Je, Malkia anamiliki eneo ndani ya nchi yetu?

Egongos

Member
Nov 5, 2007
39
8
Ndugu wana JF

Kuna taarifa ambazo sijazithibitisha kwamba, Malkia wa Uingereza anamiliki Eneo Kubwa sana Ndani ya Nchi yetu, ambapo Hata Serikali yetu haina Mamlaka ya Kuingia.

Eneo linasemekana liko Mkoa wa Iringa

Naomba mwenye taarifa kamili anijuze
 
Amekuwa Mmiliki wa ENEO hilo tangu enzi na enzi - hata wakati "Saint-to-Be" anataifisha mashamba kule Arusha ilo shamba/eneo halikuguswa.. Lipo Wilaya/MKOA? ya/wa? NJOMBE.
 
kutowahi kufika nchini sio ishu anaweza kumiliki eneo [asipo yeye mwenyewe kufika, mbona Al- Asawi aliwekeza katika umeme paispo kufika nchini? ishi ni kwamba muanzishaji thread lete source na detailed info na umbea wako
 
Ndugu wana JF

Kuna taarifa ambazo sijazithibitisha kwamba, Malkia wa Uingereza anamiliki Eneo Kubwa sana Ndani ya Nchi yetu, ambapo Hata Serikali yetu haina Mamlaka ya Kuingia.

Eneo linasemekana liko Mkoa wa Iringa

Naomba mwenye taarifa kamili anijuze

Serengeti huko waliko waarabu kwenye vitalu ukifika tu hata simu inakuambia umeingia kwenye ufalme wa waarabu..... IKULU yenyewe inamilikiwa na RA, hakuna cha kushangaa hapo................... Ila siku zao hawa CCM zinahesabika.......
 
Amekuwa Mmiliki wa ENEO hilo tangu enzi na enzi - hata wakati "Saint-to-Be" anataifisha mashamba kule Arusha ilo shamba/eneo halikuguswa.. Lipo Wilaya/MKOA? ya/wa? NJOMBE.

Kwa namna ninavyofahamu, hiyo ardhi unayoizungumzia ni kampuni ya miwati(Tanganyika Wattle Company) iliyopo Kibena Njombe.

Awali inavyosemekana ilikuwa ni mali ya Royal family ya Uingereza na ambapo CDC(Commonwealth Development Co-operation) walikuwa na hisa na TDFL pia nao walikuwa na hisa(sifahamu % ya hisa ilivyokuwa). Baadae(mwishoni mwa miaka ya 80 kama sijakosea), Royal family waliachia hisa zao zote kwa CDC n kufanya CDC kumiliki 85% ya hisa na TDFL Kuwa na 15% ya hisa.

Baada ya hapo sijui kilichotokea, lakini 2005, ikaonekana kama CDC ilikuwa inamiliki 100% ya hisa na hivyo ikauza hisa zake zote kwa Kampuni ya Kenya ijulikanayo kama KALDORA International, inayomilikiwa na masingasinga ambao asili yao ni Iringa na ndiyo wanamiliki Mufindi Paper Mills(zamani SPM Mgololo)

Katika kipindi chote cha mabadiliko TANWAT ilijipanua hadi Kilombero na kujishughulisha na upandaji wa Mi Tiki wakiwa na kampuni ya KVTC, so KVTC ikatenganishwa na TANWAT na ika fall kwa African Forestry ambayo ina misitu Uganda, Gabon na pia South Sudan.

Kwa hiyo nadhani Malkia alishaiacha hiyo ardhi ya Njombe na kama ana ardhi anayomiliki kwa sasa labda itakuwa hiyo ya Kilombero.
 
Ndugu wana JF

Kuna taarifa ambazo sijazithibitisha kwamba, Malkia wa Uingereza anamiliki Eneo Kubwa sana Ndani ya Nchi yetu, ambapo Hata Serikali yetu haina Mamlaka ya Kuingia.

Eneo linasemekana liko Mkoa wa Iringa

Naomba mwenye taarifa kamili anijuze

Kwanza kumbuka, Serikali haina mamlaka ya kuingia hata nyumbani kwako bila kufata kanuni na sheria.

Malkia ana ubalozi hapa Tanzania, hizo ardhi ni mali ya himaya yake na ndio maana anaweza kutundika bendera yake pale na hata Serikali ya Tanzania haina mamlaka ya kuingilia. Kwa hayo, utaona si Uingereza tu bali ni mataifa yote yenye ubalozi Tanzania yanahodhi ardhi yao na halikadhalika kwa Tanzania katika nchi zingine.
 
