Mali za Muluzi zakamatwa; za BEN Vipi?

Jibaba Bonge

JF-Expert Member
May 6, 2008
1,246
401
Mali za Muluzi zakamatwa Malawi

bul2.gif
Ni magari 44, jumba la biashara
TAASISI ya Kuzuia Rushwa nchini Malawi (ACB) imekamata mali za rais wa zamani wa nchi hiyo, Bakili Muluzi, kama dhamana katika kesi ya rushwa inayomkabili.
Hatua hiyo ya ACB imechukuliwa wakati bado inaendelea na uchunguzi katika kesi hiyo ambayo Muluzi anadaiwa kuingiza kwenye akaunti yake fedha za wafadhili zinazofikia dola za Marekani milioni 11.
Taasisi hiyo imesema kwamba imekamata jumba analoishi lenye thamani ya mamilioni ya fedha lililoko katika mji wa biashara wa Blantyre. Imesema pia ya kuwa imekamata magari 44 kati ya magari 149 ambayo rais huyo wa zamani wa Malawi anamiliki.
Vingine vilivyokamatwa ni jumba lake la biashara la Keza Office Park ambalo lilizinduliwa kwa mbwembwe, mgeni mwalikwa wakati huo Rais wa Tanzania, Benjamin Mkapa, na akaunti zake zote za benki.
Habari zinasema wakati hayo yakiendelea, Muluzi mwenyewe yuko Uingereza kwa matibabu.
Ofisa Uhusiano wa ACB, Egrita Ndala, amekaririwa na gazeti la kila siku la Malawi- The Daily Times, akisema taasisi hiyo bado inaendelea na uchunguzi wake.
" Kikosi cha Kupambana na Rushwa (ACB) bado kinaendelea na uchunguzi wa mali nyingine ili kujiridhisha na umiliki wake. Ni vigumu kwa sasa kusema mali nyingine ambazo zimepangwa kuchukuliwa, " alisema Ndala.
Katika hatua nyingine, kabla ya tukio hili la wiki hii, hivi karibuni rais huyo wa zamani wa Malawi alizuiwa kusafiri kwenda Uingereza na pasi yake ya kusafiria ikanyang'anywa baada ya kuzuka uvumi kwamba angetorokea Uingereza.
Hata hivyo, aliruhusiwa kuondoka kabla ya ACB kuvamia mali zake kama dhamana endapo atashindwa kesi hiyo na hatarejea nchini humo.
Habari kutoka nchini humo zinasema ya kuwa mwanasheria wa Muluzi, Jai Banda, ameomba zoezi la kukamata mali za Rais huyo lisitishwe. Muluzi aliwahi kukamatwa huko nyuma kwa kwa kesi hiyo hiyo.

Source: Raia mwema 5-11

My take:
Hivi mkuu wetu wa kaya hawezi kujifunza hapa au kwa Mwanawasa (RIP)?
 
Last edited:
Kizuri huwa kinaigwa,lakini kwa Tanzania the story is extremely different,tunaiga vibaya!Mungu atusaidie sana.Under normal circumstances ni kweli mali za Mkapa zinapashwa kukamata, of course na za wengine wengi,lakini nani amfunge paka kengele?

Mali za Muluzi zakamatwa Malawi

bul2.gif
Ni magari 44, jumba la biashara
TAASISI ya Kuzuia Rushwa nchini Malawi (ACB) imekamata mali za rais wa zamani wa nchi hiyo, Bakili Muluzi, kama dhamana katika kesi ya rushwa inayomkabili.
Hatua hiyo ya ACB imechukuliwa wakati bado inaendelea na uchunguzi katika kesi hiyo ambayo Muluzi anadaiwa kuingiza kwenye akaunti yake fedha za wafadhili zinazofikia dola za Marekani milioni 11.
Taasisi hiyo imesema kwamba imekamata jumba analoishi lenye thamani ya mamilioni ya fedha lililoko katika mji wa biashara wa Blantyre. Imesema pia ya kuwa imekamata magari 44 kati ya magari 149 ambayo rais huyo wa zamani wa Malawi anamiliki.
Vingine vilivyokamatwa ni jumba lake la biashara la Keza Office Park ambalo lilizinduliwa kwa mbwembwe, mgeni mwalikwa wakati huo Rais wa Tanzania, Benjamin Mkapa, na akaunti zake zote za benki.
Habari zinasema wakati hayo yakiendelea, Muluzi mwenyewe yuko Uingereza kwa matibabu.
Ofisa Uhusiano wa ACB, Egrita Ndala, amekaririwa na gazeti la kila siku la Malawi- The Daily Times, akisema taasisi hiyo bado inaendelea na uchunguzi wake.
" Kikosi cha Kupambana na Rushwa (ACB) bado kinaendelea na uchunguzi wa mali nyingine ili kujiridhisha na umiliki wake. Ni vigumu kwa sasa kusema mali nyingine ambazo zimepangwa kuchukuliwa, " alisema Ndala.
Katika hatua nyingine, kabla ya tukio hili la wiki hii, hivi karibuni rais huyo wa zamani wa Malawi alizuiwa kusafiri kwenda Uingereza na pasi yake ya kusafiria ikanyang'anywa baada ya kuzuka uvumi kwamba angetorokea Uingereza.
Hata hivyo, aliruhusiwa kuondoka kabla ya ACB kuvamia mali zake kama dhamana endapo atashindwa kesi hiyo na hatarejea nchini humo.
Habari kutoka nchini humo zinasema ya kuwa mwanasheria wa Muluzi, Jai Banda, ameomba zoezi la kukamata mali za Rais huyo lisitishwe. Muluzi aliwahi kukamatwa huko nyuma kwa kwa kesi hiyo hiyo.

Source: Raia mwema 5-11

My take:
Hivi mkuu wetu wa kaya hawezi kujifunza hapa au kwa Mwanawasa (RIP)?
 
Haka kamchezo kakihamishiwa Tanzania ni nani atabaki?? Nashangaa wanawachagua wa kupeleka Kisutu (Yona, Mramba na Mgonja) wakati wale wafujaji papa bado wanatesa ndani ya ofisi wakiendekeza kujilimbikizia mali na pesa kwa njia haramu!!! Ni wakati umefika sasa tulete nidhamu ya kazi kwa kuwafungulia mashataka na kufilisi mali za waliothibitika kufuja nchi hii ili iwe fundisho kwa viongozi wajao!! Je tutafika jamani??
 
kawaida yetu kuangalia na ku- appreciate kwa kichwa tu lakini hakuna utekelezaji, tunabaki kusema " you have very beautiful sofas" lakini mbona wewe hununui za nyumbani kwako???? hiyo ndio yetu sisi,

ukiuliza watakuambia kuna "mchakato" wa kuanza kutafuta ni wapi alikosea, halafu aundiwe tume ati hawataki kukurupuka.....
 
Kwa kweli hali ni mbaya sana, hili ni fundisho kwa baba Hosea, maana kama jirani zake wanaweza kuwawajibisha wakuu kama hao ni wakati nae sasa ajaribu kutokufichiana maovu na kuwaweka wazi hawa walimbikiza mali zisizokuwa halali za kibongo.

Mi kwa upande mmoja naunga mkono lakini upande wa pili nachukulia hili kama somo kwa nchi yetu. Iwe ni somo kwa maana tuige na kutekeleza ili tusiwe na taifa la vibaka wa haki za wanyonge na wapenda kuvutia pande zao tu!

Nawakilisha.
 
Imefika wakati sasa kwa wa Tanzania kufanya kazi kwa kufuta sheria na taratibu zilizopo nakuzingatia misingi ya haki, na siyo kumwangalia mtu usoni tukibagua watu waliofanya makosa.
 
Kwa kweli hali ni mbaya sana, hili ni fundisho kwa baba Hosea, maana kama jirani zake wanaweza kuwawajibisha wakuu kama hao ni wakati nae sasa ajaribu kutokufichiana maovu na kuwaweka wazi hawa walimbikiza mali zisizokuwa halali za kibongo.

Mi kwa upande mmoja naunga mkono lakini upande wa pili nachukulia hili kama somo kwa nchi yetu. Iwe ni somo kwa maana tuige na kutekeleza ili tusiwe na taifa la vibaka wa haki za wanyonge na wapenda kuvutia pande zao tu!

Nawakilisha.
Hosea hapo hana la kujifunza kwani yeye analinda waliompaa ulajii..huko malawi pia baada ya utawala kubadilika na mwenye nchi kuamua kupambana na ufisadi kwa dhati ndo maana hayo yanatokeaa..

Sisi hapa tukibadili mfumo wa utawala na kupata kiongozi wa kupambana kwa dhati na ufisadi basi tutafika hukooo...
 
Muda unacheleshwa tu ila umbo mbioni kuja maana hamna namna ya kuikatalia sauti inayodai haki. Na natural life principles...unapanda mahindi na unategema wakati wakuvuna utavuna mahindi pia. Sijapata kusikia mtu kapanda bangi halafu kavuna maharage. Kila mtu atavuna anayopanda hata kama longolongo hizi zinaendelezwa. Upo muda itakuwa ngumu kuendelea kuchezesha viini macho
 
muda unacheleshwa tu ila umbo mbioni kuja maana hamna namna ya kuikatalia sauti inayodai haki. Na natural life principles...unapanda mahindi na unategema wakati wakuvuna utavuna mahindi pia. Sijapata kusikia mtu kapanda bangi halafu kavuna maharage. Kila mtu atavuna anayopanda hata kama longolongo hizi zinaendelezwa. Upo muda itakuwa ngumu kuendelea kuchezesha viini macho

nani atamfunga paka kengele?
 
nani atamfunga paka kengele?

There you are. Maana ufisadi uliofanyika chini ya Mkapa ndiyo uliomuingiza mkuu hapo alipo. Akijaribu kukamata mali za Ben anaweza akajikuta anajikamata na yeye mwenyewe!

Hivi ni mpaka chama kingine kishike madaraka ya nchi ndiyo hawa mafisadi washitakiwe?! mbona Mwanawasa aliweza? Kwa nini huu utamaduni wa kulindana tusiuache?

Lakini ipo siku. Siku itakapofika anayelindwa na anayelinda wate watakuja kuwa watuhumiwa. Dunia itakuwa ndogo mno kwao kujificha!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom