Mama Karume, hapa umechemka!

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,882
13,171
Mama Karume anaheshimika sana si tu kwa umri wako, bali hata kwa kuwa mke wa Mzee wetu, Mzee Abeid Amani Karume,mmoja wa waasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Nimesoma leo magazeti kadhaa juu ya malalamiko yake kwa Serikali ya Muungano na pengine nitanukuu toka magazeti mfano la Tnzania Daima lal leo Julai 16 2012, linasema:
Mjane wa Rais wa Kwanza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Abeid Aman Karume, Fatma Karume, amesema haoni faida za muungano kwa kuwa serikali hiyo imemtelekeza.
Alisema hadi mauti yanamkuta mumewe alikuwa mkamu wa Rais wa Serikali ya Muungano lakinihakuna kiongozi wa serikali hiyoaliyemkumbuka kwa lolote jambolimalomfanya kuona Muungano huo hauna faida kwake.
........

Fatuma alieongeza kuwa serikali ya Muungano inamkumbuka kidogo sana lakini si kumliwaza na kwamba wakati wa Karume Muungano ulikuwa afadkhali kidogo.
..........


Fatuma ambaye ni mamam mzazi wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, aliitaka serikali ya Muungano kuwa na mgawanyao sawa wa fedha na madaraka.

Gazeti lingine , Mwananchi leo vile vile linaenda mbali zaidi na kusema:(page 4)

Mama Karume pia alifahamisha kuwa alikutana na viongozi wa Kundi la Uamsholililoko Zanzibar na kuwasikiliza na kusema anaunga mkono madai yao.

Maoni yangu:
Imeanzan kthibitika kuwa masualaya uamsho na fujo za Zanzibar zilikuwa na baraka zote za SMZ na pengine baadhi ya viongozi wake.
Sio rahisi Mama Karume akutane na Uamsho ilhali mwanawe Abeid Karume asifahau hilo, na hivyo basi viongozi wa SMZ.
Tanganyika tusijejikuta tuna twanga maji kwenye kini katika hili.

Juu ya Muungano kulalalmikiwa kutomtunza Mama Karume hili linastjaabisha , hasa ukitilia maanani kuwa SMZ ipo na haijafa, na mwanawe alikuwa RAISI WA ZANZIBAR.

Maneno ya huyu mamam nayachukulia kuwa ya kupandikizwa mdomoni na uamsho na si vinginevyo.
Huku Dar es salaam tunajua kuwa wanawe wana biashara kubwa tu,mfano AMANI HOUSE(Mbele ya Serena/Movenpick hotel), huyo mama si wa kulalalama magazetini juu ya kutotunzwa wakti wenye jukumu hilo lwapo, wanabiashara kubwa na hawajafa.

Hulka ya Mama Karume vile vile ina question mark, hivi karibuni kulikuwa na habari ya kurejeshwa kwa kiwanja cha serikali alichokipata kwa ulaghai na hatimaye kuwauzia wafanyabiashara wa ki-asia huko Zanzibar.
Huu ni utapeli.

Kwa muelekeo wa Muungano hatuna haja kwenda mbali zaidi kuchokonoa historia yake na Wazanzibari wanaoheshimika kama kina Diria na wengine, lakini kwa ujumla mchango wa Mama karume sijaupenda.


UPDATED PIECE ON THE NEWS..


bot_tabimg.gif

Monday, 16 July 2012 14:39

0000001mamakarume.jpg


Mwandishi Wetu

WAKATI taifa likiwa katika mchakato wa kuelekea kupata Katiba Mpya, Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Mama Fatma Karume ameibuka na kusema kama mumewe (marehemu Abeid Aman Karume) angekuwapo, baadhi ya mambo yanayofanywa na Serikali kuhusu Muungano sasa asingeyakubali.

Akizungumza katika mahojiano maalumu katika Kipindi cha Kutoka Zanzibar kinachorushwa na Kituo cha Televisheni ya Channel Ten, mwishoni mwa wiki Mama Karume alisema kuwa, Muungano una kero nyingi ambazo sasa zinauingiza katika matatizo.

Alisema kero hizo hata mumewe marehemu Abeid Aman Karume angekuwa hai, asingezikubali.

Mama Karume, ambaye alijinasibu kama muumini mkubwa wa Muungano, alisema mumewe hakuiunganisha Zanzibar ili imezwe bali, alitaka nchi zote mbili za Muungano ziunganishwe na kunufaika kwa usawa.


"Mzee Karume alikubali Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kuwa aliamini, kutatokea taifa moja lenye nguvu," alifafanua Mama Karume na kuongeza:


"Alijifunza kutoka Marekani ambayo ni Muungano wa majimbo mengi na iliyokuwa Muungano wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Sovieti (USSR). Alijua Tanzania nayo itakuwa na nguvu za kisiasa na kiuchumi."

Mama Karume pia alifahamisha kuwa alikutana na viongozi wa Kundi la Uamsho lililoko Zanzibar na kuwasikiliza na kusema kuwa, anaunga mkono madai yao.

Hivi karibuni Kundi la Uamsho lilisababisha kuzuka kwa vurugu zilizoambatana na kuchoma makanisa na kuongoza mijadala mikali ya kupinga Muungano, kiasi cha kufanya baadhi ya viongozi wake kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.

"Unajua vijana wa siku hizi wanajua mengi yanayoendelea kwenye Muungano. Kwa sasa na kwa kweli napenda kusema hawa watu wa Uamsho walinifuata nyumbani na wakanieleza kero zao kuhusiana na Muungano kwa kweli wana hoja," alisema na kuongeza:

"Mimi naupenda sana Muungano lakini, kwa sasa nadhani una matatizo mengi, ambayo yanapaswa kujadiliwa kwa ukweli na uwazi. Nadhani hawa watu wa Uamsho wasikilizwe," alisema Mama Karume, ambaye mumewe aliuawa Aprili 7, 1972 katika eneo la Kisiwandui Zanzibar.


Uteuzi wa watendaji Muungano

Pia Mama Karume alisema kuwa, uteuzi wa viongozi wa taasisi ambazo zinatakiwa kuwa za Muungano una walakini akisema; katika na uteuzi wa mabalozi, Zanzibar ina mabalozi watatu kati ya 33 wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani.


Pia alisema uongozi wa juu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tangu ianzishwe mwaka 1966, hasa Gavana hajawahi teuliwa kutoka Zanzibar.


Alikiri kuwa kuna Naibu Gavana kutoka Zanzibar, lakini alidai chini yake amewekewa watu wawili kutoka Bara. Naibu Gavana, ambaye anatoka Zanzibar anaitwa Juma Reli (Anahusika na Utawala).


"Hivi ni haki kweli Zanzibar kuwa na mabalozi watatu wa Tanzania au kuwa na Naibu Gavana aliyewekewa wasaidizi wawili? Nadhani kuna tatizo hapa. Haya mambo lazima yaongelewe," alisema mama Karume.

Alisema hakubaliani na jinsi suala zima la usimamizi wa fedha linavyosimamiwa na Serikali ya Muungano.


Alisisitiza hata mume wake, Karume angekuwa hai mambo hayo asingekubaliana nayo, kwani tangu mwanzo alikuwa anavutana na Muasisi mwenzake Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.


"Unajua, Mzee Karume alipokuwa hai alikuwa hataki masuala ya fedha na sarafu kuwa ya Muungano. Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kumtuma Waziri wake wa Fedha, Amir Jamal kuja Zanzibar na alikataa kutoa fedha za Zanzibar kwenda Benki Kuu," alisema mama Karume.


Aliongeza; "Baada ya kitendo kile cha kumkatalia Jamal, nilimuuliza Mzee Karume inakuwaje anakataa kutoa fedha zile... Aliniambia kuwa kinachozalishwa Zanzibar kitabakia kuwa cha huku kwani haiwezekani kwa kisiwa kulisha nchi kubwa ya Tanganyika".


Adai katelekezwa

Katika hatua nyingine, Mama Karume alidai kuwa pamoja na kuwa mke wa mwasisi wa Muungano lakini, bado hajanufaika nao.


Mama Karume alilalamika kuwa, ametelekezwa na Serikali ya Muungano licha ya ukweli kwamba, mumewe alifariki akiwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Alilalamika kwamba hajahudumiwa chochote na Serikali ya Muungano tangu mumewe afariki bali amekuwa akihudumiwa na Serikali ya Zanzibar na ndugu zake wa karibu.


"Hawa watu wa Serikali ya Muungano walinitelekeza maana hawajanisaidia chochote tangu Mzee Karume afariki.

"Kinachonishangaza ni wake za Makamu wa Rais wa Muungano waliofuata baada ya Mzee Karume wanaangaliwa na hata kupelekwa nje kwa matibabu," alisema na kuongeza;


"Ninaendesha maisha yangu vizuri, lakini kwa kweli sijasaidiwa na lolote na Serikali ya Muungano pamoja na ukweli kuwa mume wangu ni mwanzilishi wa Muungano huu."


Mtikisiko wa Muungano

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika siku za karibuni, umekuwa ukipita katika kipindi kigumu huku wanasiasa, wanaharakati na wananchi wakihoji muundo wake.


Wafuasi wa Kundi la Uamsho liliko Zanzibar walikamatwa hivi karibuni, wakihusishwa na uchomaji makanisa na uendeshaji wa mijadala ya kuelezea kero za Muungano.


Hata hivyo, malalamiko hayajaanza leo kwani yamekuwako miaka na miaka kiasi cha kufanya mwaka 1984, Rais wa Pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi, Waziri Kiongozi Ramadhan Haji Faki na Mwanasheria Mkuu Bashir Swanzey kulazimishwa kujiuzulu katika kile kilichoitwa kuchafuka kwa hali ya hewa huko Zanzibar.

Tayari suala hilo la Muungano limeanza kuibua mjadala visiwani Zanzibar katika mchakato wa kupokea maoni unaofanywa na Tume ya Katiba chini ya Jaji Joseph Warioba.



 
Kaingia kwenye kumi na nane za Uamsho jamaa wakamuweka kati wakatwanga mbele na nyuma kujashtuka anaimba wimbo wao.
Hata hivyo sisi tunaangalia katiba yetu ya Tanganyika.
 
Sasa kachemka nini.

Mseme nyinyi tu wakisema wao huo mwao?
 
Anataka msafara na pikipiki nini ili ajue tunamtambua? Haka kanchi bana kana vuimbe wa ajabu kama konokono, ngiri, mende, fisi, na jamii flani ya binadamu....
 
Haya kuanzia Mama Karume umetunukiwa cheo cha "Mama Wa Taifa" maana Watanganyika walishajinyakulia kile cha "Baba wa Taifa". Umeridhika mama au unataka uwe pia mwenyekiti wa WAMA? AAAAGRY basi kuwa mwenyekiti wa ANBEN ili uridhike.....

Cheo hicho cha Mama wa Taifa kisipokutosha uje kwa sisi Uamsho tukufanye uwe mtakatifu...


kwa hisani ya Kinyungu toka Kinegembasi
 
Sasa kachemka nini.Mseme nyinyi tu wakisema wao huo mwao?
Mkuu kwa historia ya Tanzania tu, huyu mama inabidi aishi kulingana na matukio yake.Yeye ni kiongozi, apende asipende, inabidi aishi above petty politics and businesses.Mimi ni mmoja siamini kama hapati matunzo ya serikali aidha ya SMZ au ya Muungano.Tanganyika tuko proud sana na Mama Maria, na wananchi tuna note anavyoalikwa nchi mbali mbali kumwakilisha Mwalimu.Kwa matamshi ya Mama Karume,hayana mantiki na public si mahali pake, na ndio maana nasema kachemka!
 
