Wote tunalipa kwa dola. Unapofika pale unaambiwa rate ya dola kwa siku hiyo ndio unatoa hayo madafu yako. Kwa nini serikali yetu imeshindwa kuwadhibiti hawa jamaa? Mbona kwenye mitandao ya simu imeweza? Mbaya zaidi ni kuwa hata usipofungua king'amuzi siku hiyo pesa bado inatafunwa tu. Anguko la shilingi yetu linachangiwa na mambo kama haya pia.Kwanza unatakiwa ujue sio wote wanaolipia kwa dola, pili kwa wanaoangalia majumbani au wanaoonyesha bila kiingilio wanalipa 120,000/: na wanaotoza kiingilio wanalipia 180,000 kwa mwezi. Kama unataka risiti njoo nikuonyeshe.