Jomse
JF-Expert Member
- Jan 19, 2011
- 275
- 92
Haya mambo yapo sana hasa kwa mama na mtoto wa kiume .Kwenye familia yetu yametokea mimi nina kaka watatu;mama yangu anampenda na kumjali sana huyo wa katikati,hakuna baya analolifanya.Wale wakaka wengine wamelalamika sana huo upendeleo alionao mama kwa mwenzao.Hilo la kufuliwa nalo lipo lakini si zile nguo za ndani.Mfano kwa sasa kijana ana miaka 29 na ameajiriwa lakini ikifika tarehe 20 huwa ana tabia ya kulia ukata wa pesa kiasi kwamba mama huangaika mpaka amtumie fedha Tumeshakaa chini na kumtaadharisha madhara ya kumdekeza kupita maelezo. mama hataki huyu kijana akue na aweze kujitegea.Kwanza kwa sasa yeye anapaswa kutumiwa fedha.