Mama au mke?

Nyamgluu

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
3,160
1,718
Habari wakuu. Naomba tubadilishane mawazo kwa hili.
Naenda kusoma nje. Mshahara wangu utaendelea kuingia kwenye akaunt yangu ambayo nayo ndio naitumia kwa biashara zangu. Sasa navyoondoka sijui kadi nimpatie mama au mke kwa ajili ya kuendelea ku run shughuli na matumizi mengine. Wife hajui kipato changu taslimu na ni vizuri,ila kwenda kuomba kwa mama inaweza ikawa kero.
Mwalioneje hili?
 
We mwanaume vipi?Yani una mke alafu mama yako ndo asimamie mambo yako?Unless mkeo humuamini linapokuja swala la pesa au unamwona sio smart enough kufuatilia shughuli zako humtendei haki kabisa!Yani unajaribu kutengeneza bomu linaloweza kulipua ndoa yako wakati wowote!Eti mke aende kwa mama kuomba pesa!Nwyz kabla sijaendelea naomba kuuliza kwanini unaonyesha kutokumwamini mkeo?Kwani akiujua mshahara wako utapungua?
 
Hehehe thanx lizzy naona umekuja juu.
Wife bado anapiga kitabu na anaakili sana. Hatakua anaenda kuomba hela coz nimeset kiwango flani kiwe debited kwangu nakuwa credited kwake.
Lakini unajua nyie mabinti mnadharau na kudanganyika kirahisi sana. Kutokana na hivyo unaweza kuta akadanganyika na kushawishika maana anajua kwa uhakika limit ya mumewe no matter how big or small.
 
Duuuu we kaka, yani nafasi ya mke kwako ni ipi?
Umemuoa kwa sababu ya mama yako, au kwa sababu yako na yeye muendeshe maisha. Kwanza nakuhakikishia maisha unayoishi na mkeo sio ya furaha kabisa, haiwezekani mama wa watoto wako hajui kipato chako, hajui unachopata na unachopoteza. Nasikia hsira gafla.

Kaka naomba nikuulize swali hivi ukipanda hiyo ndege halafu kwa bahati mbaya usifike huko unakokwenda, mama yako ndo atasimamia miradi yako na kukulelea watoto wako? Unamweka huyo mkeo ktk mazingira gani, si ndio atafukuzwa na watoto wake kama mbwa??

Biblia inasema hivi, mtu ataachana na mama yake na baba yake, nao watakuwa mwili mmoja, alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe. Asomaye na afahamu. Naishia hapa nitarudi tena.
 
ni mkeo wa ndoa au ni come we stay? kama ni mkeo wa ndoa na una mpango wa kuishi nae maisha yote, utakuwa humtendei haki akumwachia mama yako kadi zako. kwanza hata biblia imesema utamwacha baba na mama na utaambatana na mkeo..tafakari. mi naona kama ni dharau, kutomwamini, kutomthamini, na kutompenda hata kama una reason zako. na akigundua trust me utakuwa umeweka doa kubwa kwenye ndoa yako ambalo will take a lifetime to correct. ungemtrust, pengine ungekuta kipato chako kimeongezeka kwa kuwa anajua ashaolewa na ni jukumu lake kujenga familia yake (wewe na yeye) hana pa kukimbia. kumbuka, ajira tz ni ngumu sana, pengine hiyo biashara ingemkeep busy kabla hajapata kazi na kumwepusha kukaa iddle wakati wote ambao haupo. think...
 
Mkuu ni bora zaidi ukamfanya mkeo kama partner wako, kwenye maisha, hata kama matumizi yake ni mabaya jaribu hata kuanzisha kamradi fulani (ambako sio time consuming) ili aweze kusimamia. Unajua hata kama sio dependable mpe chance, she might surprise you.

Hakuna jambo jema kama kujua kwamba mwenzeko anakuamini kuliko kudhani kwamba anakuona useless, after all wewe mungu akikuchukua yeye ndo atabaki kuokoa jahazi, kwahiyo jaribu kumpa responsibilites hata kama hawezi ajifunze wakati wewe bado upo wa kumsahihisha
 
Duuuu we kaka, yani nafasi ya mke kwako ni ipi?
Umemuoa kwa sababu ya mama yako, au kwa sababu yako na yeye muendeshe maisha. Kwanza nakuhakikishia maisha unayoishi na mkeo sio ya furaha kabisa, haiwezekani mama wa watoto wako hajui kipato chako, hajui unachopata na unachopoteza. Nasikia hsira gafla.

Kaka naomba nikuulize swali hivi ukipanda hiyo ndege halafu kwa bahati mbaya usifike huko unakokwenda, mama yako ndo atasimamia miradi yako na kukulelea watoto wako? Unamweka huyo mkeo ktk mazingira gani, si ndio atafukuzwa na watoto wake kama mbwa??

Biblia inasema hivi, mtu ataachana na mama yake na baba yake, nao watakuwa mwili mmoja, alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe. Asomaye na afahamu. Naishia hapa nitarudi tena.

kwa kweli hata mimi nimeshangaa, na hii inadhihirisha ni jinsi gani wanawake bado tunanyanyasika kwenye ndoa. hii ni sawasawa na kuhalalisha kama ukifa leo mkeo anyang'anywe kila kitu na mama yako au ndugu zako. imeniumiza sana hii aisee
 
Hehehe thanx lizzy naona umekuja juu.
Wife bado anapiga kitabu na anaakili sana. Hatakua anaenda kuomba hela coz nimeset kiwango flani kiwe debited kwangu nakuwa credited kwake.
Lakini unajua nyie mabinti mnadharau na kudanganyika kirahisi sana. Kutokana na hivyo unaweza kuta akadanganyika na kushawishika maana anajua kwa uhakika limit ya mumewe no matter how big or small.

Huyo sio binti ni mke wako!! Labda useme hivi mke wangu anadharau na ni rahisi kudanganyika.
 
kwa kweli hata mimi nimeshangaa, na hii inadhihirisha ni jinsi gani wanawake bado tunanyanyasika kwenye ndoa. hii ni sawasawa na kuhalalisha kama ukifa leo mkeo anyang'anywe kila kitu na mama yako au ndugu zako. imeniumiza sana hii aisee

Yani mpendwa, najaribu kupiga picha huyo mke anajisikia je tu. Manake sio kwamba hakimuumi, na huyo jamaa hana hata marafiki wa kiume wakamshauri!!! Au rafiki ake mkubwa ni mama yake. Daaa wanawake tufanye kazi hii habari ya kuolewa na mtu anakunyanyasa kisa huna kitu haikubaliki!!!!
 
Kusema kweli umeniboa kwa kuonyesha kwamba mkeo hana nafasi inayoeleweka kwenye maisha yako!Mke wako anastahili kuujua mshahara wako na kupokea majukumu yako pale unapokua haupo!Kama walivyosema kina LD hapo juu..unadhani yakikukuta mengine huko mama yako ataenda kwa mkeo kumkabidhi kadi ya benki na miradi au atamwambia njoo uchukue pesa za watoto kila mwezi?After all wewe ndo utakua umesababisha hayo yote kwa kumwonyesha mama yako kwamba mkeo hatoshi kua mmiliki wa mali zako!
 
Habari wakuu. Naomba tubadilishane mawazo kwa hili.
Naenda kusoma nje. Mshahara wangu utaendelea kuingia kwenye akaunt yangu ambayo nayo ndio naitumia kwa biashara zangu. Sasa navyoondoka sijui kadi nimpatie mama au mke kwa ajili ya kuendelea ku run shughuli na matumizi mengine. Wife hajui kipato changu taslimu na ni vizuri,ila kwenda kuomba kwa mama inaweza ikawa kero.
Mwalioneje hili?

Kumuachia Bank card yako mama yako si sawa hata kidogo na ni kumdhalilisha mkeo na inaweza kusababisha ndoa yako kuingia matatani(nategemea huyu ni mke wa ndoa). Sijakupata hapo uliposema mkeo hajui kipato chako na ni vizuri. Je, kuna sababu yoyote iliyokufanya kutoona umuhimu wa mkeo kujua kipato chako?
 
Ok,ok punguzeni jazba wapendwa najua ni topic inagusa. Please twendeni pole pole.
Nampenda sana mke wangu mpaka watu wapumbavu wanasema nimelogwa. Hii ya wife ku run shughuli naona itampa wakati mgumu kwa kasociety kangu kakijinga kanakozua hayo mambo ya kulogwa. Halafu hatuishi kwenye kisiwa hii society ikimkataa wakati sipo ataishije?
VoA asante I am thinking or at least i'm thinking that i'm thinking. Get it? Lol.
 
Yani mpendwa, najaribu kupiga picha huyo mke anajisikia je tu. Manake sio kwamba hakimuumi, na huyo jamaa hana hata marafiki wa kiume wakamshauri!!! Au rafiki ake mkubwa ni mama yake. Daaa wanawake tufanye kazi hii habari ya kuolewa na mtu anakunyanyasa kisa huna kitu haikubaliki!!!!

namna hii kweli kuna umuhimu wa kufanya kazi kwa nguvu na kujijenga kiuchumi. wanaume wengi si wawazi kwa wenza wao kuhusu vipato vyao na hii ni mbaya, ndio maana wajane wanateswa na ndugu na watoto wanateseka mara tu baba anapokufa, ni sababu wanajua mume mwenyewe hakuwahi kumjali mkewe kama partner wake, kwa hiyo wanahalalisha kwamba mjane si familia yao. nikionancho mimi mtu anayefanya hivi anakuwa hajakubali kumuona mkewe kama part ya life yake, i mean, mume anaishi kimachalemachale tu akidhani bado anaishi kwenye u girlfriend na u uboyfriend ambapo anything can happen. ukiamua kuoa ujue ndio mke au mume utaeishi nae milele,(at least for christians) so you better trust her or him, otherwise ni ubatili mtupu, hakuna ndoa hapo.
 
Kumuachia Bank card yako mama yako si sawa hata kidogo na ni kumdhalilisha mkeo na inaweza kusababisha ndoa yako kuingia matatani(nategemea huyu ni mke wa ndoa). Sijakupata hapo uliposema mkeo hajui kipato chako na ni vizuri. Je, kuna sababu yoyote iliyokufanya kutoona umuhimu wa mkeo kujua kipato chako?
Babu wakati natuma post hii sikujua kuwa naweza badilishwa mawazo ndani ya JF haraka hivyo. Pamoja na kua lizzy,LD etc wamejibu kwa hasira sana ila nimewaelewa na hasira zao zimesaidia uelewa huo.
Ndoa yetu ni changa 1 year and a few months. Kuna haja gani ya yeye kujua mshahara kama kila atakacho apata na nikishindwa humueleza?
 
Ok,ok punguzeni jazba wapendwa najua ni topic inagusa. Please twendeni pole pole.
Nampenda sana mke wangu mpaka watu wapumbavu wanasema nimelogwa. Hii ya wife ku run shughuli naona itampa wakati mgumu kwa kasociety kangu kakijinga kanakozua hayo mambo ya kulogwa. Halafu hatuishi kwenye kisiwa hii society ikimkataa wakati sipo ataishije?
VoA asante I am thinking or at least i'm thinking that i'm thinking. Get it? Lol.

Hiyo society sijui ndo jamii yako, inaujinga gani, halafu na wewe unakubaliana na huo ujinga badala ya kuwasaidia watoke kwenye huo ujinga??? So na wewe ni mjinga kwa sababu umeukubali ujinga na unaishi kulingana na huo ujinga?? RE-THINK
 
Ok,ok punguzeni jazba wapendwa najua ni topic inagusa. Please twendeni pole pole.
Nampenda sana mke wangu mpaka watu wapumbavu wanasema nimelogwa. Hii ya wife ku run shughuli naona itampa wakati mgumu kwa kasociety kangu kakijinga kanakozua hayo mambo ya kulogwa. Halafu hatuishi kwenye kisiwa hii society ikimkataa wakati sipo ataishije?
VoA asante I am thinking or at least i'm thinking that i'm thinking. Get it? Lol.

sasa hapa kaka unakuwa hueleweki. we unajali nini jamii yako ikisema umelogwa kwa kuwa tu unampenda mkeo? ni lipi jema kumpenda mkeo au kutompenda? society itamkataa vipi wakati ni mkeo wa ndoa? na vipi ikimkataa wakati ushawaachia na kadi za bank? ataishije? bado inaonyesha unajali sana society yako kuliko mkeo. be a man and act like a real man.
 
Babu wakati natuma post hii sikujua kuwa naweza badilishwa mawazo ndani ya JF haraka hivyo. Pamoja na kua lizzy,LD etc wamejibu kwa hasira sana ila nimewaelewa na hasira zao zimesaidia uelewa huo.
Ndoa yetu ni changa 1 year and a few months. Kuna haja gani ya yeye kujua mshahara kama kila atakacho apata na nikishindwa humueleza?

Mkuu kwanza pole manake ni kweli nilikasirika, ila hebu jieleze vizuri yawezekana una sababu ambazo unadhani ni za msingi wewe kufanya hivo. But mke wako ni mke wako tu hata kama mmefunga ndoa jana kwa sababu hamjaanzia hapo. Naomba kuuliza, Je unamuona mkeo kama sehemu ya maisha yako??
 
Babu wakati natuma post hii sikujua kuwa naweza badilishwa mawazo ndani ya JF haraka hivyo. Pamoja na kua lizzy,LD etc wamejibu kwa hasira sana ila nimewaelewa na hasira zao zimesaidia uelewa huo.
Ndoa yetu ni changa 1 year and a few months. Kuna haja gani ya yeye kujua mshahara kama kila atakacho apata na nikishindwa humueleza?

Ni Bubu siyo Babu hahahahahah. Ndani ya ndoa hakutakiwi kuwe na siri ya aina yoyote ile ikiwemo kipato cha wahusika. Mara tu ndani ya ndoa yeyote ile mmoja wa wahusika akianza kutaka kufichaficha mambo yake basi hapo ndipo matatizo huanzia na hata kuzua balaa ndani ya ndoa.

Bora bubu umetokea,Mkuu zingatia haya.
 
LD. Ni sehemu yangu sana tu. Na labda niongezee kitu,hanyanyasiki kwa lolote na huwa tunawekana wazi kwa vitu vitukeravyo. Pili she has her businesses and she is happy. Ukweli sina mashaka nae LAKINI ukweli pia ni kwamba binadam ni binadam,nimeona mengi kwa ndugu na marafiki kusalitiwa,nami kuumiza kichwa ni ili nami nisije umizwa kama hao wengine.
 
Back
Top Bottom