Well said Mkuu, Anaposema serikali haina mamlaka ya kuingia sijamuelewa, sababu katika hayo mashamba kuna barabara za serikali zinazounganisha kijji kimoja hadi kingine, hakuna restriction yoyote ya mtu kutopita wala kuingia maana maeneo yenyewe yamesogeleana sana na watu na miaka ya nyuma kidogo hawa jamaa walikuwa ndo wanaohudumia vijiji vyote jirani katika utoaji wa chanjo kwa watoto na kina mama waja wazito pamoja na kutoa vitabu kwa shule zinazopakana nao, na hata mpango wa uelimishaji kuhusu maambukizi ya ukimwi wao ndo walianza kabla hata serikali haijaanza na waliunda timu za uelimishaji zikishirikisha wananchi kutoka vijiji 17 vinavyopakana na kampuni na hata mpango wa care and treatment walipouanza walibase zaidi kwa wafanyakazi na wanavijiji wanaopakana nao na hapa serikali ilishirikiana kwa karibu ili kuwaunga mkono. Mambo yamechange kidogo sasa chini ya Singasinga.
 
Kuna shamba lingine kule kilombero limepandwa mitiki nalo wanasema ni la Malkia
 
Kwa namna ninavyofahamu, hiyo ardhi unayoizungumzia ni kampuni ya miwati(Tanganyika Wattle Company) iliyopo Kibena Njombe.

Awali inavyosemekana ilikuwa ni mali ya Royal family ya Uingereza na ambapo CDC(Commonwealth Development Co-operation) walikuwa na hisa na TDFL pia nao walikuwa na hisa(sifahamu % ya hisa ilivyokuwa). Baadae(mwishoni mwa miaka ya 80 kama sijakosea), Royal family waliachia hisa zao zote kwa CDC n kufanya CDC kumiliki 85% ya hisa na TDFL Kuwa na 15% ya hisa.

Baada ya hapo sijui kilichotokea, lakini 2005, ikaonekana kama CDC ilikuwa inamiliki 100% ya hisa na hivyo ikauza hisa zake zote kwa Kampuni ya Kenya ijulikanayo kama KALDORA International, inayomilikiwa na masingasinga ambao asili yao ni Iringa na ndiyo wanamiliki Mufindi Paper Mills(zamani SPM Mgololo)

Katika kipindi chote cha mabadiliko TANWAT ilijipanua hadi Kilombero na kujishughulisha na upandaji wa Mi Tiki wakiwa na kampuni ya KVTC, so KVTC ikatenganishwa na TANWAT na ika fall kwa African Forestry ambayo ina misitu Uganda, Gabon na pia South Sudan.

Kwa hiyo nadhani Malkia alishaiacha hiyo ardhi ya Njombe na kama ana ardhi anayomiliki kwa sasa labda itakuwa hiyo ya Kilombero.

Hii kampuni ya wakenya walionunua Sao Hill Paper Mill ndio wamenunua pia misitu yote kule Njombe iliyokuwa mali ya CDC; maana yake ni kwamba sehemu kubwa ya mkoa wa Njome inamilikiwa na waKenya akiwamo Rais wao mstaafu Moi ambae ana hisa kwenye hiyo kampunu ya masinga singa!! Halafu wabongo mnalalamika kuwa ardhi yenu itapokwa na wageni wakati wenzenu wamekwisha wahi!!
 
Haitakuwa ajabu hata wafalme wa Saudia na UAE wanamiliki maeneo makubwa tu hapa tz.
Ni mashamba ya miwati na chai huko Lupembe na Njombe kama sikosei inaendeshwa chini ya kampuni iitwayo Crown(sorry nimesahau jina)
 
Uwezekano ni mubwa usisahau kule zenji jamaa wa oman anamiliki eneo kubwa sana!
 
Hii kampuni ya wakenya walionunua Sao Hill Paper Mill ndio wamenunua pia misitu yote kule Njombe iliyokuwa mali ya CDC; maana yake ni kwamba sehemu kubwa ya mkoa wa Njome inamilikiwa na waKenya akiwamo Rais wao mstaafu Moi ambae ana hisa kwenye hiyo kampunu ya masinga singa!! Halafu wabongo mnalalamika kuwa ardhi yenu itapokwa na wageni wakati wenzenu wamekwisha wahi!!

usisahau kuwa joseph mungai baba yake ni mkikuyu aliyelowea iringa, wao wakazaliwa iringa so si ajabu kwake kuwavuta wakenya wenzie kuja bongo
 
Ndugu wana JF

Kuna taarifa ambazo sijazithibitisha kwamba, Malkia wa Uingereza anamiliki Eneo Kubwa sana Ndani ya Nchi yetu, ambapo Hata Serikali yetu haina Mamlaka ya Kuingia.

Eneo linasemekana liko Mkoa wa Iringa

Naomba mwenye taarifa kamili anijuze

Walitutawala, wanatutawala na watatutawala tukiendelea kuwa wajinga. Kwani malkia analifanyia nini eneo hilo? Kama halijaendelezwa basi Wizara ya ardhi iligawe hilo eneo kwa watanzania wasio na ardhi na wenye uhitaji.
 
Back
Top Bottom