Elections 2010 Malipo ya Salma Kikwete yazua utata!

Hapo ndipo huwa naona umaana wa "uhandishi" wa habari na si kubebabeba watu au kikundi fulani kwa maslahi binafsi,kwa hakika Mwanahalisi wanazidi kuwaonesha watanzania hali halisi ya viongozi katika taasisi za serikali wanavyotumika katika kufanikisha maslahi ya watu fulani.

Sio "uhandishi," ni "uandishi!" Ok?
 
Mie nafikiri CCM wasingejibu maana all in all she still a first lady and she will be the first lady until another president swear in, so I think she still entitled all the first lady benefits. Changanya na zako

Kwa sheria ipi anapata hizo benefit za kutumia mali za serikali kwa maslahi ya Chama? Usiropoke kabla ya kufanya utafiti!
 
Michelle Obama campaigned for Barack in 2008 elections!
Chelsea Clinton campaigned for Hillary in 2008
Cindy McCain campaigned for John McCain in 2008
Lucy Kibaki did the same, the list goes on and on.
Why not Salma???

they are not using tax payers money on their campaign,salma mkwere does.

open your eyes acha ushabiki
 
Hili gazeti limekwisha mtaani mapema hiyo ni kwa sababu ya watu wengi kulinunua kujua kilichomo au Fisadiz wamepiga bao kwa kuyanunua kwa wingi mtaani ili watu wasipate mwanya wa kusoma utumbo unaofanywa na CCM?
 
Salma Kikwete kortini

picture-4.jpg

Na Saed Kubenea - Imechapwa 15 September 2010

http://www.mwanahalisi.co.tz/print/salma_kikwete_kortinihttp://www.mwanahalisi.co.tz/printmail/salma_kikwete_kortini
salma_206.jpg

SALMA Kikwete, mke wa rais anayemaliza muda wake Jakaya Mrisho Kikwete, aweza kuburuzwa mahakamani kujibu matumizi mabaya ya mali ya umma, MwanaHALISI limeelezwa.
Wakili Mabere Marando alieleza mjini Dar es Salaam jana kuwa amekuwa akipokea maombi ya watu binafsi, vikundi na asasi, vikimwomba afungue kesi dhidi ya Mama Salma kwa "matumizi mabaya ya mali ya umma."
Mama Salma anadaiwa kutumia magari na "usafiri mwingine" wa serikali, kuzunguka nchi nzima kumpigia kampeni mume wake kwa kilichoitwa "mgongo wa kodi za wananchi."
Wakili Marando amesema atamwandikia notisi Mwanasheria Mkuu wa serikali (AG), wakati wowote sasa, juu ya nia ya wateja wake kufungua kesi dhidi ya Salma kama sheria inavyoruhusu.
Katika kesi hiyo, Marando amesema, ataunganisha pia serikali ambayo imekuwa kimya wakati raslimali za taifa zikitumiwa nje ya utaratibu.
"Ninapanga kumburuza Salma na serikali mahakamani. Ni suala la utaratibu tu. Tutataka serikali ieleze ni kiasi gani ametumia kwa muda wote na tutaomba mahakama itamke, pale itakapomwona na hatia, kwamba fedha zote hizo zirejeshwe serikalini," ameeleza Marando.
Alipoulizwa iwapo haihitajiki notisi ya muda mrefu kwa kesi kufunguliwa, Marando alisema anajua inahitajika notisi ya siku 90, "…lakini hili siyo suala la leo na kesho tu. Tutaweza kuendelea na kesi hata baada ya uchaguzi."
Kauli ya Marando inaendana na taarifa za ufuatiliaji ziara za Mama Salma nchi nzima kwa kipindi cha kabla na baada ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi wa madiwani, wabunge na rais.
Taarifa zinasema kikosi cha wafuatiliaji ambacho kimetia nanga hivi sasa mjini Musoma, juzi Jumatatu kiliendelea kunukuu nyendo za mke wa rais katika kampeni za uchaguzi za mume wake.
"Tunachukua taarifa zote za matukio, mahojiano, kupiga picha za mapokezi, mikutano na kurekodi hotuba ambazo zinatolewa katika mikutano ya ndani na ya wazi," ameeleza mmoja wa wafuatiliaji.
Hii itakuwa kesi ya kwanza na ya aina yake kumkabili mke wa rais tangu kupatikana kwa uhuru.
Mpango wa kumshitaki First Lady kwa kumuunganisha na serikali unakuja muda mfupi baada ya mke wa Rais wa Zambia, Thandiwe Banda kuswekwa mahakamani kwa mashitaka ya aina hiyohiyo.
Mama Banda anatuhumiwa kutumia helikopta na magari ya umma kumpigia kampeni mumewe huku akigawa pesa ambazo vyanzo vyake havijaweza kuthibitishwa.
Mmoja wa wafuatiliaji wa ziara za Mama Salma amelieleza MwanaHALISI, juzi Jumatatu kuwa kuna tofauti ndogo kati ya mashitaka dhidi ya mke wa Banda na yale dhidi ya mke wa Kikwete.
Akitoa mfano, mfuatiliaji huyo amesema Mama Salma aliwasili mjini Musoma kwa ndege ya serikali, Septemba 12, Jumapili iliyopita akiwa na mlinzi wake na baadhi ya wahudumu.
Ndege hiyo ya aina ya Fokker yenye namba ya usajili 5H – TGF ni mali ya serikali. Ilikuwa na jumla ya abiria wapatao 10 ingawa ina uwezo wa kubeba abiria 48 hadi 50.
"Alikuja na ndege ya serikali. Dreva wake analipwa na serikali. Alipokewa na viongozi wa serikali. Msafara wake mkoani ulijaa magari ya serikali pia. Hayo ndiyo baadhi ya matumizi mabaya ya fedha na raslimali za umma," ameeleza mfuatiliaji.
Miongoni mwa waliotajwa kumpokea Mama Salma, wakiwa na usafiri wa serikali, ni Mkuu wa Polisi wa Mkoa Robert Boaz, mkuu wa usalama wa mkoa na mkuu wa wilaya ya Musoma, Geoffrey Ngatuni.
Magari yaliyokuwa kwenye msafara ni pamoja na yale ya magereza, usalama wa taifa, OCD, RSO na DSO, wakati yeye, Salma alipanda katika gari aina ya VX – v8 Land Cruiser T206 BJY.
"Katika maeneo mengi tayari tumethibitisha matumizi ya rasliamli za serikali isivyohalali. Katika hili la Musoma, tunataka kuthibitisha iwapo ndege hiyo ya serikali iligharamiwa," ameeleza mfuatiliaji.
Amesema wanachofanya ni kufuatilia ufujaji ambao unaingiza taifa katika umasikini na kuziba fursa za mamilioni ya wananchi kupata elimu, makazi bora, chakula na afya njema.
Mfuatiliaji amesema kinachosikitisha ni kwamba aliyebebwa kwa fedha za umma, kupokelewa na waajiriwa wa serikali, magari ya serikali na muda wa umma, hana ujumbe wa umma bali wake binafsi na mume wake.
Katika mikutano mingi, hasa kabla na baada ya kampeni kuanza, ujumbe wa Mama Salma umekuwa kumpeni za mume wake.
"Chukua mfano wa hapa Musoma. Alipofika Jumapili alikwenda Mwibara, wilayani Bunda. Jana (Jumatatu) alikuwa hapa. Ujumbe ni uleule - kampeni za mumewe," ameeleza.
Mfuatiliaji amesema ujumbe wa Mama Salma ni kuchagua CCM na Kikwete; kuvunja makundi na kuwa wamoja; na kuhubiri kile anachoita "madhara ya kuchagua vyama vya upinzani."
"Katika hali hii anatumia fedha za umma kujenga familia yake binafsi. Je, walipakodi wasio wanachama wa CCM au wasiotaka kumchagua Kikwete mwaka huu, wanafaidika vipi? Wameliwa," anaeleza kwa sauti ya uchungu.
Gazeti lilishindwa kumpata Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Ndege za Serikali, kueleza iwapo ndege aliyotumia Mama Salma ilikuwa imekodishwa au ni bwerere.
Ofisa mmoja wa cheo cha Dispatcher wa mamlaka hiyo aliyejulikana kwa jina moja la Makuru, hata kabla ya kuulizwa swali hilo, alipogundua anayeuliza ni mwandishi wa habari, alikataa kusema lolote akidai kuwa siyo msemaji wa mamlaka.
Kwa kauli yake, Mama Salma aliwaambia wasikilizaji wake mjiniMusoma kuwa lengo la ziara yake ni kuhamasisha viongozi wa CCM kujenga umoja, kuvunja makundi, kupita kwa wananchi kuwaomba wachague CCM na Kikwete.
Alisema kama ni rushwa ilianza enzi za TANU na kwamba "Jakaya kajitahidi kwani nyumba haijengwi siku moja…wanawake watazidi kupewa mikopo…CCM ina wenyewe na itazidi kupeta."
Kufikishwa kwa Salma mahakamani kunaweza kuleta mtizamo mpya kuhusu nafasi ya wake wa marais na majukumu yao.
Aidha, asasi za kijamii ambazo wake wa marais wanaunda mara baada ya waume zao kuingia madarakani, nazo zinaendelea kutiliwa shaka kwa madai kuwa zinakuzwa na kuneemeshwa na "urais."
Alipoulizwa ni lini hasa ataweza kupeleka notisi ya kufungulia mashitaka Salma na serikali, Wakili Marando alijibu, "Unauliza lini? Nasema wakati wowote. Hata kesho. Hili siyo suala la kukawiza."
Mgombea urais wa CHADEMA, Willibrod Slaa, alilaani, wiki mbili zilizopita, kile alichoita Salma kutumia raslimali za taifa kwa faida ya familia yao.
Alikuwa akitaja gharama za usafiri na matunzo kwa waliomo katika misafara yao ambayo ni ya kifamilia zaidi kuliko taifa.
 
Mama Salma Kikwete ni nani katika serikali?

lC.gif
John Bwire​
Septemba 15, 2010
rC.jpg

HIVI Mama Salma Kikwete, mke wa Rais, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ni sehemu ya uongozi wa taifa letu? Kama jibu ni ndiyo ni ibara gani ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayofafanua nafasi yake na wajibu wake kwa Watanzania kwa kuwa mke wa Rais?
Kama jibu ni hapana, ubavu wa mama huyu wa kuzunguka na kutamba mikoani katika mikutano ya hadhara na hafla mbali mbali anazozifanya akikipiga kampeni za wazi wazi za kumfagilia mumewe na chama chake chake cha CCM kwa kutumia rasilimali za umma anautoa wapi?
Tunauliza maswali haya kwa sababu mwenye macho anaona na mwenye masikini anasikia kwamba mama huyu katika kampeni zake na hafla mbalimbali anazoandaliwa zinagharamiwa fedha za walipa kodi wa nchi hii.
Fedha za Serikali ya nchi hii yenye watu wapatao milioni 40 kwa maslahi ya chama chenye wanachama milioni 4.6 tu (idadi ambayo iliwahi kuthibitishwa na makamu mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa).
Ingawa uongozi wa Serikali na chama tawala cha CCM umeweka pamba masikion, ukweli wa mambo ni kwamba mama huyu amekuwa gumzo kwa mambo anayoyafanya hasa anapokuwa mikoani kwa kutumia nyenzo za serikali na kupata heshima zote anazopewa Rais kana kwamba yeye ni sehemu ya taasisi ya Urais.
Anafanya vyombo na taasisi za serikali mikoani na wilayani kuwa na wakati mgumu kiasi cha kughafurika kumsomea ripoti za maendeleo ya mkoa, Polisi kuhangaika huku na kule kuhakikisha usalama wake na katika kufanya hivyo, wananchi wa eneo husika kukwamishwa kwa muda shughuli zao kwa vile ‘Rais asiyetambuliwa na katiba' anapitishwa.
Siyo siri kwamba hadhi ya Urais anayopatiwa mama huyu haikuonekana kwa mama Maria Nyerere, mke, wa muasisi wa taifa hili, Mwalimu Julius Nyerere na wengine wote waliofuata. Huyu ana nini cha ziada na kama anacho kwa nini haianishwi kwenye katiba ili Watanzania tumjue tusishangae na anachokifanya?
Tunadhani wakati umefika sasa wa nafasi ya mke wa Rais kuanishwa rasmi katika katiba Watanzania waujue wajibu na mipaka yake katika uongozi wa nchi hii ili kuondoa mkanganyiko huu ulioletwa na mke wa Rais huyu anayemaliza ngwe yake ya miaka mitano ya uongozi wake.
Ni muhimu kufanya hivyo ili kuanzia kipindi kijacho cha uongozi mke wa yule anayepewa dhamana ya kuingia katika ofisi ya juu kabisa, asipotoke, asibabaike, wala kufanya shughuli zake kwa kubabatisha akiwa ‘First lady' wa nchi hii.
Kwa kuwa atakuwa ‘First lady' wa nchi na siyo wa chama chochote, basi ni lazima tukishikilie kwamba katiba impatie nafasi ambayo itamfanya kuwa mlezi wa taifa kama alivyokuwa Mama Maria Nyerere kuanzia mwaka 1961 hadi mwaka 1985 alivyoondoka Ikulu baada ya Baba wa Taifa kustaafu kwa hiari yake mwenyewe kuliongoza taifa hili.
hs3.gif
 
Michelle Obama campaigned for Barack in 2008 elections!
Chelsea Clinton campaigned for Hillary in 2008
Cindy McCain campaigned for John McCain in 2008
Lucy Kibaki did the same, the list goes on and on.
Then Why not Salma???

The problem is not Salma campaigning for Kikwete, but her use of public funds for the campaigns. Remember the money she is accused of using is not money from CCM! If you don't understand, man, please go to school!
 
Huyu jamaa kapafanya ikulu ni mahali pa familia. Ndugu na wajomba zake wote watahamia huku miaka mitano ijayo_Ona sasa mke, mtoto wote wanatumia rasilimali za nchi kuzunguka nchi nzima kwa kigezo cha kuomba kura.Mbona chaguzi TZ zimepita nyingi na awamu hii ni ya nne hakuna aliyewahi kutumia famialia kuzunguka nchi nzima kwa kampeni Kwa awamu hii kuna nini.Wananchi tujiulize kuna ni,,,,,,,,,,,,,,,,,,??????????????????
 
Tafadhali aliyekwisha pata gazeti la Mwanahalisi la leo tafadhali tujuze yanayo endelea. Siko katika nafasi ya kupata hilo gazeti siku nzima ya leo, tafadhali naomba nipate japo headlines.
Thanx in advance.

Nimeweka scanned copy ya gazeti la mwanahalisi. Bahati mbaya file is too large kuja lote as one doc so kuna page mbili, itakuwa ngumu kusoma kwa flow unless udown load then uweke kwenye world doc ili kupata flow, au print. I am sorry that what I can do.
 
Attachments

  • Scanned Mwanahalisi[1].doc
    1.1 MB · Views: 20
  • Scanned Mwanahalisi[2].doc
    1.5 MB · Views: 21
Alipokuwa moshi alikuwa kila njia anayopita anawatupia akinamama kanga barabarani,
naomba pia mnijuze huyu mama alikuwa mwalimu je bado analipwa mshahara, au alishaacha kazi. Na aliacha kwa kigezo gani wakati walimu nchi hii hawatoshi, mimi naomba afunguliwe mashitaka ya kutoa rushwa na kutumia vibaya madaraka ya mumewe
 
Kubenea is one of our few national heroes like the late Sara-Wiwa of Nigeria. Kwanza, walimwagia tindikali wakajifanya wa kwanza kwenda kumjulia hali hospitalini; pili, wakalifungia gazeti lake kwa muda wa miezi mitatu; tatu, wakaenda kupekuwa ofisi yake kinyume na sheria - kwa ujinga wakabeba computer wakati data zinaweza kukaa kwenye external drives kama flash disk, online encrypted all the time na kadhalika; nne, wamemwomba kujieleza mara nyingi. This guy was born to be a real journalist, hero, savior!
 
Salma Kikwete kortini

picture-4.jpg

Na Saed Kubenea - Imechapwa 15 September 2010

http://www.mwanahalisi.co.tz/print/salma_kikwete_kortinihttp://www.mwanahalisi.co.tz/printmail/salma_kikwete_kortini
salma_206.jpg

SALMA Kikwete, mke wa rais anayemaliza muda wake Jakaya Mrisho Kikwete, aweza kuburuzwa mahakamani kujibu matumizi mabaya ya mali ya umma, MwanaHALISI limeelezwa.
Wakili Mabere Marando alieleza mjini Dar es Salaam jana kuwa amekuwa akipokea maombi ya watu binafsi, vikundi na asasi, vikimwomba afungue kesi dhidi ya Mama Salma kwa "matumizi mabaya ya mali ya umma."
Mama Salma anadaiwa kutumia magari na "usafiri mwingine" wa serikali, kuzunguka nchi nzima kumpigia kampeni mume wake kwa kilichoitwa "mgongo wa kodi za wananchi."
Wakili Marando amesema atamwandikia notisi Mwanasheria Mkuu wa serikali (AG), wakati wowote sasa, juu ya nia ya wateja wake kufungua kesi dhidi ya Salma kama sheria inavyoruhusu.
Katika kesi hiyo, Marando amesema, ataunganisha pia serikali ambayo imekuwa kimya wakati raslimali za taifa zikitumiwa nje ya utaratibu.
"Ninapanga kumburuza Salma na serikali mahakamani. Ni suala la utaratibu tu. Tutataka serikali ieleze ni kiasi gani ametumia kwa muda wote na tutaomba mahakama itamke, pale itakapomwona na hatia, kwamba fedha zote hizo zirejeshwe serikalini," ameeleza Marando.
Alipoulizwa iwapo haihitajiki notisi ya muda mrefu kwa kesi kufunguliwa, Marando alisema anajua inahitajika notisi ya siku 90, "…lakini hili siyo suala la leo na kesho tu. Tutaweza kuendelea na kesi hata baada ya uchaguzi."
Kauli ya Marando inaendana na taarifa za ufuatiliaji ziara za Mama Salma nchi nzima kwa kipindi cha kabla na baada ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi wa madiwani, wabunge na rais.
Taarifa zinasema kikosi cha wafuatiliaji ambacho kimetia nanga hivi sasa mjini Musoma, juzi Jumatatu kiliendelea kunukuu nyendo za mke wa rais katika kampeni za uchaguzi za mume wake.
"Tunachukua taarifa zote za matukio, mahojiano, kupiga picha za mapokezi, mikutano na kurekodi hotuba ambazo zinatolewa katika mikutano ya ndani na ya wazi," ameeleza mmoja wa wafuatiliaji.
Hii itakuwa kesi ya kwanza na ya aina yake kumkabili mke wa rais tangu kupatikana kwa uhuru.
Mpango wa kumshitaki First Lady kwa kumuunganisha na serikali unakuja muda mfupi baada ya mke wa Rais wa Zambia, Thandiwe Banda kuswekwa mahakamani kwa mashitaka ya aina hiyohiyo.
Mama Banda anatuhumiwa kutumia helikopta na magari ya umma kumpigia kampeni mumewe huku akigawa pesa ambazo vyanzo vyake havijaweza kuthibitishwa.
Mmoja wa wafuatiliaji wa ziara za Mama Salma amelieleza MwanaHALISI, juzi Jumatatu kuwa kuna tofauti ndogo kati ya mashitaka dhidi ya mke wa Banda na yale dhidi ya mke wa Kikwete.
Akitoa mfano, mfuatiliaji huyo amesema Mama Salma aliwasili mjini Musoma kwa ndege ya serikali, Septemba 12, Jumapili iliyopita akiwa na mlinzi wake na baadhi ya wahudumu.
Ndege hiyo ya aina ya Fokker yenye namba ya usajili 5H – TGF ni mali ya serikali. Ilikuwa na jumla ya abiria wapatao 10 ingawa ina uwezo wa kubeba abiria 48 hadi 50.
"Alikuja na ndege ya serikali. Dreva wake analipwa na serikali. Alipokewa na viongozi wa serikali. Msafara wake mkoani ulijaa magari ya serikali pia. Hayo ndiyo baadhi ya matumizi mabaya ya fedha na raslimali za umma," ameeleza mfuatiliaji.
Miongoni mwa waliotajwa kumpokea Mama Salma, wakiwa na usafiri wa serikali, ni Mkuu wa Polisi wa Mkoa Robert Boaz, mkuu wa usalama wa mkoa na mkuu wa wilaya ya Musoma, Geoffrey Ngatuni.
Magari yaliyokuwa kwenye msafara ni pamoja na yale ya magereza, usalama wa taifa, OCD, RSO na DSO, wakati yeye, Salma alipanda katika gari aina ya VX – v8 Land Cruiser T206 BJY.
"Katika maeneo mengi tayari tumethibitisha matumizi ya rasliamli za serikali isivyohalali. Katika hili la Musoma, tunataka kuthibitisha iwapo ndege hiyo ya serikali iligharamiwa," ameeleza mfuatiliaji.
Amesema wanachofanya ni kufuatilia ufujaji ambao unaingiza taifa katika umasikini na kuziba fursa za mamilioni ya wananchi kupata elimu, makazi bora, chakula na afya njema.
Mfuatiliaji amesema kinachosikitisha ni kwamba aliyebebwa kwa fedha za umma, kupokelewa na waajiriwa wa serikali, magari ya serikali na muda wa umma, hana ujumbe wa umma bali wake binafsi na mume wake.
Katika mikutano mingi, hasa kabla na baada ya kampeni kuanza, ujumbe wa Mama Salma umekuwa kumpeni za mume wake.
"Chukua mfano wa hapa Musoma. Alipofika Jumapili alikwenda Mwibara, wilayani Bunda. Jana (Jumatatu) alikuwa hapa. Ujumbe ni uleule - kampeni za mumewe," ameeleza.
Mfuatiliaji amesema ujumbe wa Mama Salma ni kuchagua CCM na Kikwete; kuvunja makundi na kuwa wamoja; na kuhubiri kile anachoita "madhara ya kuchagua vyama vya upinzani."
"Katika hali hii anatumia fedha za umma kujenga familia yake binafsi. Je, walipakodi wasio wanachama wa CCM au wasiotaka kumchagua Kikwete mwaka huu, wanafaidika vipi? Wameliwa," anaeleza kwa sauti ya uchungu.
Gazeti lilishindwa kumpata Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Ndege za Serikali, kueleza iwapo ndege aliyotumia Mama Salma ilikuwa imekodishwa au ni bwerere.
Ofisa mmoja wa cheo cha Dispatcher wa mamlaka hiyo aliyejulikana kwa jina moja la Makuru, hata kabla ya kuulizwa swali hilo, alipogundua anayeuliza ni mwandishi wa habari, alikataa kusema lolote akidai kuwa siyo msemaji wa mamlaka.
Kwa kauli yake, Mama Salma aliwaambia wasikilizaji wake mjiniMusoma kuwa lengo la ziara yake ni kuhamasisha viongozi wa CCM kujenga umoja, kuvunja makundi, kupita kwa wananchi kuwaomba wachague CCM na Kikwete.
Alisema kama ni rushwa ilianza enzi za TANU na kwamba "Jakaya kajitahidi kwani nyumba haijengwi siku moja…wanawake watazidi kupewa mikopo…CCM ina wenyewe na itazidi kupeta."
Kufikishwa kwa Salma mahakamani kunaweza kuleta mtizamo mpya kuhusu nafasi ya wake wa marais na majukumu yao.
Aidha, asasi za kijamii ambazo wake wa marais wanaunda mara baada ya waume zao kuingia madarakani, nazo zinaendelea kutiliwa shaka kwa madai kuwa zinakuzwa na kuneemeshwa na "urais."
Alipoulizwa ni lini hasa ataweza kupeleka notisi ya kufungulia mashitaka Salma na serikali, Wakili Marando alijibu, "Unauliza lini? Nasema wakati wowote. Hata kesho. Hili siyo suala la kukawiza."
Mgombea urais wa CHADEMA, Willibrod Slaa, alilaani, wiki mbili zilizopita, kile alichoita Salma kutumia raslimali za taifa kwa faida ya familia yao.
Alikuwa akitaja gharama za usafiri na matunzo kwa waliomo katika misafara yao ambayo ni ya kifamilia zaidi kuliko taifa.

Siku za nyuma nilifahamu kuwa ni majambazi tu ubadilisha number plate za magari yanapofanya ujambazi, na gari upewa usajili mara moja tu. Sasa hawa CCM wanabadilisha namba za magari kama majambazi yanapokwenda kuiba, CCM wanabadilisha wanapotumia vibaya fedha yetu ya kodi, hivi wao pia sio majambazi kwa kutumia mbinu ya majambazi?
 
Michelle Obama campaigned for Barack in 2008 elections!
Chelsea Clinton campaigned for Hillary in 2008
Cindy McCain campaigned for John McCain in 2008
Lucy Kibaki did the same, the list goes on and on.
Why not Salma???

Yes they all campaigned for their close relatives who were vying for a presidential position. But they never used tax payers money from the nation's coffers. In fact all their campaign monies were disclosed for public scrutiny. Here we have a first lady who is using tax payers money and othet government facilities to campaign for his husband who is the incumbent vying for presidency which is not acceptable even in the USA.
 
Michelle Obama campaigned for Barack in 2008 elections!
Chelsea Clinton campaigned for Hillary in 2008
Cindy McCain campaigned for John McCain in 2008
Lucy Kibaki did the same, the list goes on and on.
Why not Salma???

Michelle used money from the Obama Campaign team to campaign for her husband (The obama campaign team collected money from even beggers in the street). Chelsea clinton and Cindy the same as michelle they have a campaign team which happened to disclose their financial position before they even start the campaign (if you remember the Clinton saga of cash shortage that led her to endorse an assurance that she will be to campaign until the end). Lucy Kibaki I do not know whether she even campaign for her husband since she is a very controversial lady. The issue with Salma is the usage of public funds (our taxes) to finance her campaign trails for her husband. She and CCM campaign team have been trying to prove that she is not using public funds. They should show us the evidence that they are not using public funds for campaign.

Unless there is credible evidence I am short to believe what they are saying. Likewise, Raj I think gives us the reason to convince us that she is not using public funds.
 
Kubenea is one of our few national heroes like the late Sara-Wiwa of Nigeria. Kwanza, walimwagia tindikali wakajifanya wa kwanza kwenda kumjulia hali hospitalini; pili, wakalifungia gazeti lake kwa muda wa miezi mitatu; tatu, wakaenda kupekuwa ofisi yake kinyume na sheria - kwa ujinga wakabeba computer wakati data zinaweza kukaa kwenye external drives kama flash disk, online encrypted all the time na kadhalika; nne, wamemwomba kujieleza mara nyingi. This guy was born to be a real journalist, hero, savior!

Unasema kweli kabisa, hakuna mwandishi mwenye ujasiri kama yeye hapa TZ!!!
 
Back
Top Bottom