Malipo ya king'amuzi cha Dstv yanatisha

watanzania hawajui haki yao mimi nimegoma kulipia takribani miezi mitano sasa juzi juzi walinipigia kwa nini sijalipia, niliwaambia sina hela ya kuchezea na wakakata simu. Naamini kabisa wataeje dstv wakiamua kulazimisha bei ishuke inawezekana kabisa

Nimelipia mpaka tar...15/2/2012 ikiisha tu naachana nao kabisa. Ni bora kuonyesha mikanda ya lufufu mara mia kuliko kuendelea kufaidisha makaburu.
 
nipe jamani maana hawa startimes dah mpka upate frequency ya TBC ndo ungalie kingamuzi sasa nlipo dah locatino mbovu
 
Nyie wote mnaoomba namba za hao vishoka kuweni makini pia na wewe unayehitaji wakuPM kuwa makini wako humuhumu watu wa DSTV watakuPM kama wanahitaji huduma yako kumbe wanataka kukukamata.Nakumbuka kipindi cha nyuma niliwahi kuja humu JF na issue ya jinsi ya kupata free channeli za DSTV zilikuwa kama 12 hivi nakumbuka kuna mtu aliniPM nikamwelekeza jinsi ninavyozipata bure baada ya kama wiki hivi zikapotea kabisa,halafu siku nyingine mwingine akaniPM akiniuliza vp bado unazipata zile chaneli?sikumjibu chochote,Kwa hiyo kuweni makini.
 
Watz wenye hisa dstv hami mpungwe na yule mzee mwenye upara ana daraja kuelekea kusini .galama ya abuzabi tv ni chini sana kwa mwaka unalipia dola mia tu
 
Hakuna unyonyaji wowote hapa huu ni upuuzi, hakuna binadamu anayehitaji kuangalia DSTV ili maisha yake yaende vizuri. Tena ni bora utafute hobby zengine za maana ujieldeleze kifikra kuliko kuangalia TV.

DTSV ni gharma kwa vile kununua rights za kurusha vipindi bora ni gharama, kupata rights za soccer/movies/series nzuri inachukua mabilioni ya dollar, na mwishoni gharama hizo lazima ziende kwa mteja. Ndo maana hizi kampui zengine vipindi vyao vinawaboa, hawajawekeza kwenye kununua content na ndo maana bei zao nafuu, kwa kifupi you get what you paid for.

GTV walijifanya cheap, wako wapi sasa? Gharama za uendeshaji ziliwashinda wakafilisika.

Pia sio kinyume cha sheria kupanga bei kutokana na dollar, wangekataa kupokea shillingi kungekuwa na tatizo ila wanachofanya ni kujilinda na uporomokaji wa thamani ya shillingi ndo maana wanaangalia exchange rate. Kivingine ingebidi wabadilishe bei kila siku kulingana na shillingi inavyoporomoka hii inaongeza gharama za uchapishaji/labeling na gharama hiyo ingebebwa na mteja.
 
Mie nina channel za mpira na nina miezi6 sijalipa,mbona vishoka wapo,tena wanatoka hukohuko,tena ukula ball bila mashaka,vuta mshiko tu.
 
kinachotuweka weng dstv n soka tu..siku kampun nyngne ikianza kuonesha tu epl, dstv soko lao kushney....btw, dom kuna ile cable kampan, unalipa buku ten tu kwa mwez, ina michannel kibao ya kiarabu hyo mech hata za carling wanarusha...ikija jjn hapa mbn dstv watafunga ofcn ndan ya mwez.
 
Dstv siku hizi kila kukicha wanapandisha gharama ya malipo ya king'amuzi chao, je kampuni hii imeshakuwa ya kifisadi? Kwa sasa malipo yamefikia shilingi 180,000/: kwa mwezi, huu c unyonyaji! Hawaoni kwamba tunawafanyia Kazi wao, ama kweli kaburu ni kaburu hata ukimpaka rangi habadiliki. Wadau nauliza hakuna mamlaka inayoweza kuzibiti unyonyaji huu?. Nawasilisha.

Siyo kweli mimi nimelipa Tsh 125,000/= kwa Dstv Premium kwa mwezi huu wa pili.Kama umeliapa hiyo umeibiwa na hapo ulipolipia.Kama vipi wapigie numba hii kwa msaada zaidi...0787600096/7.Vinginevyo hayo ni majungu mtu wangu..
 
Back
Top Bottom