Mama Kilango v/s Sophia Simba ndani ya uchaguzi wa UWT...

twu fin.JPG


a. Hata kama hatuipendi, siasa inatuhusu sana maana wanasiasa wakisha chaguliwa hukutana katika vikao vyao na kupitisha au kusimamia utekelezaji wa sera zinazoathiri maisha ya raia wote bila kujali ni wa chama gani. Aidha wanasiasa pia huchaguza viongozi ambao wakati mwingine husimama kwa niaba ya vyama vyao hadi kuwapata viongozi wetu ambao ni Madiwani, Wabunge na hadi Rais na Makamu wa Rais.

b. Hata kama hatukipendi au kukiunga mkono CCM, hiki ndicho sasa chama tawala na hata uchaguzi wa 2015 kutakuwa na mnyukano mkubwa kati ya CCM na CHADEMA au vyama vingine vyovyote vitakavyokuwa na nguvu za upinzani wakati huo. Hivyo Viongozi wowote wanaochaguliwa sasa katika ngazi ya chama kitaifa hata katika jumuiya za vyama vya siasa iwe CCM, CHADEMA CUF n.k si wa kuwapuuza maana huingia katika vikao vyao na ku-shape maisha ya Watanzania wengine wote kupitia sera wanazozieleza na kuzitekeleza na zaidi ya yote kusimamisha wagombea wao (madiwani, wabunge, Rais na Mwenza wake) ambao baadaye hushiriki kama kutunga sheria ndogo-ndogo ktk Halmashauri na Sheria za nchi Bungeni.

Hawa wanasiasa pia wana ‘rungu’ walitumialo kuwaogopesha viongozi wanaotoka katika vyama vyao kufuata matakwa au misimamo yao, mfano ni vigumu sana Waziri yeyote hata Waziri Mkuu kwenda kinyume na Katibu Mkuu wa chama chake tawala na Wajumbe wake wa Kamati kuu au Halmashauri ya chama chake, mwanasiasa mbadhilifu atatumia tungu la kibadhilifu na mwanasiasa mwadilifu atatumia rungu la uadilifu!


Tukiyatambua hayo; siku chache zijazo kutakuwa na uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT- CCM (T); hata kama wewe si mwana CCM, unayo sauti kupitia mitandao kama hii kukataa na kutoa maoni yako ikiwa ni sehemu ya kuwambia wapiga kura wa mkutano mkuu wa UWT- CCM (T) kuwazika WANASIASA WANAOTAKA KUENDELEA KUWA MADARAKANI WAKATI HAWANA SIFA NA WAMESHIRIKI KULIFIKISHA TAIFA HILI TULIPO SASA.
Kama hujali, mimi najali kwamba vyama vyote vya siasa vipate viongozi wake walio na uadilifu na wenye sifa za kuongoza.

Chombo cha habari kimeturahisishia kazi kwa kutoa picha zinayowaelezea wagombea watatu wa UWT- CCM (T).
Na kwa kweli mimi nita- ‘mind’sana endapo tutaendelea kuwa na mtu wa mipasho au kumbeba anayekurupuka na kelele tukamwacha mtu anayejali maendeleo toka chini (grassroots) na ambaye harudi nyuma kuhamasisha wanawake na vijana wengine juu ya harakati za maendeleo hadi kitakapoeleweka!

Hawa wote watatu wanaishi Tanzania na tumewafahamu kwa kujua aina ya maisha yao na wanachosimamia:spy:; funguka na sauti yako itamfikia mjumbe-mpiga kura!
 
Mie sioni nafuu hapa. Wote ni mafisadi wa kawaida. Sijui kwenye mechi ya uchafu kama kunaweza kuonekana usafi.
 
Back
Top Bottom