Mama amfanyia unyama mwanawe

Babu Lao

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
2,043
179
Mtoto Juma ambaye alikuwa akijieleza huku akilia, alisema, "pamoja na kujitetea kwa muda mrefu lakini mama hakunielewa hata kidogo na kuendelea kuning'ang'aniza kwamba mimi ndiye mwizi niliyemuibia fedha zake," alisema na kuongeza:

"Aliniingiza ndani na kisha kunifunga mikono yote miwili pamoja na miguu kwa mpira wa kufungia mizigo kwenye baiskeli na kuanza kunipiga" .

Alidai baada ya kipigo hicho, mama yake hakumfungulia mpira aliokuwa amemfunga miguuni na mikononi hali iliyomlazimu kulala sakafuni kwa siku tatu kabla ya kufunguliwa na kukutwa mikono imevimba.

Kwa mujibu wa mtoto huyo, mama yake alipokuta mikono imevimba alichemsha maji ya moto na kumkanda na alipoona uvimbe haupungui, aliamua kuchukua barafu na kumuwekea kwenye mikono.

Inaelezwa kwamba jana asubuhi ndipo mtoto huyo alifunguliwa na baada ya kutoka nje, alikimbilia barabarani alipokutana na wasamaria wakampeleka kwa Mwenyekiti wa Kitongoji, Sosthenes Mahushi.

Angalizo: Je huyu ni mama mzazi kweli wa mtoto au alimuiba akiwa mdogo?????
 

Attachments

  • Mtoto.jpg
    Mtoto.jpg
    39.1 KB · Views: 127
Nimetoa machozi hivi huu unyama wa namna hii utaisha lini, mtoto wako mwenye uliyemzaa kwa uchungu wa hali ya juu huwezi mfanyia kitendo hicho ninawasi wasi mtoto sio wake.
 
Nimetoa machozi hivi huu unyama wa namna hii utaisha lini, mtoto wako mwenye uliyemzaa kwa uchungu wa hali ya juu huwezi mfanyia kitendo hicho ninawasi wasi mtoto sio wake.

Hilo swali hata mimi nimejiuliza sana!!!
 
Huyu mama ni katili ile mbaya. hasira alizonazo kwa baba wa mtoto ameamua kuzimalizia kwa mtoto wake. mama angalia hasira hizo zitakupeleka pabaya na utakuja jutia
 
Duh!! Juma pole jembe langu,Ni ukatili wa hali ya juu Ingawa sura ya juma imekaa Ki-Maiko Scofield!!!! hakustahili adhabu kama hii.,,
attachment.php
 
hivi jamani hawa wazazi wa namna hii waliumbwa au walitokea kuzimu moja kwa moja, natamani huyu mama hata ningepewa dk 5 za kukaa nae na kumfunza adabu ya namna ya kukaa na mtoto, hebu sheria ya haki za mtoto ya mwaka 1989 ya UN ifanye kazi vizuri hapa Tanzania na co kuiweka kwenye makaratasi tu. Waziri mwenye dhamana ya hili suala hebu toka ofisini shughulikia haya mambo
 
jamani inasikitisha,kitoto kizuri kweli,huyo mama nae aadhibiwe,hasira zake kazimalizia kwa mtoto
 
duh.kama ni kweli.yawezekana ikawa mtoto ashakanywa saana lakini hackii.ila dah hi adhabu imezidi...pia yawezekana mama maisha yanampiga,thts why..Mungu msameh huyu..
 
Back
Top Bottom