Mama mdogo aina hii afanyweje?

Enny

JF-Expert Member
May 26, 2009
962
130
Kuna rafiki yangu kaja jana kunilalamika kuhusu mama yake mdogo kuwa ana roho mbaya sana hataki watoto wa dada yake wapate bali watoto wake tu. Jamaa kaniambia alikuwa anafanya kazi kongo kwenye kampuni moja ya madini kama expat sasa waliingiliwa na majambazi mara mbili kwa kipindi cha interval ya miezi mitatu. Sasa jamaa akaamua kutafuta kazi tz na akapata, hivyo akaamua kuacha kule na kurudi tz. Basi aliporudi akafunga safari kwenda mkoani alipo mama mdogo wake kuwasalimia, na katika story za maisha akawasimulia jinsi walivyopona kuumizwa na majambazi, alipewa pole sana kwa yaliyowakuta huko. Lakini baada mwaka mmoja akaja kusikia kuwa mama yake mdogo huyo anatangaza kuwa huyo jamaa alipanga na majambazi waje waibe pale kazini kwao na wakagawana hela ndio maana amefanya mambo mengi ya maendeleo. Wakati jamaa alikuwa analipwa vizuri kule kwa kipindi cha miaka miwili yote aliyokaa huko ameweza kufanya mambo mengi nyumbani. Sasa alitaka ampigie simu huyo mama ili kumtukana. Mimi nikamshauri asifanye hivyo aachane nae. Akaniambia mara nyingi amekuwa akiongea negative kuhusu yeye na wadogo zake. Je ni ushauri gani una mfaa huyu rafiki yangu maana naona amechukia sana.
 
Mnh, haya maisha jamani! Anyway, mshauri jamaa aepukane na huyo mama yake mdogo. Kuna uwezekano kuwa huyo mama ana katabia ka kipuuzi ambacho amezaliwa nacho hivyo hawezi kukaacha. Vinginevyo ampige mkwara mzito ikiwezekana hata kumuweka kitimoto na ndugu wachache.
 
hivi mama mdogo naye anakusumbua?
Kawa mama mzazi au baba mzazi au mke?

Anaendekeza tu, na wala sioni kama ana tatizo lolote.
 
Kama anaweza anyamaze kimya na kuacha kwenda kwa hyo mama mdogo unless kuna kitu anapata faida nacho maishani.

ila inaonekana hawapendi wanedelee kama alivyosema kwa hiyo akae na kuwahudumia wadogo zake mwenyewe bila hivyo atawaumiza kimaisha zaidi.

akiona hawamtafuti basi ataweza kunyamaza na pia wasimsumulie maendeleo yao akae akidhani hawana mbele tena.

haya yanaletaga matatizo na atajuta,

mwambie akae kimya kabisa hata kama huyu mama kasaidia kuwalewa.

Pia kumtukana ni kujitakia balaa eti ampigie live no action zake zitalipa yote.
 
hivi visa vingine tunavitafuta wenyewe,kwenda kumueleza mambo yote hayo wakat unajua yuko negative naww pamoja na ndugu zako inamaanisha nn.aachana na hiyo mambo,jaribu kuweka distance nao kabisa mwishowe atamuita huyo kaka jambazi
 
huyo mama mdogo wako anaweza kuwa pacha wa mama mdogo wangu...

Ila mama mdogo atakuumizaje kichwa?
Umuone usimuone hapunguzi wala kuongeza chochote...
Mpotezee.......
 
..................maneno matupu hayavunji mfupa......................kwa hiyo akae naye mbali...........keep his distance from gossipers.........................they are no good at all.................they are dream killers..........
 
Very simple mbona ni kiasi cha kum delete tu,kila mtu aendelee na maisha yake.....hakuna kumpigia cm wala kupotea njia!
 
Kuna rafiki yangu kaja jana kunilalamika kuhusu mama yake mdogo kuwa ana roho mbaya sana hataki watoto wa dada yake wapate bali watoto wake tu. Jamaa kaniambia alikuwa anafanya kazi kongo kwenye kampuni moja ya madini kama expat sasa waliingiliwa na majambazi mara mbili kwa kipindi cha interval ya miezi mitatu. Sasa jamaa akaamua kutafuta kazi tz na akapata, hivyo akaamua kuacha kule na kurudi tz. Basi aliporudi akafunga safari kwenda mkoani alipo mama mdogo wake kuwasalimia, na katika story za maisha akawasimulia jinsi walivyopona kuumizwa na majambazi, alipewa pole sana kwa yaliyowakuta huko. Lakini baada mwaka mmoja akaja kusikia kuwa mama yake mdogo huyo anatangaza kuwa huyo jamaa alipanga na majambazi waje waibe pale kazini kwao na wakagawana hela ndio maana amefanya mambo mengi ya maendeleo. Wakati jamaa alikuwa analipwa vizuri kule kwa kipindi cha miaka miwili yote aliyokaa huko ameweza kufanya mambo mengi nyumbani. Sasa alitaka ampigie simu huyo mama ili kumtukana. Mimi nikamshauri asifanye hivyo aachane nae. Akaniambia mara nyingi amekuwa akiongea negative kuhusu yeye na wadogo zake. Je ni ushauri gani una mfaa huyu rafiki yangu maana naona amechukia sana.

Maadam anajiumiza kwa roho yake mbaya,rafiki yako azidishe maendeleo ili mama azidiwe na maradhi yake afilie mbali. Ya nini kupoteza muda badala ya kupiga ndege wawili kwa jiwe moja! Akaze maendeleo yake na kila akiendelea ndio maradhi ya mama mdogo yanavyozidi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom