Injinia
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 849
- 26
Kiongozi hili suala sijui kama limeshatungiwa sheria, nilisikia kuna plan kama hiyo ila sijui maendeleo yake. Kama bado halijatungiwa sheria ndio hivyo tena vijana inabidi waanze mapema ARV, hakuna la zaidi.
Mkuu, swala la kuanza dawa mapema ni gumu kwa sababu:
1. Kinga ya mwili huwa na uwezo wa kujikimu mpaka pale kinga itakapopungua CD4 sawa na au pungufu ya 350/mm3
2. Kuanza dawa mapema kunahusika na madhara mengi zaidi ya dawa
3.Pamoja na kwamba dawa zinatolewa bure Tanzania, haina maana kuwa ni bure haswa, kuna wafadhili na serikali wanaoingia gharama
Na sababu zingine ambazo ni za kisayansi-tiba zaidi, haifai kuwekwa jukwaa hili
Ila kupima mapema ni bora ili pia kinga hii niliyozungumzia iweze kufuatiliwa (follow up) kama inavyostahili ili inapofikia kiwango stahili basi dawa zianzishwe