Mama Kilango v/s Sophia Simba ndani ya uchaguzi wa UWT...

Mimi siamini sana katika factor ya umri (mkubwa ama mdogo) kwenye uongozi. Mimi naamini zaidi kwenye uwezo wa kiuongozi. Tunategemea viongozi wenye umri mdogo wawe wabunifu sana kuliko wale wazee, lakini mara nyingi tumeona matokeo kinyume na matarajio haya. Tumeona pia mafanikio makubwa yakiletwa na viongozi vijana sehemu mbalimbali, ambako viongozi wazee wameshindwa. Mfano wa Joseph Kabila Kabange anavyoimarisha demokrasia kule DRC na pia anavyojenga mabarabara na viwanja vya ndege sasa hivi kule nchini kwake, anavyojenga mahospitali na anavyotetea nchi yake kufaidika na madini na rasmlimali - haya yaliwashinda baba zake akina Kabila Sr na Mobutu Sseseseko Kukungwendu wa Zabanga (aliyekuja kufa kidhalili kabisa), tunaona mambo makubwa aliyoyafanya Paul Kagame wa Rwanda. Tunaona mafanikio makubwa ya kuleta mabadiliko ya mahusiano kati ya watu weusi na weupe kule Marekani thru non-violence movements ya kijana Dr. Martin Luther King Jr, tunaweza pia kujifunza kutoka kwa akina Mwl. Nyerere na wenzake na makubwa waliyoyafanya kwa nchi yetu na Dunia kwa ujumla...and the list goes on! Tujiulize hawa wote walikuwa wazee?

Ukiwa muumini wa mabadiliko ya ukweli basi kwa vyovyote vile utatakiwa kuniunga mkono mimi na wanamapinduzi wengine wanaojitokeza kuomba nafasi za uongozi wa chama chetu, na kisha utanipa mawazo yako bila kujali ni kijana ama ni mzee kiasi gani. Sina nia nyingine yoyote ile zaidi ya kutaka kuingia kwenye vikao vya juu vya maamuzi ya chama changu ili kushawishi mabadiliko kutokea. Chama Cha Mapinduzi kinahitaji wanamapinduzi kama mimi kwa sasa, kwanza kwa ajili ya succession planning na pili kwa ajili ya nguvu mpya ya mabadiliko wanayoyahitaji waTanzania wa sasa. Kisipoamka na kuchukua nguvu mpya on board, kitayumba na hii itapelekea Taifa pia kuyumba. Tulio na nia nzuri na nchi yetu, na chama chetu tunachukua hatua kwa kuingia ndani na kushawishi mabadiliko! Wenzetu mjue kuwa tunachukua risk kubwa sana na mnachoweza kufanya si kingine tu bali kutuunga mkono na zaidi kututia moyo.

Najipanga kuomba kibali cha kugombea na nina imani kabisa chama changu kitanipa fursa hiyo ili nifike mbele ya wanachama wenzangu wa jumuiya hiyo kutafuta ushindi na ninaamini wapiga kura watanielewa na kunipa kura za ushindi ili tufanye kazi pamoja.
Mimi nilikuwa najua Chama kinapokuwa na Jumuia zake kama ilivyo kwa utamaduni na muundo wa CCM ni kwamba unaposema Jumuia ya Wanawake basi, tunategemea kiongozi wa Jumuia hiyo atakuwa mwanamke, na vilevile kwa jumuia ya vijana basi kiongozi wake anakuwa ni kijana, vilevile kwa wazazi, nilijua atakuwa mtu mfulani mwenye umri wa makamo au mzee ndio atakuwa kiongozi wa jumuia. Anyway mimi si mwanachama wa CCM nitakuwa naelewa vibaya. Nikutakie mafanikio kanisa katika harakati zako Mh Kigwangala
 
[h=2][/h]JUMAMOSI, AGOSTI 04, 2012 05:33 NA MWANDISHI WETU, DODOMA

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), Sofia Simba, amesema jumuiya hiyo haihitaji vurugu na mabadiliko zaidi, kwa kuwa iko imara kutokana na uongozi wake.

Alisema kama kuna mgombea wa nafasi ya mwenyekiti anayetaka kuleta mabadiliko, huyo anataka kuleta vurugu, kwa kuwa jumuiya iko imara kutokana na misingi imara aliyoiweka.

Sofia aliyasema hayo jana makao makuu ya CCM mjini hapa, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kurudisha fomu ya kutetea nafasi yake wakati wa uchaguzi wa jumuiya hiyo, utakaofanyika baadaye mwaka huu.

Pamoja na mambo mengine, Sofia alikuwa akimjibu mgombea mwenzake, Anne Kilango, ambaye juzi alichukua fomu na kusema ameamua kugombea nafasi hiyo kwa kuwa anataka kuleta mabadiliko ndani ya UWT.

“Kuna mwenzangu mmoja amechukua fomu hapa jana (juzi) na kujigamba kuwa anataka kuleta mabadiliko eti kwa sababu ana uwezo wa kufanya hivyo.

“Pia mtu huyo alisema yeye ndiye anayefaa kwa sababu aliingia UWT akitokea ngazi ya wilaya na kwamba mimi niliingia UWT nikitokea ngazi ya kata.

“Sasa ngoja niwaambie, mimi ndiye ninayeijua UWT kwa sababu nimeanzia chini hadi kufika hapa nilipo, kwani niliwahi kuwa Katibu wa UWT katika Tawi la NDC, kisha nikawa Mwenyekiti wa UWT Kata ya Upanga Magharibi pale Dar es Salaam mwaka 1993.

“Pia niliwahi kuwa Diwani wa Kata ya Upanga Magharibi mwaka 2000 na nikawa Mbunge mwaka 1995, na kikubwa zaidi kinachonifanya nitofautiane na huyo mtu ni kwamba, tangu mwaka 1998 nimekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la UWT.

“Sasa angalieni wenyewe mimi na yeye ni nani anayeijua jumuiya, ni yeye aliyeingia akitokea wilayani au mimi niliyeingia nikitokea chini kabisa kwa wanajumuiya?

“Pamoja na hayo, nawaambia UWT iko imara, haihitaji mabadiliko makubwa kama anavyosema, kama anataka kuleta mabadiliko basi anataka kutuletea ugomvi ambao siyo sera yetu.

Kwa mujibu wa Sofia, wakati yeye akishika nafasi hizo, Anne Kilango alikuwa hajaingia katika siasa na kwamba wanachama wa UWT wanatakiwa kuwachagua viongozi wanaoifahamu vizuri jumuiya kuliko wasiofahamu.

 
Ina Maana Anna Kilango UBUNGE wa WILAYA sasa basi? CHADEMA wanachukua?
 
Kilango hafai ana tamaa sana...kwanza hajui uongozi..angoje 2015 awe first lady..
 
Hawa inabidi tuwapangie siku wakutane pale Travertine hotel ili wapashane mbele ya mashabiki wao.
 
Tatizo Kilango msimamo wake unayumba siku hizi!Ameanza kukaa kichama zaidi kuliko kizalendo!Simba kwakweli hizi nafasi wanazompa zinamzidi uwezo labda wampe timu inayojiweza chini yake!!Kiuwezo Kilango akiamua anaweza zaidi Ya Simba,ila siku hizi haeleweki!
 
Hii ni jumuiya ya CCM lakini inaitwa UWT!Kwa nini isiitwe jumuiya ya wanawake wa CCM?Hili jina lao la sasa limekaa kiwiziwizi sana kuwahadaa wanawake wengi nchini
 
Hii ni jumuiya ya CCM lakini inaitwa UWT!Kwa nini isiitwe jumuiya ya wanawake wa CCM?Hili jina lao la sasa limekaa kiwiziwizi sana kuwahadaa wanawake wengi nchini

Ilikuwa ni Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania hapo awali ambayo ilihusisha wanawake wote, lakini baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, CCM kama kawaida yake ikapora jumuia zote ikiwepo ya umoja wa vijana Tanzania na jengo lake pale karibu na Fire. Ngoja tuchukue dola watakoma ubishi mara moja.
 
Hawa si walishutumianaga kwamba Sophia alitaka kumchukulia Anne mume wake, WOTE HAWAFAI TOO VOCAL, wambea, vihiyo, Anne kanunua degree OUT kwani mumewe ndio Mkuu wa OUT, both are watu wa mipasho tu nothing new....
 
Hawa wote ni vipepe tu,
kumbe siasa za kike zinahusisha mipasho.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kilango kapima upepo na kuona 2015 hana jimbo sasa anataka uenyekiti ili arudi bungeni viti maalum.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom