Mama Fatma Karume athibitisha Karume hakushiriki Mapinduzi ya Jan, 1964! TBC Live

Umejuaje kama sehemu unayoisema ilikuwepo lakini haikuonyeshwa, tupe clip ya hiyo part
popiexo, niliiona hii program iliporushwa kwa mara ya kwanza siku ya Mapinduzi January 12,2009. Tena kama Tido asingekuwa mkurugenzi TBC, program ile isingerushwa, maana ilikuwa tuu sensetive, Mama Karume alizungumza very frank kwa kutoa ukweli mtupu, ambao kwa serikali zetu wasingependa ukweli huo uwekwe hadharani!

Kipindi kinaendelea, watch TBC Live....
 
Ndio maana waliopo madarakani wanavuna mapesa sasa, ili baadae wakiondoka madarakani familia zao ziendelee kuishi peponi.
 
Kweli Nazjaz, ilitelekezwa, ila JK ameisha ikumbuka hivi karibuni, sasa ni full matunzo na kabinti kakapewa ubunge viti maalum!.

Hahahaha...mkuu Pasco umenivunja mbavu zangu....kumbe ubunge nao waweza kupewa kama fadhila? Hii ndiyo Tanzania zaidi ya uijuayo!
 
Wanabodi,

Leo tunapoandhimisha Karume Day, kwa wale wenye access ya TV, please watch TBC Live, Mjane wa Karume, Bi. Fatma Karume, anahojiwa na Susan Mungi kuhusu kifo cha Karume.

Mahojiano hayo yalifanyika miaka ya nyuma na leo ni marudio, kwa kumbu kumbu yangu, nilipoyaona kwa mara ya kwanza, ndipo mbele ya safari alipotoboa siri ya Karume kutoshiriki Mapinduzi actively ambapo alitorokea bara.

Kipindi kimekatishwa, sijui kama kitaendelea.

More up date comming!.

Heshima kwako Pasco.

Tafadhali fafanua kidogo Julius yupi maana kuna mijitu inazunguka huku na kule wakieleza kila aina ya uchafu mzee wa watu.
 
Pasco hii post yako inanithibitishia ukweli wa moja ya makala niliyowahi kusoma hapo wakati fulani kuwa Karume hakushiriki na alitoroka asubuhi ile ya mapinduzi?...na inasadikiwa John Okello ndiye aliyeongoza mapinduzi hayo.....sasa hapa swali linabaki kuwa je kuna umuhimu wa kumuenzi karume na kama upo aenziwe kwa kipi wakati hata hayo mapinduzi yeye hakushiriki?.......Na kwa ni ni historia ya zaznibar haimpi nafasi John Okello kuwa ni mmoja kati ya wanamapinduzi?
 
Heshima kwako Pasco.

Tafadhali fafanua kidogo Julius yupi maana kuna mijitu inazunguka huku na kule wakieleza kila aina ya uchafu mzee wa watu.
Ngongo, niko poa, nataka nijielekeze Karimjee kwenye kukusanya maoni.

Kwa isuue zozote za kitaifa, ukisema Julius, it is the one and only, Julius Kambarage.
 
lakini ifike wakati wananchi tusiwe tunadanganyika na mambo ya kitoto .......mwanae ndio rais wa Zanzibar na mwingine ni balozi wa tanzania ujerumani.......sasa rais wa Zanzibar ambaye ni mwanae inawezekanaje kumsahau mama yake? au kuna matatizo ndani ya familia yao?
 
Pasco hii post yako inanithibitishia ukweli wa moja ya makala niliyowahi kusoma hapo wakati fulani kuwa Karume hakushiriki na alitoroka asubuhi ile ya mapinduzi?...na inasadikiwa John Okello ndiye aliyeongoza mapinduzi hayo.....sasa hapa swali linabaki kuwa je kuna umuhimu wa kumuenzi karume na kama upo aenziwe kwa kipi wakati hata hayo mapinduzi yeye hakushiriki?.......Na kwa ni ni historia ya zaznibar haimpi nafasi John Okello kuwa ni mmoja kati ya wanamapinduzi?
Nicky82, hata kama hakushiriki physically, lakini alishiriki kwenye planning. Hakuna ubishi kuhusu kiongozi wa ukweli wa Mapinduzi yale kuwa ni John Okello na ndie Mwenyekiti wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi, lakini kwa vile Karume, ndie aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar, ndiye aliyeleta Muungano na Nyerere na ndiye aliyeuwawa kwa kupigwa risasi, hivyo kuyatoa muhanga maisha yake kwa ajili ya Zanzibar, anastahili kabisa kuenziwa bila mashaka yoyote, ila pia ili Zanzibar kuwa wakweli, wanatakiwa kumuenzi hata na John Okello japo kwa kutajwa tuu itatosha.
 
lakini ifike wakati wananchi tusiwe tunadanganyika na mambo ya kitoto .......mwanae ndio rais wa Zanzibar na mwingine ni balozi wa tanzania ujerumani.......sasa rais wa Zanzibar ambaye ni mwanae inawezekanaje kumsahau mama yake? au kuna matatizo ndani ya familia yao?

Inawezekana alikuwa anareffer miaka ile ya mwanzo baada ya kifo cha mumewe
 
lakini ifike wakati wananchi tusiwe tunadanganyika na mambo ya kitoto .......mwanae ndio rais wa Zanzibar na mwingine ni balozi wa tanzania ujerumani.......sasa rais wa Zanzibar ambaye ni mwanae inawezekanaje kumsahau mama yake? au kuna matatizo ndani ya familia yao?
Godwine, hii ni simulizi ya kilichotokea enzi hizo baada ya kifo. Ameeleza SMZ haukufanya chochote, wanae, Ali na Amani ndio walimtunza mama yao kwa mishahara yao!, wote wawili walitimuliwa kazi na ndipo dhiki na mateso yalipofuata na hakupata msaada wowote isipokuwa kutoka kwa Julius!. That was then!.
 
1079.jpg
images

Ngongo, niko poa, nataka nijielekeze Karimjee kwenye kukusanya maoni.

Kwa isuue zozote za kitaifa, ukisema Julius, it is the one and only, Julius Kambarage.

Mkuu niliuliza maksudi kwasababu kuna kikundi cha watu sijui wanagharamiwa na nani wanafanya kila hila kubadili historia tukufu ya taifa letu.Hakuna wa kumfanana J Nyerere kama si yeye Tanzania ingekuwa haikaliki,umewahi kujiuliza Tanzania ingeanza kuongozwa na Mkapa au Mwinyi kipindi inapata uhuru hali ingekuwaje.
 
Mahojiano hayo yako so emotional. kama una machozi ya karibu, lazima, utabubujikwa, Mama Karume, anatoa machungu ya moyoni jinsi alivyotelekezwa baada ya kifo cha mumewe, hakusaidiwa hata senti tano na viongozi wa SMS hata kumtembelea tuu na kumfariji kwa kumpa pole.

Msaada wake ulikuwa ni wanae Amani na Ali ambao wote walikuwa wanafanya kazi, ndio walimsupport.

Ukafikia wakati SMZ ikawatimua kazi wanae wote wawili na hapo ndipo maisha ya dhiki, taabu na mateso makuu yakamfika mama huyu...

Mkombozi pekee aliyejitokeza kumsaidia, alikuwa ni Julius, ndie alimpatia pesa, akamnunulia nyumba na kumpatia matumizi.

Mama Karume anazungumza kwa uchungu, machozi yanamtoka...Kipindi kikatishwa!

Kwa hiyo umefahamu fika siku ya mapinduzi ilikuwa ni siku ya kupinduliwa wazanzbari bali sio ukombozi wa wananchi wenyewe,unajua kuwa mwaka 1963 ndio zanzbar ilipopata uhuru ? Na hapo hapo ndipo ilipopata kiti katika umoja wa mataifa ? Huyo mama maneno yake mengine ni mzushi,karume alijibambikia mabilioni ya pesa kawekeza marekani,na amani ananjua muulizeni,karume wake zake wote wana majumba zanzbar mwisho yamekuwa magofu yako kule vuga.

Karume sio mzanzbari halisi,na mtu ambaye wa kuja tu,walipanga na nyerere na yeye kaja zanzbar kuwaeleza wananachi,na kipindi hicho zanzbar ulikuwa unangia tu bila ya passport,kulikuwa na uhuru flani,watu wa africa mashariki walikuwa wanangiliana bila ya tatizo lolote kabla ya mapinduzi uanajua hilo.

Nyerere aliwatumia watu amabo waje zanzbar,wakatoa information na ndipo wakaja kufanya mapinduzi,baada ya mapinduzi karume kajitangaza yeye ni rais,pia waliokufa siku ya mapinguzi hakuwepo sultana hapa,mohd shamte mfalme wa zanzbar alikimbilia uk,na yule ni mzaliwa wa zanzbar,na zanzbar hadi mwaka 1963 kulikuwa hakuna utumwa,wala ubaguzi,nchi ilikuwa huru kabisa,na uchumi wa zanzbar ulikuwa mzuri ukilinganisha na tanganyika.

Mapinduzi ya zanzbar yalishindikizwa na waengereza,na kushirikiana na nyerere,yote ni kwa sababu ya usilamu,ukiangalia hata uganda pia ilikuwa nchi ambayo usilamu ulikuwa ukikuwa kiasi kikubwa na kwa vile nyerere ni christianity ndio alipopeleka jeshi kumpindua iddi amini,nyerere alikuwa mlokole sana,kila muda anakuja wengereza kufanya ibada na ndipo alipofanya njama na hawa wazungu kuja usaambaratisha uislamu zanzbar.

Kiukweli sisi wazanzibar hatufurahii mapinduzi,kwa sababu waliokufa wazee wetu,iwe warabu iwe watu weusi,lakini nawaambia kuwa walikufa siku hio sio waarabu tu,hata weusi wengi tu,tena wazanzbari halisi,mungu atawalipa wale wote mahafidhina walikuja kuuwa wazee wetu zanzbar ameeeeeeen
 
Familia ya Sokoine nayo imetelekezwa vibaya, hii ndio serikali ya CCM

Hivi serikali itasaidia wangapi jamani..ni watanzania wangapi wanaolipa kodi wanaokufa kwa njaa na magonjwa kila siku? Does it mean kwamba mtu akipewa dhamana ya uongozi basi ndo awe mzigo wa walipa kodi yeye na familia yake hata akifa? mpaka leo tunawatunza akina Lowasa et al ambao sioni walitufanyia nini zaidi ya ku-preside ufisadi wa jasho letu! Tufike mahali tutambue kwamba kodi za watanzania maskini siyo 'common heritage of mankind'! Zinapashwa kuwanufaisha watanzania wenyewe..na siyo viongozi ambao wameshaiba vya kutosha! Kama baba yako ni waziri doesnt mean that you should be a minister also. Nina imani watu kama akina mama Nyerere wanakula pension za waume zao. and thats the way it should be. No special favour! Na wala siyo kutuletea hadithi hapa eti serikali itunze familia zao. Ni mawazo kama haya ya 'entitlement' yanawafanya akina Ridhiwani na watoto wa akina Lowassa wanafundishwa ufisadi tuu na kupenda vya bure na mkato mkato.....baada ya kufundishwa maadili ya kuchapa kazi kwa bidii!

Wabongo tunakera sana! wacha watu wachape kazi wale jasho lao! Why special treatment??
 
lakini ifike wakati wananchi tusiwe tunadanganyika na mambo ya kitoto .......mwanae ndio rais wa Zanzibar na mwingine ni balozi wa tanzania ujerumani.......sasa rais wa Zanzibar ambaye ni mwanae inawezekanaje kumsahau mama yake? au kuna matatizo ndani ya familia yao?
Godwine.

Hapo alizungumzia historia yake baada ya kifo cha Karume,mume wake.

Nilivyoelewa mimi halalamiki hali yake kwa sasa hivi. Ni wazi kama mtoto,watoto wake walimsaidia wakati huo ambapo walikuwa wanafanya kazi baada ya kifo. Ni wazi kwa vyeo vya Urais na Ubalozi mama huyu anapata matunzo mazuri tu kwa sasa.
 
lakini ifike wakati wananchi tusiwe tunadanganyika na mambo ya kitoto .......mwanae ndio rais wa Zanzibar na mwingine ni balozi wa tanzania ujerumani.......sasa rais wa Zanzibar ambaye ni mwanae inawezekanaje kumsahau mama yake? au kuna matatizo ndani ya familia yao?

alisahaulika kabl amwanae hajawa rais!! Huko nyuma wakati wqmane si Rais, aliachanizwa serikali balai wanae walikuwa wakimsaidia kama familia (alli na amani).kuna kipindi walifukuzwa kazi hali ikawa tete!!
 
Back
Top Bottom