Mama kupiga dabali ruksa?

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,949
4,444
attachment


Jamani hapa tunaongea kama wazazi
Je ni halali mama kupiga dabali watoto mgongoni?
Akipiga hivi dabali haiathiri malezi na makuzi ya watoto?
Yaani hapa nazungumzia umemwacha mkeo nyumbani akaja jirani akaomba amwangalizie mtoto sasa anapata mishemishe yakwenda dukani kununua mafuta kwenye kibapa je ruksa kuwapiga watoto dabali mgongoni kama hivi kwenye picha? Ukiwa kama baba ndo umeona mkeo kawapiga dabali watoto mgongoni utachukua hatua gani kuona mbegu zako ulizo panda na zikamea vizuri zinapigwa dabali mgongoni?
Karibuni wazazi.
Ni mimi baba Happy mwenye hasira kali.
 
dah lugha inakua mkuu
kubeba watoto wawili mgongoni
Hatari zinaweza kuwepo pande zote mbili:
1- Kwa mama, anaweza kuathirika mgongo baada ya kipindi fulani. Mgongo ni sehemu "sensitive" sana, ukikosea kidogo kubeba kitu kizito unaweza kupata madhara makubwa.
2- Kwa watoto kama ikijatokezea mbeleko kufunguka na watoto kuanguka. Sioni athari nyengine kwa watoto zaidi ya hii "physical" kama ikitokea.
 
Sijaona picha, ila kama kapiga dabali watoto wake wawili sawa, ila kama kachanganya na wa jirani si sawa.
 
picha yako haifunguki.

Ila ukiona mkeo kabeba watoto namna hiyo ndo ujue kumsaidia ulezi, sio alee wanao na wewe pia akulee mwisho wote mtapigwa 'dabali'
 
mi mmama,ngoja kina baba wenye hacra kali kama zako waje wakujibu.hebu image kama hao watoto i mapacha na bado hawajafikia umri wa kutembea na mama analazimika kwenda sokon na hana msaidizi wala jarani wa kumwachia je akipiga hiyo dabali utamind?
 
Tena amsaidie kabisa kutengeneza ulezi wa uji wa watoto.

Akina baba wanasahau sana ulezi wanawaachia akina mama peke yao, tena wa tarime mtamuuu.

picha yako haifunguki.

Ila ukiona mkeo kabeba watoto namna hiyo ndo ujue kumsaidia ulezi, sio alee wanao na wewe pia akulee mwisho wote mtapigwa 'dabali'
 
Tena amsaidie kabisa kutengeneza ulezi wa uji wa watoto.

Akina baba wanasahau sana ulezi wanawaachia akina mama peke yao, tena wa tarime mtamuuu.

kabisaaaaaa la sivyo mkewe akiwabeba watoto tripo tripo asilalamike.
Maana dabali tu katoa macho.....
Tripo si atazimia....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom