Malumbano ya Spika Sitta na Mzee Mrema

Kwa mwendo huu kabla ya uchaguzi ujao Mrema atakua ametangaza kurudi CCM. Sasa neno linatimia kwamba viongozi wengi wa upizani ni wakala wa CCM wa kuteka watu wenye mawazo tofauti na kuwachanganya wakati wa uchaguzi. We TLP unaenda kuongelea mambo ya kukigawa chama cha mapinduzi wapi na wapi? Loh!!!
 
Mimi nina wasi wasi na akili ya Mrema na uwezo wake wa kufikilia. Kuna vitu vingine ambavyo anafanya mpaka unajiuliza mara mbili. Yeye ni kiongozi wa chama cha upinzani sasa anapojitokeza hadharani na kutetea uongozi mbovu wa chama tawala tumuweke kundi gani? Mi nadhani ana depression ya maisha huyu. Hata hivyo hata kwa physical tired he is real off
 
hata chizi saa nyingine anaweza akaongea kitu ambacho kina mantiki ndani yake...mara zote mrema amekuwa akionekana kama vile ni mtu wa kuropoka na kuharibu misimamo ya vyama na sera zake....hivi karibuni alikuja na la kumsifiua kikwete kuwa ni kiongozi mzuri ila anangushwa na wasaidizi wake..na sasa ameenda hatua za mbele zaidi kuweka bayana baadhi ya watu wanao muharibia mkuu wa nchi na chama chake nia thabiti ya kuongoza vizuri!hapa kubwa sio nani kasema nn, ila je anachosema kina ukweli wowowte au ni pumba!!!!!mimi nashawishika kukumbuka principal moja ya kwenye fizikia, wanasema "to every action there must be equal and opposite reaction"..sorry kama nimekosea but hija yangu ni kwamba hili limesemwa na linaweza kuwa na mrejesho sawa na lilivyofika kwa walengwa!..lakini tusiajifiche kwenye vivuli vya vyama vyetu na kusahau kuwa ukweli utasimama hata kama hatuutaki kabisa!.....labda tuangalie mwenendo mzima wa ligi ya richmond, je lowassa alicheza kama mchezaji au alikuwa referee? mi nina uhakika kuwa spika kuna sehemu alilazimika kucheza kama mchezaji,na kuna sehemu akawa mwamuzi!..lakini alivyokuwa akiamua ni watazamaji ndo walikuwa wakiona na hili la mrema pia la kuamuliwa mashabiki!.....
 
Ni wapi na kwa hoja ipi Sita amezungumzia Richmond? Au Lyatonga anaota zama hizi ni kama zake Pale alipoenda kamata dhahabu ya wakubwa uwanja wa ndege akaamrishwa kufunga mdoma na kukaa kimya. Zoezi la kuufunga mjadala wa Richmond liliendeshwa kijasusi na NEC ya ccm na ni kwa namna ile ile Mrema alinyamazishwa kuhusu dhahabu. Sita ndie mwana wa amani wa nchi hii kwa kurizia kuiondoa richmond maana ni nini kingefuata kama angengangania kama sio kura ya lutokuwa na imani na serikali bungeni? Na sote tunafahamu kuhusu mjadala wa richmond aliyeshindwa kutekeleza sehemu yake ni Rais. Kauli ya kwamba watendaji wanamwangusha rais ni ya kisaanii kwani ukweli ni kwamba Rais ndie kikwazo kwa watendaji wake. Mrema kweli kafilisika kisiasa, kimaadili na kimtizamo. Bado kwa akili yake ndogo anafikiri watz bado wanavurugwa na propaganda mfu. Haelewi kwamba utandawazi umewafanya vijana hata wa darasa la saba kumzidi kimtazamo. Mrema ameitosa TLP kwa gharama ya kupewa jimbo la Vunjo kwa huruma ya ccm. Sasa kitakachompata ni pale atakaposhuhudia kimaro akimgalagaza. Kuchanganyikiwa kwake kutazidi. EEH MWENYEZI MUNGU AHSANTE KWA KUTUZUIA KUMPA NCHI MWANDAWAZIMU MWAKA 1995. LEO HII TUNGEKUWA WAPI?
 
Wote ni wababaishaji tu hakuna jipya kati yao wanagombania madaraka na kula tu hakuna kipya hapa
 
hata chizi saa nyingine anaweza akaongea kitu ambacho kina mantiki ndani yake...mara zote mrema amekuwa akionekana kama vile ni mtu wa kuropoka na kuharibu misimamo ya vyama na sera zake....hivi karibuni alikuja na la kumsifiua kikwete kuwa ni kiongozi mzuri ila anangushwa na wasaidizi wake..na sasa ameenda hatua za mbele zaidi kuweka bayana baadhi ya watu wanao muharibia mkuu wa nchi na chama chake nia thabiti ya kuongoza vizuri!hapa kubwa sio nani kasema nn, ila je anachosema kina ukweli wowowte au ni pumba!!!!!mimi nashawishika kukumbuka principal moja ya kwenye fizikia, wanasema "to every action there must be equal and opposite reaction"..sorry kama nimekosea but hija yangu ni kwamba hili limesemwa na linaweza kuwa na mrejesho sawa na lilivyofika kwa walengwa!..lakini tusiajifiche kwenye vivuli vya vyama vyetu na kusahau kuwa ukweli utasimama hata kama hatuutaki kabisa!.....labda tuangalie mwenendo mzima wa ligi ya richmond, je lowassa alicheza kama mchezaji au alikuwa referee? mi nina uhakika kuwa spika kuna sehemu alilazimika kucheza kama mchezaji,na kuna sehemu akawa mwamuzi!..lakini alivyokuwa akiamua ni watazamaji ndo walikuwa wakiona na hili la mrema pia la kuamuliwa mashabiki!.....
Chizi ni chizi tu ukiona chizi anakuchekea jua anataka umpe unachokula
 
Majasho unamtumikia nani?
Umelipwa shiing' ngapi mwenzangu?
Utawasilisha lini majibu ya tafiti hii kwa tajiri yako?
 
jamani kwa maoni haya , mrema yuko sahihi............ ni jambo lisilokubalika kwa spika wa bunge kuzungumzia nje ya bunge jambo lilifungwa mjadala bungeni na yeyey mwenyewe akiwa amekalia kiti cha spika.......... anataka kutuambia kuwa ukumbi wa bnge haumtoshi kufanya siasa zake na sasa ameamua kutumia kila jukwaa analokaribishwa kiwe la harambee, kanisani, miradi ya maendeleo vijijini nk.............. ni mfano mbaya wa spika anayeweza kusimamaia misingi ya utawala bora

mbaya zaidi anatumia sasa mistari ya biblia aliyokariri kutaka ahurumiwe............. ni aibu mwanasiasa kutumia dini kujihami baada ya kushindwa kuelewana na marafiki zake waliompa u-spika alionao.............

kwa kweli amelifedhehesha bunge na hata mimi sinuungi mkono katika uchaguzi ujao wa spika............... nitamuunga mkono naibu wake kama atajitokeza kuutaka kkabiliana na sita..................
 
Chizi hazaminiwi na ukiona mtu anaemdhamini chizi ujue amekusudia kuzifanyia vurugu taaluma kwa manufaa ya kibinafsi. Mrema anapaswa kutambua kwamba watanzania wa leo sio wale wa ..47
 
huyu ni kachero maarufu ,naona sasa anajitaidi kutetea maslai yao na si ya taifa .nani asiyemjua mrema kapandikizwa hivyo hoja zake hazina mantiki kwani aliyoyasema sitta ni kweli yalitokea ,,nakumbuka kauli ya khamisi mgeja (mwenyekit wa ccm mkoa wa shinyanga) ni miongoni mwa watu waliotaka spika atolewe akidai anakivuluga chama mimi na wahangaa hawa makada wa hiki chama hivi tujiulize ccm ni chama cha nani?miaka ya mwanzoni kilikuwa chama cha wakulima na wafanyakazi lakini sasa kimekuwa chama cha wala rushwa na mafisadi .hata mtoto mmdogo hilo analitambua hivyo spika ni mtu sahihi kwa kipindi kama hichi yanasemwa mengi mara tatizo uwaziri mkuu bt i think mtu mkweli upata baraka ekooooo SPIKA SITTA NATAMANI UNGEKUWA RAIS MAANA OUR PRESIDENT YEYE NI VASCO DAGAMA .....................
 
Unapokuwa mwanasiasa na ukashindwa kufikia malengo yako ya kisisa na hasa ikafikia mahali hata ule mkate wa kila siku hupati mara nyingi unaweza kuwehuka.

Hivyo unakuwa tayari kumtumikia mtu au kikundi chochote na kusema chochote wanachokuagiza regardless kina mantiki gani hata kama unaonekana zombie katika jamii.

Hapo ndipo alipofikia mrema. anakula sasa matapishi yake mwenyewe. Sasa wale mafisadi wanamtumia wakidhani bado ana influence katika jamii.

Shame on him. Inatakiwa atambua sasa kuwa haiba yake kwa watanzania imekwisha na angeheshimika kama angestaafu siasa na kwenda kiraracha kulima kahawa na ndizi
 
Kwa kiasi fulani Mrema yupo sahihi jamani maana huyu huyu Sitta ndiye aliwafanya Watanzania tusijue kwanini Richmond imefungwa na mjadala wake bila ya majibu na hukumu nzuri, Bunge haliwezi kuwa kama mahakama jamani
 
Ndugu wana JF naomba tujadili hoja na si watu..........nawasilisha hoja ya Mrema na waandishi wa habari jana dhidi ya Spika

SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA MH.SAMWELI SITTA AMEKOSA SIFA YA KUWA MHIMILI WA DOLA

Ndugu Waandishi wa Habari, leo nimewaiteni ili kutoa dukuduku langu kuhusu baadhi ya viongozi wakuu wa nchi wanavyoleta uchochezi ambao unaweza kusababisha uvunjifu wa amani na utulivu hapa nchini.

Mimi nikiwa mkereketwa wa amani na utulivu hapa nchini, siwezi kukaa kimya wakati kuna viongozi ambao wanatoa kauli za uchochezi ambazo zinaweza kuhatarisha amani na utulivu.

Nimesikitishwa sana na kauli zinazotolewa na Spika wa Bunge Mh Samweli Sitta ambaye amekaririwa na vyombo vya habari akisema kwamba kulikuwepo na mipango ya kumfukuza uanachama wa CCM kwa sababu ya msimamo wake kuhusu suala la Richmond.

Mh Spika ameyasema hayo akijua wazi kwamba Bunge la Jamhuri lilishafunga mjadala huo na ni yeye aliyedai kuwa yeyote atakae aanzisha mjadala huo anapaswa kushughulikiwa kwa mujibu wa kanuni za Bunge. Kwa kauli hiyo Mh Spika amekiuka Azimio la Bunge, jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya uongozi.

Aidha Mh Spika anataka kushawishi watu wamuone kwamba anaonewa katika suala zima la Richmond na kwamba huenda pengine serikali ilikuwa inataka kuficha kitu fulani kuhusu suala la Richmond, ndio maana CCM ilitaka kumfukuza uanachama wa CCM. Huo ni uchochezi, ni sawa na kuwapaka matope viongozi wenzake wa chama na serikali.

Akiwa kama Spika wa Bunge anapaswa kuwa mtu wa kwanza kulinda Azimio la Bunge na si vinginevyo.



SPIKA ALIKUWA MWAMUZI NA MCHEZAJI

Tangu mwanzoni mwa mgogoro wa Richmond Mh Spika alionyesha kuwa alikuwa mchezaji na mwamuzi.

Spika kama mwamuzi anayesimamia haki ndani ya Bunge hakupaswa kuonyesha ushabiki au kujionyesha kwamba anaunga mkono upande fulani, alitakiwa asiwe na upande wowote. Lakini yeye alionyesha kabisa kwamba yuko pamoja na wabunge wanaojiita ‘makamanda wa vita dhidi ya ufisadi’, hapo tayari ana kundi lake. Na hatimaye alifanya ziara mikoani akifuatana na wabunge hao pamoja na wafadhili wao.

Kwa maana hiyo Spika alikuwa mwamuzi na mchezaji kwa wakati mmoja jambo ambalo ni kinyume na utawala bora.

Spika hadi leo anaendelea kuonyesha ukereketwa wake kwa kusema kwamba alinusurika kufukuzwa CCM lakini bado haogopi, bali ataendelea na mapambano. Na anasisitiza kwa kusema kwamba ‘huo ndio ukweli kwani tatizo lipo wapi?’

Hiyo ina maana kwamba ameshaamua kuegemea upande mmoja dhidi ya upande mwingine, wakati yeye akiwa msimamizi wa haki. Je kwa staili hiyo haki itatendeka?

Je, kwa mfano Jaji Mkuu angesema kwamba yeye ni mkereketwa wa vita dhidi ya ufisadi. Je,. watuhumiwa wa ufisadi wangepewa haki yao ya kujitetea mahakamani?

Kwa kauli zake Spika anathibitisha kwamba yeye bado yuko pamoja na wabunge ambao wanajiita makamanda wa vita vya ufisadi. Ambao wanasema hawajaridhika kwa sababu baadhi ya Maazimio ya Kamati ya Bunge bado hayajatekelezwa.

Vile vile kauli za Spika zinawachochea na kuwapa nguvu wanaharakati ambao wanasema wataandamana nchi nzima kupinga jinsi serikali ilivyolishughulikia suala zima la Richmond
JINSI YA KUONDOA MAKUNDI NDANI YA BUNGE

Mgawanyiko ndani ya Bunge hauwezi kuisha kama Spika ataendelea kuwa na makundi. Kwa sababu yeye tayari ameonyesha kwamba ana kundi lake ndani ya Bunge. Na pia ameshindwa kusimamia haki ndani ya Bunge, kwa sababu amekuwa mwamuzi na wakati huo huo mchezaji.

Vile vile analeta migogoro na uchochezi baina ya Bunge na Serikali kutokana na kauli zake. Ili kuleta upendo na mshikamano ndani ya Bunge, na kuondoa migongano na migogoro kati ya Bunge na Serikali, nashauri Mh Spika Sitta ajiuzulu au aondolewe, na asiendelee kuwa Spika wa Bunge lijalo.

Pia namshauri Spika pamoja na hao wabunge wanaojiita makamanda wa vita dhidi ya ufisadi, kwamba endapo hawaridhiki na jinsi serikali ilivyolishughulikia suala la Richmond, wajiondoe CCM, badala ya kuleta uchochezi ambao unaweza kuhatarisha amani na utulivu.


HV huyu mzee kama kafilisika kimawazo na kiuchumi c atafute njia zingine tu za kumuwezesha kujikimu ... Kwanza ni NANI aliyemfanya yeye msemaji wa CCM... coz sababu zote zilizoongelewa hapo zilipaswa kutamkwa na mwanachama wa CCM kwani SITTA naye alizungumza kichama zaidi... mi naona huyu mzee kashaona chama chake khakina mwelekeo anatafuta mlango wa uwani arudi CCM...

Mi simlaumu mrema ..kwanza najua keshazeeka... pengine hata hakumbuki yeye ni mwanachama wa chama gani ...achilia mbali ya kuwa ana wadhifa upi... sitashangaa siku akija na hoja ya nyerere kuwa hai serikali imemficha... au hoja ya kuwa mfumo wa chama kimoja unapaswa kurudishwa....

Nina walaumu hao wanaojiita wanachama na viongozi au watu wa karibu na Mrema... unawezaje kumwacha anaropoka mambo ambayo hayamhusu kwa hgarama pengine za chama bila kuzungumza mambo ya msingi ya chama

****************************************************
ITS BETTER IF U KEEP YOUR MOUTH SHUT....AND PPL ASSUMING THA YOUR A FOOL... RATHER THAN OPEN YOUR MOUTH AND REMOVES ALL THE DOUBTS
 
Majasho unamtumikia nani?
Umelipwa shiing' ngapi mwenzangu?
Utawasilisha lini majibu ya tafiti hii kwa tajiri yako?

Unajua PJ kuna watu humu wametumwa kumchafua Sitta wanataka kuficha source ya mtafaruku wenyewe ambao ni Richmond na ufisadi tuwasahau waliofanya makosa ya ufisadi tuanze kujadili makosa ya Sitta ambayo kimsingi siyaoni kama wao wamelipwa mimi nitakuwa counterpart wao free of charge because personaly i see no wrong to Sitta what has done is according to kanuni za bunge

siku hizi JF imejaa Sitta Sitta kila sehemu badala ya kuilaumu kamati ya bunge ya CCM iliyokaa na kupitisha maamuzi dhidi ya Richmond wanamlaumu Spika why wajilaumu wenyewe Spika alikuwa kama mouth piece tu pale bungeni kila kitu kilikuwa kimeshamalizwa kwenye kamati ya CCM it pains kuona innocent person anafanywa kuwa victim no way
 
Hivi Sitta si spika wa Bunge? Doesn’t he have emancipation power within the bunge regardinfg hoja? Was it not in his power to make sure the bunge made right decisions/ comes to the right conclusion regarding Richmond etc? je alifanya hivyo? kama kweli yeye ni mpiganaji kwanini alikubali kuvunja hoja Ya Richmond?
 
Sitta ajibu hoja za Mrema na sio kumtukana binafsi...yeye mwenyewe alifunga mjadala wa Richmond na alisema atakae ufukua ataadhibiwa na kanuni za bunge..leo hii kwenye makanisa ansema alitaka kufukuzwa kwa ajili hiyo....huo ujasiri wa Siita angetuonyesha wakati bunge lina funga mjadala wa Richmond...unnaaa watanzania hatutaki...........

Aliyefunga mjadala wa Richmond si Sitta ni kamati ya bunge ya CCM yeye alisoma tu maazimio yale asingekuwapo siku ile hata Anna Makinda naibu spika angesoma hata Jenifa Mhagama angesoma
 
Unajua PJ kuna watu humu wametumwa kumchafua Sitta wanataka kuficha source ya mtafaruku wenyewe ambao ni Richmond na ufisadi tuwasahau waliofanya makosa ya ufisadi tuanze kujadili makosa ya Sitta ambayo kimsingi siyaoni kama wao wamelipwa mimi nitakuwa counterpart wao free of charge because personaly i see no wrong to Sitta what has done is according to kanuni za bunge

siku hizi JF imejaa Sitta Sitta kila sehemu badala ya kuilaumu kamati ya bunge ya CCM iliyokaa na kupitisha maamuzi dhidi ya Richmond wanamlaumu Spika why wajilaumu wenyewe Spika alikuwa kama mouth piece tu pale bungeni kila kitu kilikuwa kimeshamalizwa kwenye kamati ya CCM it pains kuona innocent person anafanywa kuwa victim no way

Luteni,

Heshima mkuu wangu. Kuna kitu kimoja wote hapa tunasahau, Sitta ni SPIKA WA BUNGE LA THE REPUBLIC OF TANZANIA… je kama yeye ni kweli mpiganaji na anatetea maslahi ya watu alivyokubali kuvunja hoja ya Richmond alikuwa anatetea watanzania au mshahara wake na posho?

Na je it wasn’t in his power to make sure bunge alikubali kuvunja hoja ya Richmond mpaka haki itokee?
 
Nadhani Mrema anahoja ya msingi kwa Sitta. Sitta kama kiongozi wa bunge amelizika swala la Richomnd mwenyewe halafu analifukulia kwenye madhabahu, kwanini asingekataa kulifunga mpaka serikali iseme kinagaubaga imeyatekeleza vipi maamuzi au mapendekezo ya bunge katika swala la Richmond?
Ni kweli kuwa Sitta anaendekeza makundi ndani na nje ya Bunge na haya yanajionyesha kwa kauli zake zinavyotafunana kila wakati. Nadhani hata ubunge wa Urambo Mashariki upo mashakani kwake, nadhani aende jimboni kujiimarisha zaidi unless otherwise anataka jimbo moja la Dar Es Salaam. Aende Jimbo la Ubungo atapita kiurahisi kabisaaa!!!!

Usiwe na wasiwasi na ubunge wa Six yeye si saizi ya ubunge kama kuupata ataupata hata bila kufanya kampeni kampeni anayofanyiwa na watu wakiwemo kina Mrema inatosha wenyewe hawajui kama wanamfanyia kampeni

kuhusu kufunga mjadala wa Richmond kawaulize wahusika wenyewe kina EL na RA na kamati ya CCM ya bunge Sitta hahusiki yeye nikama redio huwezi kuhoji redio hoji mtangazaji hata mtangazaji hahusiki hoji Mhariri atakueleza alikoipata hiyo habari Period.
 
This is Mrema in his true colours! Huyu mtu tangu mwanzo tulishamshtukia kuwa anafanya kazi ya kishushushu kwenye upinzani. Hana lolote ndio maana kila anakohamia ni migogoro tu. Alianza kwa kugombana na wapambanaji akina Mabere Marando alipokuwa NCCR-Mageuzi akiwa na vibaraka wake akina Prince Bagenda, na baadaye TLP wakampokea bila kujua kwamba wanamkaribisha nyoka. Sasa anafanya kazi za CCM halafu anajiita mpinzani. Hii ni ajabu na kweli. Ukifuatilia hapa kuna fungu limetolewa na mafisadi walewale kwa madhumuni yaleyale ya kifisadi. Wana JF kuweni macho. Chambueni hizi thread, msije mkadanganyika. Sumu ya mafisadi ni kali sana na inasambaa haraka sana.
 
Luteni,

Heshima mkuu wangu. Kuna kitu kimoja wote hapa tunasahau, Sitta ni SPIKA WA BUNGE LA THE REPUBLIC OF TANZANIA… je kama yeye ni kweli mpiganaji na anatetea maslahi ya watu alivyokubali kuvunja hoja ya Richmond alikuwa anatetea watanzania au mshahara wake na posho?

Na je it wasn’t in his power to make sure bunge alikubali kuvunja hoja ya Richmond mpaka haki itokee?


Hivi mlitaka Bunge lifanye nini zaidi kuhusu Richmond? Mapendekezo yalitolewa, mengine yametekelezwa na mengine yapo kwenye hatua ya kutekelezwa. Au kuna wanaodhani kwamba Bunge ndio lingemfuta kazi Edward Hosseah, kwa mfano? This is impossible. Bunge lilifanya kazi yake vizuri na serikali inatakiwa kutekeleza mapendekezo, na ndio maana Spika aliufunga mjadala. Hilo ni kosa? Sidhani kama anastahili shutuma kutoka kwa mtu mchovu kama Mrema. Leave the Speaker alone!
 
Back
Top Bottom