Mama Kilango jiandae mwisho wako ni 2015

John W. Mlacha

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
3,504
1,341
Mimi ni mwanamapinduzi na mwanaharakati ...huyu mama kaja katuharibia jimbo letu anaongea sana na hakuna anachofanya zaidi ya kuwahadaa wananchi wa same.. sasa mama nakuambia kuwa mwisho wako unakaribia..

jimbo zuri lakini wananchi wake wanaishi gizani ..kuanzia afya ,elimu na barabara ...jimbo lote hakuna barabara ya lami hata moja ...wananchi waliahidiwa barabara ya lami toka mkomazi hadi same lakini hadi leo hakuna hata dalili na ni ndoto na nina uhakika wewe mama huwezi kuileta ..sasa jua kabisa kuwa mwisho wako ni 2015...nitapita nyumba kwa nyumba na kuwaelewesha wananchi kuwa nchi yao inaliwa na wajanja na wewe ukiwa mmoja wao...

pokea kwanza hii alert ....
 
Acheni majungu hata sisi tusiokuwa wa jimbo lake tunajua anachokifanya.......Barabara za Same Mashariki zinapitika mwaka mzima tangu mama huyu amekuwa Mbunge. Vipi barabara za kwenda milimani kama Ndungu-Lugulu uliitengeneza wewe?? Kiwanda cha Tangawizi ulihusika?? Mafisadi Bungeni ulishawahi kuwanyoshea hata kidole?? ........ Hao waliokutuma ulete upupu wako hapa waambie watafute njia nyingine.
 
huyu mama kigeu geu sana niliona alivyo mtetea ngereja baada ya kamati teule ya bunge ya juzi ndo nikajua ni mtu wa ovyo
 
Ni ushamba kumlaumu mtu kama huyu...mpiganaji pekee ninae mkubali..kuumbua mafisadi si kazi ndogo
 
Acha uongo hakuna walichofanya wakati kuna mpango jimbo la mamam huyu kusaidiwa na IRAN wachimbe mafuta au hufahamu mahusiano mazuri ya familia ya mama huyu na IRAN?
 
Huyu mama akiondolewa, sio kwa sababu hajawatendea mema watu wa jimbo lake, bali ni kwa kuwa anawasema sana wanaoikwibia nchi hii. Hata hivyo kwenye mjadala wa sheria ya kutunga Katiba, aliikwenda chaka tena kwa umbali mkubwa, na sijui kama ameshapatikana maana nasikia alikuwa anatafutwa kwa kupotelea chakani.

Lakini nimegundua pia kwenye mambo ya sheria, huyu mama ni mweupe kweli kweli!
 
Acha uongo hakuna walichofanya wakati kuna mpango jimbo la mamam huyu kusaidiwa na IRAN wachimbe mafuta au hufahamu mahusiano mazuri ya familia ya mama huyu na IRAN?

Mhhhhhhhh! SAME kuna mafuta!!!!!!!!! kule milimani, aisee itabidi wachimbe umbali mrefu sana hadi kuja wayapate hayo mafuta.
 
Ni ushamba kumlaumu mtu kama huyu...mpiganaji pekee ninae mkubali..kuumbua mafisadi si kazi ndogo

Nasitasita kuamini ktk hilo la kuumbua, labda uniambie ni mtu anayejua 'kukazia hukumu' zilizopitishwa na wengine. Lakini labda unishawishi kwa kutaja jambo 1 au mawili aliyoyaanzisha personally.
 
Hivi huyu mama si kaolewa Dodoma? Sasa yeye ni mkazi wa Same au Mtera? Watani zangu wapare hebu kuweni serious. msimchague huyo kada wa mafisadi
 
Nasitasita kuamini ktk hilo la kuumbua, labda uniambie ni mtu anayejua 'kukazia hukumu' zilizopitishwa na wengine. Lakini labda unishawishi kwa kutaja jambo 1 au mawili aliyoyaanzisha personally.

Huyu mama hamna kitu kabisa wale aliokuwa anawalipua ilikuwa ni chuki binafsi kwa ajili ya mmewe.Vinginginevyo si kweli kwamba huyu ni mpambanaji,hata ili suala la kumtetea Ngereja ulikuwa ni ujinga mtupu
 
Mh. Anna Kilango ndiye anayekusanya kodi toka kwa wananchi wa Tanzania? Maendeleo yanaletwa kwa kutumia pesa za kodi........labda nyie hamlipi ndio maana hizo barabara hazijengwi au unadhani wanaokusanya kodi wanapeleka pesa mahali bila kuangalia mchango wa hilo eneo katika uchumi wa Taifa? Unafikiria mtavuna tangawizi kiasi gani iweze kutoa kodi ya TShs 900 million gharama ya kujenga kilometa moja ya lami?

Usiwe mwepesi kulaumu bajeti hupangwa na serikali na siyo mbunge.
 
Kelele nyingi tu kumbe hakuna kitu.Naomba wana JF tupeane taarifa za maendeleo majimboni kwa wabunge wanaojifanya wanaongea sana bungeni
 
Hata sendeka hamna kitu alicho fanya jimboni kwake cku zao zina hesabika.

Kwa sendeka ndio hovyo kabisa mkuu... yani nilikua mitaa hiyo siku za karibuni yani hoi kabisa, sijui wanamchaguaje huyo jamaa
 
Acha uongo hakuna walichofanya wakati kuna mpango jimbo la mamam huyu kusaidiwa na IRAN wachimbe mafuta au hufahamu mahusiano mazuri ya familia ya mama huyu na IRAN?
msaada!!!!!!!!
ule ambao mzee malecela alipewa kumsaidia kuingia ikulu mzee kifimbo akamtilia usiku wameshaulipa??? acha kunivunja mbavu mdau
 
Back
Top Bottom