Mama mjamzito ajifungua mayai 2 Tabora

Grader

JF-Expert Member
Feb 23, 2009
445
64
Mama mjamzito ajifungua mayai mawili badala ya mtoto katika hospitali ya misheni ya Ndala- Nzega, Tabora. Habari zinasema ya kuwa mama huyo alikuwa anahudhuria kriniki kama kawaida na siku zilipofikia za kuzaa alipelekwa hapo na kulazwa ili kusubiri kuzaa. Cha ajabu alipopelekwa labour alijifungua mayai mawili badala ya mtoto/watoto.
 
Naomba uweke picha husika ya hilo tukio, then story yenyewe !!!! la sivyo hamisha hii topic kwenda Habari mchanganyiko au JF Doctor plzzz.
 
Duh yaani Tz tunatia aibu ni mambo ya ushirikina tu usiokua na tija, sasa si bora angetagishwa yai la dhahabu kama story ya The Goose who lay golden egg :pray: Mungu atusamehe sijui ni lini tutaamka toka usingizini.
 
Hii ni evolution jamani, muda si mrefu wake zetu watakuwa wanataga mayai na kuendelea kuchapa kazi (50/50) kisha mayai kuanguliwa na mashine! Hii itakuwa nzuri sana na itapunguza mateso kwa mwanamke na kuongeza muda wa kufanya kazi.
 
you can say that again?!!
 
Pole sana kwa huyo Mama, haya ni maajabu kweli! Sijui mayai hayo ni size gani? Na hayo mayai yamehifadhiwa wapi???
 
.........Hapa sasa ndio mtu utaona umuhimu wa kupata huduma ya ultrasound kipindi cha ujauzito ili ujue umebeba nini, lakini kibongo bongo huduma hii ipo kwa wachache wenye pesa. Maskini mama wa watu kateseka miezi 9 kumbe kabeba mayai.......Ehhhhhhhh!!
 
Ultra Sound Itaweza kung'amua Mambo ya Giza kweli
 
Hii habari iko kwenye gazeti la mwananchi. Lakini ukiisoma kwa makini na kujaribu kutumia 'ubongo' wako utaona kuna kitu kama utapeli hivi kutoka kwa huyu mama... Mimi nitakuwa mtu wa mwisho kuamini vitu vya kipuuzi kama hivi
KATIKA hali isiiyokuwa ya kawaida, Mkazi wa kijiji cha Mwisole wilayani Uyui Mkoa wa Tabora, Kabula Kayungilo (20) amejifungua mayai mawili kama kuku badala ya mtoto.

Tukio hilo ambalo liliwaduwaza wakazi wengi wa Mji wa Tabora huku wengine wakitaka mayai hayo yafanyiwe uchunguzi wa kitalaamu ili kubaini kulikoni, lilitokea jana katika Hospitali ya Misheni ya Ndalla wilayani Nzega.

Mganga mkuu wa hospitali hiyo inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Dk Reuben Nyaruga, alisema tukio hilo lilitokea jana asubuhi wakati mama huyo alipofika kwa ajili ya huduma ya kujifungua mtoto.

Dk Nyaruga alimtaja mkazi huyo kuwa ni Kabula kayungilo (20) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mwisole wilayani Uyui.

Alieleza kuwa msichana huyo alipokewa hospitalini hapo jana asubuhi akidai ni mjamzito anayejisikia uchungu wa kujifungua.

"Lakini uchunguzi wa awali uliofanywa na madaktari ulionyesha kuwa msichana huyo hakuwa na mimba ingawa alionekana kuwa na tumbo kubwa kiasi," alisema Dk Kayuga na kuongeza:

"Wakati muuguzi akiendelea kumpima ghafla msichana huyo aligumia maumivu ya kujifungua na kumfanya muuguzi amuandae kwa ajili ya kujifungua."

Alisema baada ya kuandaliwa mahala pa kujifungua, msichana huyo alijifungua mayai mawili yanayofanana na mayai ya kuku jambo ambalo lilimshangaza mwenyewe na muuguzi.

"Waliamua kuvunja yai moja ili kuona kilichokuwa ndani. Wakakuta kiini cha yai linalofanana kabisa na yai la kuku," alisema na kueleza kuwa yai lingine walimpa ndugu wa mume wa mwanamke huyo.

Kwa mujibu wa Dk Kayuga hii ni mara ya pili kwa msichana huyo kuhisi kuwa na mimba. "Mara ya kwanza mimba yake ilitoka ikiwa na miezi mitatu." alisema.

Akieleza historia ya mgonjwa huyo, Dk Nyaruga alisema katika zahanati ya kituo cha Mwisole alipokuwa akihudhuria kliniki, cheti chake kinaonyesha alihudhuria mara mbili.

"Mara ya kwanza aliwekewa alama ya mkato na mara ya pili alionekana ana mimba ya wiki kumi na sita," alisema.

Mume wa msichana huyo Bugalama Mahona alieleza kuwa mkewe huyo alianza kuhudhuria kliniki baada ya kuamini kuwa ana mimba.

"Sasa tulikubaliana kwamba aje katika hospitali hiyo kubwa ili ajifungue kwa usalama zaidi," alisema Mahona.

Akizungumzia tukio hilo msichana huyo alisema kabla ya kutaga mayai hayo alijisikia uchungu wa kujifungua.

"Nilikuwa nikitarajia kumpata mtoto wa kwanza baada ya mimba ya kwanza kutoka," alisema.
 
Mama mjamzito ajifungua mayai mawili badala ya mtoto katika hospitali ya misheni ya Ndala- Nzega, Tabora. Habari zinasema ya kuwa mama huyo alikuwa anahudhuria kriniki kama kawaida na siku zilipofikia za kuzaa alipelekwa hapo na kulazwa ili kusubiri kuzaa. Cha ajabu alipopelekwa labour alijifungua mayai mawili badala ya mtoto/watoto.

this....
 
Pole sana kwa huyo Mama, haya ni maajabu kweli! Sijui mayai hayo ni size gani? Na hayo mayai yamehifadhiwa wapi???

watakuwa wameshagongea chipsi...bila shaka ni ya size ya kuku...chipsi mayai safiiiii....anashushia na mountain dew maisha yanaendelea
 
Back
Top Bottom