Mama anasema nioe wa zamani

Apataye Mke Amepata Kitu Chema, Naye Amejipatia Kibali Machoni Pa Bwana!
Achana na mambo ya ..sijui express youself...voda to voda na mengineyo ya kishenzi mkuu.

Kaa chini, tuliza kichwa, dont rush...This is apermanent matter, na usijute baadae wala kumlaumu FULANI!..bE YOURSELF!
 
Siyo chaguzi zote za wazazi ni za heri, nyingine zinaangalia maslahi yao ....

Nilishawahi kuona movie ya wa-Nigeria (true story), Mama alimchagulia kijana wake mchumba. Bahati mbaya huyo mchumba alikuwa taahira (mentally retarded). Mama alifanya hivyo kwa malengo yake, kumbe alienda kwa mganga akapewa madawa na sharti ilikuwa ni kijana wake lazima aoe mke ambaye ni taahira.

Sio chaguzi zote za mzazi ni nzuri/ziko genuine, nyingine zinaangaalia maslahi ya Mama/wazazi na siyo maslahi ya kijana. Ukikubaliana nae, yeye atafaidika kwa kutimiza malengo yake, wewe utakuwa umebeba msalaba ambao utaujutia maisha yako yote.

Kwa wakristo, akifanya wrong choice ajue amejimaliza kwa kuwa huwa hawawezi ku-reverse maamuzi hayo mara baada ya kiapo mbele ya Padre/Mchungaji. "Until death do us part", ni maneno mabaya sana na ni kifungo cha maisha. Kwa sababu ya maneno hayo kuna watu huwa inafika anaombea mwenzi afe ili asonge mbele na maisha yake mengine.

kweli ni maneno makali lakini siombei afe na wala hayo maneno hayatanifanya nifikie hali ya kujifia......ikishindikana kwa upande wangu nitatengua maneno...tutakuja kuzikana tu.
 
mie cjui kwanini cpendi hiyo dana ya kuchaguliana wachumba, nadhani kila mtu amtangulize Mungu wake aombe apate mke/mume mwema, mambo ya kuchaguliana yanakuaga na matatizo msururu......kwanini kanza mama akucahgulie?wengi wanaingia kwenye ulokole cku hizi kwa ajili ya mambo fulani fulani tu....
 
Wakuu nilistaajabu mama alipo nipigia simu na kuniambia nioe mchumba wangu wa zamani ambae tumesoma wote primary toka darasa la kwanza mpaka la saba secondary na kungineko tulisoma tofauti na kila mtu akaendelea kivyake lakini tunapigiana cmu na kupeana hi ishu kubwa mpaka tukatengena yeye ameokoka yupo na Yesu mm bado ananiita wa Mataifa nilimweleza ombi la maza hili kasema atakuja tuongee wadau mchango tafadhari.

At the end of the day kaka, kwani mama ndio anaoa si wewe? Do you feel the girl/woman? Usitake niamini kuwa analosema mama ndio tiki.
 
At the end of the day kaka, kwani mama ndio anaoa si wewe? Do you feel the girl/woman? Usitake niamini kuwa analosema mama ndio tiki.

Muoaji ni mm lakini ushauri, wosia na itifaki lazima vizingatiwe mama ameona mbali
 
Muoaji ni mm lakini ushauri, wosia na itifaki lazima vizingatiwe mama ameona mbali

Sasa mpwa kwa mfano ukakubali ushauri wa mama. Huyu uliyenaye sasa itakuwaje? Manake namwona kama ana kamimba flani hivi.
 
Sasa mpwa kwa mfano ukakubali ushauri wa mama. Huyu uliyenaye sasa itakuwaje? Manake namwona kama ana kamimba flani hivi.

Hahahaha huyu si niliwaambia alinibambikizia hako kamimba maana tokea nikatae mpaka leo yupo kimyaa sijui kweli alikuwa na mimba au alikuwa ananizuga maana kimyaa alikutana na mjanja ningeanza kuhudumia tambala unashangaa miezi inaenda mara mwezi wa 18 hajazaa.
 
Sasa kama umemtosa, si umkamatie huyo mdogo wake ZD ujiunge nasi kumtukuza Mungu?
 
Muoaji ni mm lakini ushauri, wosia na itifaki lazima vizingatiwe mama ameona mbali

Nakubali wazee wanaona mbali, lakini unaweza ukaoa kumridhisha mama then ndoa isi-work out, utamlaumu mama? Inawezekana mama amemuona she's ok, na kuwa angemfaa mwanae (yaani wewe), kumbe ikawa wewe ndio humfai yeye! Ikaja kuonekana kazi ya mama ina doa bure. Kama yupo wa sasa naye unamuambia nini? Kuwa umeona siyo chaguo?
 
Nakubali wazee wanaona mbali, lakini unaweza ukaoa kumridhisha mama then ndoa isi-work out,

Unajua mama anaona miaka inazidi kwenda na mchumba wangu wa zamani yupo yupo tu na anatabia njema safi kabisa kuwa mwandani lakini tunatofautiana kidini yeye ameokoka mm bado ndo maana tupo mbali mbali lakini mama amemkubali na mm namkubali na yeye ananikubali mvutano upo kwenye dini ndo maana mm nimeamua kusaka kifaa kingine ila mama sijamwambia hilo.
 
Muoaji ni mm lakini ushauri, wosia na itifaki lazima vizingatiwe mama ameona mbali

Wewe bana huyu binti unamfahamu vema kuliko hata mama yako kwa sababu ushawahi kuwa nae.Na kwa maelekezo yako inaonyesha wewe mwenyewe ushamzimikia licha ya kuwa mama yako kasema.Kama binti atakubali wewe tangaza ndoa tu sie tusherehekee.Nyie mmetoka mbali bwana na waarabu wa pemba wanajuana kwa vilemba.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom