Malumbano ya hoja leo ITV: Nafasi ya Vijana katika siasa za Tanzania

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,564
7,973
Salam Wadau,
Nimepata mwaliko wa kushiriki kipindi cha leo cha malumbano ya hoja katika kituo cha television cha ITV, kitakachoanza kuruka hewani ''live" kuanzia saa tatu usiku.
Mada itakayokuwa mezani ni Nafasi ya vijana katika siasa za Tanzania: Je, vijana wanatumika kama madaraja katika vyama vya siasa Tanzania?

Kwa taarifa ambazo sijazithibitisha zinapasha kwamba miongoni mwa waalikwa ambao watakuwa meza kuu ni pamoja na viongozi wa vijana toka vyama vikubwa vya siasa nchini; Chadema, CCM na CUF. Pia nimedokezwa kuwa Adam Chagulani (Kijana aliyekuwa diwani wa Igoma kupitia Chadema) anatarajiwa kuwepo pamoja na vijana wengine wenye nyadhifa mbalimbali katika vyama vya siasa na mashirika/taasisi mbalimbali za kijamii na kisiasa.

Ningependa kupata mawazo yenu katika mada iliyoko mezani, wakati tukisubiri kuingia ulingoni. Je kuna ukweli kiasi gani katika mada husika? Karibuni kwa mjadala.
 
Rweiyunga asiongoze show, kwa sababu anatabia za kimagambamagamba.
 
waulize hivi kwa nini vijana wanaopewa nafasi kwenye hivo vyama wengi ni wale ambao wazazi wao walishawai kuwa viongozi mfano , riziwani kikwete, nape ,january makamba,antony mavunde ...li boya lemutuz... sioi wa arumeru na wengineo...kwani siasa inarithishwa?upuuzi mtupu
 
Nimekusoma mamito. Maoni yako ni yepi lakini katika hoja iliyoko mezani?
 
Rweiyunga asiongoze show, kwa sababu anatabia za kimagambamagamba.
...afadhali ya Rweyunga Fatuma Almasi Nyangasi ndo usiseme anatabia ya kukatisha waongeaji wanaonekana wanasema ukweli hasa wanapokuwa wanaibana Serikali kulingana na mada inayokuwa mezani;
hiki kipindi cha Malumbano ya Hoja kwa nyakati hizi kimepoteza mvuto kwasababu ya uhoga wa waongozaji wa kipindi chenyewe.
 
Ha ha ha Mwita Maranya to be revealed kesho, Intelijensia ya GR kufanya kazi

Mimi nitakuwepo, nitalinganisha picha iliyoko ktk avatar yake na washiriki watakao kuwepo. Pengine nitagundua mtu anayefanana fanana Mwita Maranya, kisha nitampongeza huyo mwanachadema mwenzangu.
 
mtazamo wangu kwa mada iliyoko mezani;

mi naona ni kweli vijana katika siasa wamekua wakitumiwa kama madaraja, kutokana na kwamba ''siasa za nchi zinazoendelea ikiwepo Tanzania zinatagemea sana historia na SIYO kwenda na wakati'' katika hilo si rahisi kijana kupewa nafasi, na hii ni kwasababu ya elimu duni walionayo viongozi wetu wengi inayowafanya uwezo wao wa kufikiri uwe na mipaka.

Cha kufanya ni sisi vijana kuwa na roho ngumu ya kutopenda kupelekeshwa na kusimamia misingi na kanuni ya uongozi kwa kadri ya elimu na ufahamu wetu jambo litakalo tupelekea tuanze kusilikilizwa na kuwa wa kutegemewa katika kuongoza mambo ya siasa na si kuwa madaraja ya wazee kumiliki nafasi zote katika siasa.
 
Kipindi kina boa kila siku unakuta kuna watu hao hao ukiachilia mbali meza kuu ila wengine mpaka wameshaanza kuboa.

Anyway for this lets wait n see!
 
...afadhali ya Rweyunga Fatuma Almasi Nyangasi ndo usiseme anatabia ya kukatisha waongeaji wanaonekana wanasema ukweli hasa wanapokuwa wanaibana Serikali kulingana na mada inayokuwa mezani;
hiki kipindi cha Malumbano ya Hoja kwa nyakati hizi kimepoteza mvuto kwasababu ya uhoga wa waongozaji wa kipindi chenyewe.

Nadhani watazamaji wa kipindi pamoja na washiriki wa kipindi hicho tunawajibika kuwaeleza ukweli hao watangazaji kama tunadhani hawako fair katika uendeshaji wa kipindi badala ya kulalamika hapa tu.

Bila shaka washiriki wa kipindi wana nafasi nzuri zaidi ya "kuwanyoosha" kutokana na kuwabana kwa hoja wanapokuwa kilingeni.
 
siku ikiwa topic ya malovee nione nitakupa madesa ya ukweli..hizi topic za kisiasa tena siasa za kizushi za bongo sishiriki mkuu

Ha ha haa usinchekeshe mamito Luckymito,
siku ikitokea kipindi cha malumbano ya hoja itv kuna mada ya malovee siku hiyo hapatatosha, wanasema mapenzi yanarun dunia!!!
btw, nakushauri usicheze mbali na siasa kwakuwa zina mchango mkubwa sana katika mafanikio ama kutokufanikiwa kwako kimaisha kwahiyo usthubutu kuipotezee kabisa.
 
Last edited by a moderator:
mtazamo wangu kwa mada iliyoko mezani;

mi naona ni kweli vijana katika siasa wamekua wakitumiwa kama madaraja, kutokana na kwamba ''siasa za nchi zinazoendelea ikiwepo Tanzania zinatagemea sana historia na SIYO kwenda na wakati'' katika hilo si rahisi kijana kupewa nafasi, na hii ni kwasababu ya elimu duni walionayo viongozi wetu wengi inayowafanya uwezo wao wa kufikiri uwe na mipaka.

Cha kufanya ni sisi vijana kuwa na roho ngumu ya kutopenda kupelekeshwa na kusimamia misingi na kanuni ya uongozi kwa kadri ya elimu na ufahamu wetu jambo litakalo tupelekea tuanze kusilikilizwa na kuwa wa kutegemewa katika kuongoza mambo ya siasa na si kuwa madaraja ya wazee kumiliki nafasi zote katika siasa.

Umesema kweli mkuu PrN-kazi lakini pia ni ukweli kwamba kuna baadhi ya vijana wamesoma vizuri na wana uwezo wa kufanya mambo makubwa kwa ajili ya maendeleo ya nchi hii. Unadhani wanapata nafasi za kutosha kufanya kile kinachotarajiwa?
Ukiondoa wale wanaoendelea kukua kisiasa kwa migongo ya majina ya wazazi wao, wale wengine waliotokea familia zilizo nje ya system wamepata nafasi za kutosha kufanya siasa ama wanatumika kwa manufaa ya wazee walioko kwenye mamlaka ya vyama vya siasa wasiopenda kung'atuka?
 
Last edited by a moderator:
Naomba ufafanuzi Kwanza kuhusu maana ya kijana au vijana.nasema hivi kwasababu kuna vijana kiumri lakini wazee kiakili kama NAPE,vilevile kuna wazee kiumri lakini kiakili na fikra ni vijana kama DR SLAA.
 
Back
Top Bottom