Malori ya mkutano wa CCM

Mkutano wa CCM kama chama tawala kinatakiwa kitueleze wametufanyia nini kwa miaka yote ya utawala wao! Sio kuanzisha ligi tena na wapinzani, wakifanya hivyo watazidi kujishushia credibilty. Tunadanganyana tumeweza na tunasonga mbele angali bado tunatambaa wakati wenzetu wanakimbia hata jirani zetu waliotuzunguka.
WAKE UP TANZANIAN.....!!!!!!:angry:
CCM yamwaga mamilioni kuivaa CHADEMA
CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimedaiwa kutumia mamilioni ya fedha kugharimia mkutano wake wa hadhara unaotarajiwa kufanyika leo katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam, katika kile kinachoonekana kujibu mapigo ya mahasimu wao, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


Kinyume na madai ya CCM kwamba lengo la mkutano huo ni kuhamasisha uhai wa chama na kutolea ufafanuzi mambo kadhaa yanayojitokeza ndani ya chama hicho, lakini duru za siasa zimedai kuwa, lengo kuu ni kujipima nguvu na CHADEMA ambacho wiki mbili zilizopita kilifanya mkutano wa hadhara katika viwanja hivyo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Katika mkutano huo wa CHADEMA ambao ulirushwa moja kwa moja na kituo cha luninga cha ITV, maelfu ya wanachama waliofurika, walifika katika viwanja hivyo kwa njia zao bila kusombwa na magari, wala kupokea posho. Ili kuhakikisha mkutano wa leo unafunika ule wa CHADEMA kwa kupata watu wengi, CCM imeamua kuwasafirisha wajumbe wake kwa magari makubwa ya kukodi kama vile malori na mabasi kutoka kila tawi na kuwafikisha katika viwanja hivyo.


Mbali ya kusombwa kwa magari, CCM pia imeamua kugawa bure fulana na kofia, na kuna madai kuwa chama hicho kitatoa posho kwa wanachama wake watakaohudhuria mkutano huo.
Mkakati wa kuhakikisha mkutano huo unapata watu wengi, umesukwa kuanzia ngazi ya matawi, wilaya hadi mkoa kwa zaidi ya wiki moja sasa.


Kana kwamba hiyo, haitoshi, CCM imeandaa baadhi ya wasanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Flava) watakaotumbuiza mapema kabla ya kuanza mkutano kwa nia ya kuwavuta wanachama.
Baadhi ya wasanii hao ni Diamond, Marlaw, Frola Mbasha na wengine wengi ambao walipata kutumika wakati wa mikutano ya kampeni ya Rais Jakaya Kikwete.


Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Uenezi na Itikadi CCM, Nape Nnauye alisema baadhi ya mawaziri na makada maarufu ndani ya chama hicho tawala, watahutubia katika mkutano huo.
Alisema mkutano huo unaotarajiwa kuwa wa aina yake, ulipangwa siku nyingi kwa lengo la kuwakutanisha pamoja viongozi wa chama wa mashina na matawi waliochaguliwa hivi karibuni katika uchaguzi wa CCM unaoendelea katika ngazi mbalimbali.


“Kuna vyombo vimesema mkutano huo utahutubiwa na Mzee Mkapa, Mwinyi. Hiyo sio kweli maana hata mwenyekiti wa chama taifa, Rais Jakaya Kikwete hatakuwepo jukwaani,” alisema Nape.
Aliwataja mawaziri watakaohutubia mkutano huo kuwa ni pamoja na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano), Steven Wassira, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Samuel Sitta, Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) na Kamati Kuu (CC), Abdulrahman Kinana na Nape mwenyewe.


“Mzee Kinana atazungumzia masuala ya katiba na sheria na atatoa kauli kuhusiana na vurugu zilizotokea visiwani Zanzibar na kueleza msimamo wa chama kuhusu kikundi cha Uamsho cha visiwani humo kinachodaiwa kuwa chanzo cha vurugu hizo.
“Wasira atajikita kwenye uchumi, Dk. Mwakyembe atazungumzia jinsi serikali inavyoshughulikia masuala ya uchukuzi, Magufuli atazungumzia utekelezaji wa ilani katika eneo la ujenzi na mkakati wa kuondoa foleni jijini Dar es Salaam,” alisema Nape.

Kama ilivyokuwa kwa CHADEMA, CCM nao wameamua kurusha mkutano huo moja kwa moja kupitia kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC) na Televisheni ya ITV na baadhi ya vituo vya redio.
Aliwataka wananchi, wanachama wa CCM na wakereketwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja hivyo ili kuwasikiliza viongozi wa chama na serikali watakaozungumzia kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015.


CHADEMA yaipa masharti magumu
Akizungumzia mkutano huo wa CCM, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, aliponda juhudi za kukusanya watu ili kuonesha kuwa chama hicho tawala bado kinapendwa.
Akizungumza kutoka Jimbo la Mtama, mkoani Lindi kwa njia ya simu, Dk. Slaa alisema CCM inatakiwa kuwaambia Watanzania na wananchi namna gani imetimiza ahadi zake ilizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, zikiwemo za kuwaletea wananchi maisha bora badala ya kusomba watu kwa magari.

Dk. Slaa aliongeza kuwa, hali za Watanzania kwa sasa ni mbaya mara mbili hata kabla ya uchaguzi mkuu na kila mtu amepigika vibaya, kinyume kabisa na namna alivyoahidiwa na watawala.
CHADEMA pia kimewataka viongozi watakaohutubia wananchi, waseme waziwazi idadi ya viongozi wa CCM waliokwisha vuliwa magamba hadi sasa, tangu wawatangazie Watanzania kuwa wanapambana na watu hao miaka miwili sasa.

“CCM isijisumbue wala kujidanganya kusomba watu na kuaminisha umma kuwa bado inapendwa. Watu wameichoka kwa sababu imewadanganya.
“Tunataka waseme, wamewaleteaje watu maisha bora kama walivyowaambia wakati wa kampeni, na pili waseme ni magamba mangapi yamevuliwa tangu wajitape kufanya hivyo,” alisema Dk. Slaa.
 
Haya bandugu, ukiliona lori limebeba watu wa kuhudhuria mkutano wa CCM jangwani leo hebu tupia namba zake hapa... Nimeliona moja likitokea Mbagala charambe mida hii lenye namba T327AWV FUSO

Namba za nini??
We sema tukiyaona tuyapopoe na mawe!!
 
ikiwezekana hata picha kabisa,mie niko jangwani kwa sasa naona wanaendelea kusomba viti vya plastic vyeupe viko kama 1,000 na kujenga stage na wanaandaa mabango.Full ulaghai ukipita mgao wa 10,000 nitakujuza.



Ingetakiwa wakosekane watu wa kukalia hizo viti! Ingependeza sana!
 
huku kwetu wamevichuku vibibi vichawi vile viwangawanga wameendanavyo huko tunawaombea wapate ajali na ile kosta waliyoenda nayo yani mtaa upo shwali from vigagula ngoja wakamwangushe mwenyekiti wao tena. Watajambamaputo
 
huku kwetu wamevichuku vibibi vichawi vile viwangawanga wameendanavyo huko tunawaombea wapate ajali na ile kosta waliyoenda nayo yani mtaa upo shwali from vigagula ngoja wakamwangushe mwenyekiti wao tena. Watajambamaputo

Na wamevivisha kanga za kikwetwe na tshet zake dah! Hawa wazee bora Mungu ajitwalie kama anataka kutusaidia
 
attachment.php

Mh! Ni kweli at! PCCB wako wapi hapa?
 
Wanapelekwa Jangwani muda huu kwani mkutano unaanza saa ngapi?
Au wao ni solar pannels wanaenda kuzalisha umeme ili utumike mkutano utakapoa anza?

Loh, natumia kimobitel ningekugonga like! Umenichekesha mkuu, ha ha ha ha! Watanzania wafanywa solar panel
 
watatumia mafuso wakidhani sio malari kwani huwajui chichiem wewe,halafu wanachama wa ccm chakula chao kikuu ni nini? tshirt au nini, maana kila mkutano wanapewa wakati kwa sasas nchi haina hata mafuta ya taa ambayo yanatumiwa na watanzania zaidi ya 87% kama nishati ya mwanga,kazi tunayo
 
Chama kinawajali wanachama wake, kama wanatokea kongowe na usafiri wa pamoja upo kuna ubaya gani kuutumia?

Wanawapa V-T-Shirt na Usafiri; Wao Mabig Boss wanasomba Fweza zote Kifisadi; Angalia Nyumba Mafisadi wanakotoka, Hawa watu kwenye Malori wamebebwa toka kwenye Bonde la Mzimbazi Unajua tena Mvua Ikija - Rais anawatembelea kwa Helikopta na kuwatupia Mablanketi... SHIDA TUPU
 
Hivi ati ccm inapimana ubavu na cdm,hiki ni kichekesho yaani tembo apimane ubavu na swala? Wapi na wapi.miaka yote toka uhuru mpaka leo unaanza kuogopa chama cha juzi juzi tu.shame on you ccm
 
Wapinzani presha inapanda presha inashuka..mnaweweseka.

Anaeweweseka na yule analiye copy na kupest event ya mwenzake isitoshe hajui hata mkutano wenyewe una dhamira gani?
 
Nyuso za vijana ziko CDM mioyo yao iko CCM this is the truth.

Teh teh hata nape nae anajiliwaza namna hiyo subiria feedback ktk chaguzi zinazokuja then utabadili mwenyewe statement yako
 
CCM wanapenda watu kuwa wajinga maana mwenye akili timamu hawezi kwenda kushangaa porojo.
 
Back
Top Bottom