Mkuu kwa historia ya Tanzania tu, huyu mama inabidi aishi kulingana na matukio yake.Yeye ni kiongozi, apende asipende, inabidi aishi above petty politics and businesses.Mimi ni mmoja siamini kama hapati matunzo ya serikali aidha ya SMZ au ya Muungano.Tanganyika tuko proud sana na Mama Maria, na wananchi tuna note anavyoalikwa nchi mbali mbali kumwakilisha Mwalimu.Kwa matamshi ya Mama Karume,hayana mantiki na public si mahali pake, na ndio maana nasema kachemka!

HUYU KAZOWEA KUCHEMKA.........MSOME HAPA.

.Nyumba ya Habari, Matukio na Ushauri: `Kiwanja alichopewa Mama Karume kirejeshwe serikalini`
 
Mkuu kwa historia ya Tanzania tu, huyu mama inabidi aishi kulingana na matukio yake.Yeye ni kiongozi, apende asipende, inabidi aishi above petty politics and businesses.Mimi ni mmoja siamini kama hapati matunzo ya serikali aidha ya SMZ au ya Muungano.Tanganyika tuko proud sana na Mama Maria, na wananchi tuna note anavyoalikwa nchi mbali mbali kumwakilisha Mwalimu.Kwa matamshi ya Mama Karume,hayana mantiki na public si mahali pake, na ndio maana nasema kachemka!

Tukuamini wewe au tumuamini yeye?

Mkiambiwa kweli hamtaki.
 
Huyu mama kachemka sana.yani hakumubuki kuwa miaka kumimiliyopita ni mwanawe wa kumzaa aliyekuwa ikulu ya zanzibar?dr shein ameka ikulu kwakiopindi kisichofik miaka miwili sasa ni nani hasa aliyemtosa huyu mama kati ya shein na mwanae?
 
Tukuamini wewe au tumuamini yeye?Mkiambiwa kweli hamtaki.
Huna haja ya kuniamini mimi mkuu, hayo yote tunasoma wote magazetini.

Sasa la kutapeli viwanja vya serikali nalo la kusingiziwa?

Soma hapo mwenyewe kwa hisani ya link ya Safari-ni-Safari(from ChingaOne Blog)
[h=1]`Kiwanja alichopewa Mama Karume kirejeshwe serikalini`
Fatma%20karume.jpg
[/h]
Kamati ya Baraza la
Wawakilishi inayochunguza ubadhirifu wa mali za Serikali ya Zanzibar imeitaka
serikali kurejesha kiwanja alichopewa kinyume na sheria, mke wa Rais wa kwanza
wa Zanzibar Mama Fatma Karume.
Kwa mujibu wa ripoti ya
uchunguzi kiwanja hicho namba 186 chenye mita za mraba 750 kipo katika mtaa wa
Kinazini, mkabla na Jemgo la historia la Dk. David Livingstone, mjini
Unguja.


Ripoti imeeleza kwamba
kiwanja hicho kilikuwa kikimilikiwa na Wizara ya Kilimo na Maliasili kabla ya
kupewa Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB) kujenga makao makuu yake. Uchunguzi wa
kamati umebaini kuwa ZRB baada ya kupewa uwanja huo walishindwa kuuendeleza
baada ya kupata uwanja mwingine katika eneo la Mazizini na kujenga makao makuu
yake na uwanja ulirejeshwa Wizara ya Ardhi.


Ripoti imesema Wizara ya Kilimo ilitoa kiwanja
hicho kwa ZRB kupitia barua ya Agosti 28, 2002 yenye kumbukumbu WKMMU/29/5/41/72
kwenda Wizara ya Ardhi ya kuwapa ZRB. Uamuzi wa Wizara ya Kilimo na Maliasili
ulikubaliwa na Wizara ya Ardhi na kukabidhi uwanja kwa ZRB Septemba 9, 2002
kupitia barua yenye kumbukumbu namba MUNA/34/14/378/ VOl.1 na kutoa shahada ya
haki ya matumizi ya ardhi ya Aprili 4, 2003.
Hata hivyo, ripoti
imesema baada ya ZRB kupata sehemu nyingine ya kuendelea na ujenzi waliamua
kukirejesha kiwanja hicho serikalini ambapo aliyekuwa Waziri wa Ardhi,
Makazi,Maji na Nishati, Mansour Yussuf Himid, aliamua kiwanja hicho kumpatia
mama yake Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, mwaka
2010.


Akihojiwa na kamati hiyo Desemba 7, mwaka jana,
Waziri Mansour, ambaye sasa ni Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum alikiri
kiwanja hicho kumpa mama Fatma Karume baada ya kumuomba ili aweze kukitumia kwa
shughuli zake za biashara ambazo hazijaelezwa.
Ripoti imeeleza kwamba
baada ya mama Fatma kupewa uwanja huo ndani ya mwezi mmoja aliuuza kwa Kampuni
ya F & K Enterprises Limited, ambapo anamiliki na hisa.
Uchunguzi umebaini kuwa
baada ya mama Fatma na wenzake kupitia kampuni hiyo kukabidhiwa uwanja huo
waliuuza kwa Sh. milioni 150 kwa mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar, Ali Shahib
Khamis, na Waziri kumpatia hati miliki namba L.O.NO Z-53/S.178/2010/186 na
R.O.NO Z-150/2010 ikiwa ni shahada ya matumizi ya ardhi iliyotolewa kwa mujibu
wa sheria namba 12 ya ya ardhi ya mwaka 1992.


Akihojiwa na kamati juu
ya kuuza ardhi hiyo ndani ya mwezi mmoja tangu kupewa mama Fatma, Mansour
alisema hii ilitokana na kampuni yao kushindwa kufikia malengo waliojiwekea na
hivyo kumua kukiuza kiwanja.
Kamati imesema
haikuridhishwa na utaratibu wa kisheria uliotumika kutoa kiwanja cha serikali
baada ya mama Fatma Karume na wenzake kushindwa kuwasilisha nyaraka za
kuthibitisha maombi yao kwa wizara kabla ya kutolewa kiwanja hicho.


“Mpaka tunatoa taarifa
hii hakuna ushahidi wowote ambao mama Fatma aliuwasilisha pamoja na kuahidi
angefanya hivyo kama alivyotakiwa kufanyaharaka iwezekanovyo,” ripoti
imesisistiza. Ripoti imeeleza kwamba kamati ilichukua hatua mbali mbali za
kufuatilia suala hilo ikiwa pamoja na kuwahoji watendaji wakuu wa wizara,
lakini imeshindwa kupata ushahidi wa maombi ya barua ya mama Fatma Karume au
kampuni hiyo.


“Kamati kwa kauli moja
inathibitisha kwamba hakuna ushahidi wa kuombwa kiwanja hicho na hivyo, ina
wasiwasi waziri ametumia vibaya madarakan yake, ameamua kukimilikisha kiwanja
cha serikali kwa mtu bila ya maombi yoyote kinyume na taratibu na sheria,”
ripoti inasema.


Hata hivyo, kamati imesema baada ya Waziri
Mansour kuhojiwa juu ya kukosekana kwa maombi ya wahusika, alisema yalikuwepo
maombi ya kampuni ya F&K Enterpreses LTD katika faili maalum na
alishangazwa na taarifa za kutoweka kwa nyaraka
hizo.
Habari na - MWINYI
SADALLAH




CHANZO:
NIPASHE

 
Mme wake alikuwa RAIS wa ZNZ (anapata marupurupu ya viongozi wastafu wa ZNZ)
Mtoto wake alikuwa RAIS wa ZNZ (Anapata marupurupu ya viongozi wastaafu wa ZNZ)

Kwahiyo anataka Serikali ya JMT nayo impatie marupurupu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom