Mama Karume, hapa umechemka!

Mme wake alikuwa RAIS wa ZNZ (anapata marupurupu ya viongozi wastafu wa ZNZ)
Mtoto wake alikuwa RAIS wa ZNZ (Anapata marupurupu ya viongozi wastaafu wa ZNZ)

Kwahiyo anataka Serikali ya JMT nayo impatie marupurupu?

Yes, Makamu wa Rais wa Tanzania, mbona Jumbe anapewa?
 
HUYU HAPA MBELE YA BANGO LA POMBE!!!!

13.jpg
Hilo bango hapo nyuma linatangaza nini vile? hayo si ndio mambo hawayataki na hao uamsho wao sii wanachoma moto bidhaa hizo?
 
Hajaongea ili uupende wala kumfurahisha mtu mkuu, hakupenda kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa bali kueleza yaliyomo moyoni mwake
 
kuwa mke wa kiongozi haimaanishi una busara yawezekana alikupenda kwa sababu we ni mrembo ila kichwani hakujali. Kama si uroho ni nini na uhudumiwe vp ilhali wanao wamepewa 2 walikuwa na vyeo vya kupewa. Karume mwanao kapewa cheo badala ya mshindi wa kura Makamu wa rais Dr. Ghalib Bilal na yule mwanao balozi! unapaswa kushukuru na si kulaum. akili za Uamsho changanya na za kwako si kukurupuka tu
 
yuko sahihi hasa swala la bank kuu angalau kidogo swala la rais wa muungano wazanzibar waliwahi kukamata.lakini gavana bado wala mwanasheria mkuu.Lakini kwa sasa kwa kuwa wanakatiba yao waendelee kivyao na tanganyika kivyetu.Jamani mama anatuaga.
Maaskofu wa TEC wamesema tangu uamsho walete za kuleta hakuna kiongozi wa serikali aliyewanyooshea kidole zaidi ya kuzunguka mbuyu.Hata mama huyu anafikisha ujumbe wa uamsho.LIWALO NA LIWE
 
Sasa huyu mama kakosea wapi tatizo lenu nyinyi mtu akidai haki ya z'bar mnamuona adui yenu pia kasema z'bar inamezwa na tanganyika hata kama angekuwepo mumewe asingekubali hii hali sasa tatizo likowapi na nikweli jiulize swali dogo tu taasisi zote za muungano makao makuu yako wapi hivi nani atakubali dhuluma hadi lini
 
bila muungano, serikali ya tanganyika ingemsaidia vipi mtoto wake kuwa rais? muungano umemfanya mwanae karume awe rais na yeye amekula kwa mgongo wake. mama nyerere atasemaje sasa.....akawaulize kina makongoro kama wanapata upendeleo wowote.....asatafurahi mafuta ya chura...
 
Mme wake alikuwa RAIS wa ZNZ (anapata marupurupu ya viongozi wastafu wa ZNZ)
Mtoto wake alikuwa RAIS wa ZNZ (Anapata marupurupu ya viongozi wastaafu wa ZNZ)

Kwahiyo anataka Serikali ya JMT nayo impatie marupurupu?

Mkuu, hata mimi hapa ndipo ninaposhangaa, anataka JMT imfanyie nini zaidi? Ana shida gani huyu mama????
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom