAZI NA KUMUACHA MUME WANGU MJINI KWENDA KUKAA NAYE KIJIJINI MACHAME KAMA ALIVYOKUA ANATAKA YEYE, kwakweli amekua mtu wa visa anafanya mambo kwa makusudi hlf anasema simpendi, mf: siku 1 aliniambia atakuja kwangu jumamosi hlf kwa makusudi akaja ijumaa bila kunijulisha na mimi nilikua kazini mschana kaenda kwao kuzika akakuta geti limefungwa badala anipigie simu akaanza kulia na kuwapigia wifi zangu kuwaambia kw nimemfungia yn sa 10 jioni ndo baba mkwe anapata taarifa toka kwa mabint zake na kunijulisha huku akisikitishwa na kitendo alichofanya mkewe. YN NI MENGI SN ANANIFANYIA MPAKA NAONA KERO SIJUI NIFANYAJE?? NIFANYAJE WAPENDWA??

Dawa kubwa ni kukaa KIMYA, usifungue mdomo wako hata siku moja, hao ni wengi sana ambao hawaheshimu ndoa za watoto wao shika kauli mbiu hii, ngoja niiandike kwa kizungu kupunguza ukali " The best answer for a foolish is silence"
 
Nakuhurumia sana mpendwa wangu, wakwe kama hao wananyima watu raha ya maisha. Kama ambavyo wengi wamekushauri nami pia nakusihi usikubali kuacha kazi yako ukakae Machame, because by the time she dies mumeo nae atakuwa ameshapata mke mwingine na hivyo kusambaratisha ndoa yenu. Mueleze mumeo msimamo wako. Uliolewa uishi nae na sio wakwe. Stick to your guns na usiogope kusemwa. Hata kama mumeo ni mzaliwa wa mwisho mila zingine zimepitwa na wakati. Muombe Mungu akupe ushujaa maana hajakuumba na roho ya woga.:hat:
 
Pole shosti, kumbuka kua mama mkwe ni sawa na mama yako jaribu kumpenda tafuta njia kama ulivyokua unajaribu ku win moyo wa mumeo na ukampata basi kwa mkwe pia utaweza, sisemi kua ni rahisi lakini hata mumeo na wifi zako wakiona unavyojitahidi kumpenda mkweo watamsema mzazi wao na yeye akiwa kama mkwe ajarudi. jukaze kike dada umependa boga upende na ua lake....
 
ASANTE KWA USHAURI kweli nilishakaa na mama nikamweleza kuwa sitaweza kuacha kazi nikakaenaye kijiji si tuu kutokana na ugumu wa maisha bali pia kuishi mbali na mume kutachangia uwezekano wa kuleteana ukimwi, mama hanielewi ndo kwanza kila siku akaanza kulalamika anaumwa leo kichwa,kesho tumbo, keshokutwa maskio analalamika hana mtu wa kumwangalia basi nikamwambia aje mjini tukae naye ili tumpeleke na hosp. Kubwa AKAKATAA AKASEMA HAWEZI KUMUACHA MUMEWAKE PEKE YAKE, analalamika kila kukicha yn!
Kama yeye awezi kumuacha mume wake ambaye ameshakula chumvi nyingi,vipi wewe ambaye bado wote damu zenu zinachemka? Mpotezee huyo mama hana nia nzuri na ndoa yako,anataka kukualibia kwa Mr wako ili akuache,kwani utakapo enda kukaa naye kule kijijini,atafikisha ripoti mbovu kwa mumeo,kama uhamini wewe subutu kwenda naye huko kijijini,yatakayo kukuta utanitafuta. Chakufanya we shika 50 zako ila usimzalau wala kumtusi,kwa lolote atakalokufanyia we mpotezee tu na unatakiwa uonyeshe msimamo wako na huo msimamo mumeo aujue.
 
Hapo mwenye kuokoa hilo jahazi ni mume wako, kwa nini anakosa msimamo??

Mumeo ana msimamo gani kwenye hilo? yeye ndiye mtatuzi. akisema mke wangu haendi kijijini hiyo ni FULL STOP. Huko kijijini utakwenda kulala na baba mkwe, ukimkatalia, atakuzushia makubwa sana kwa mume wako, kwamba unatembea na wanaume wengine.

Ukiondoka mjini nako unawaachia machangu wamchukue mume wako.

Baki na mume wako mjini, FULL STOP!
 
Huyo anataka akufanye ushitakiwe na dhamira na ujione mkosaji,mpuuze halafu jaribu kuongea na mwanae(mumeo)ili amkanye tabia yake hiyo!
mwanzo mume wangu alikua na msimama lkn mama yake akaanza kumlalamikia kuwa alimzaa na kumlea kwa shida sana na baba yake alimtelekeza akahangaika kumlea mwenyewe na anamtoto wakiume 1 tu (mumewangu)alitegemea akioa mkwewe(mimi) nitaenda kukaa naye, mwanae akaanza kubadilika na kuanza kunishawishi nihamie kijiji nikamwambia twendewote akasema hatoenda niende mimi nami kwa ustaarabu nikamwambia sitoenda basi mara kwa mara anakua na maneno ya kunilaumu tu mpaka naona ndoa chungu
 
na ushikilie msimo wako.

Kwa maelezo uliyotoa sasa hapo chini tatizo wala si mama mkwe; Ni mumeo.

Mimi angekuwa mume wangu ningemwambia forget, kuniambia niende kwa mama yako ni sawa na kunambia nirudi kwetu;

Dada usikubali hata kwa fimbo kwenda huko kijijini utajuta na utaja kufa kwa maradhi (sorry to say)

Tulikuwa na jirani yetu nikiwa primary, alikuwa anaishi na wife wake vizuri tu tena ni baba mzee wa kanisa.

Ghafla nikasikia ooh mke wangu anaenda kijijini, mimi mtoto wa mwisho na kaka yangu alijenga ghorofa (kaka padri) hivyo wife anaenda kumlea mama. Hiyo familia ilikuwa inaishi next to us na tulikuwa marafiki sana kuanzia watoto mpaka wazazi.

Kibaya zaidi mke wa jamaa aliondoka na watoto; kwao kibosho.

Ndani ya kama miezi sita yule baba akawa anatembea na muuza maandazi tena mchafuuu. Nilikuwa darasa la tano kama sikosei lakini imagine nilikuwa najua uhusiano wa huyo mzee na mama muuza maandazi; maana kila mtu alikuwa anajua. Maana huyo mama alikwa kama ameamia fulani, anapika na kupakua.

Kama ni kumlea mama si waweke housegirl au basi mara elfi aje Dar mumlee vizuri (japo nayo ni shida but much better)

Hivi kweli mwanaume rijali aoe afu aishi maisha ya ki bachelor??? Haingii akilini, mi ngemwambia ukiona natoa mguu humu ndani jua our marrigae is over! full stop! Hiyo mila ni potofu kuliko ukeketwaji.
mwanzo mume wangu alikua na msimama lkn mama yake akaanza kumlalamikia kuwa alimzaa na kumlea kwa shida sana na baba yake alimtelekeza akahangaika kumlea mwenyewe na anamtoto wakiume 1 tu (mumewangu)alitegemea akioa mkwewe(mimi) nitaenda kukaa naye, mwanae akaanza kubadilika na kuanza kunishawishi nihamie kijiji nikamwambia twendewote akasema hatoenda niende mimi nami kwa ustaarabu nikamwambia sitoenda basi mara kwa mara anakua na maneno ya kunilaumu tu mpaka naona ndoa chungu
 
Naona watu mmelipa uzito swala la kuacha kazi; mi nimelipa uzito swala la kuacha mume. Hata kama ungekuwa house wife hukuolewa kuwa mlezi wa mama yao.
 
Huyo mama mkwe anataka kukuletea balaa dada yangu. Kama ni mimi siongei mara mbili hili suala. Ni kutafuta sumu ya panya tu na kumwekea kwenye kinywaji huyo mama mkwe mpuuzi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom