Malezi ya wazazi huchangia sana mabinti zao kuwa wasagaji!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Mwanamke ambaye ana tabia a kujilaumu yeye kama mwanamke na kulaani kuwa kwake mwanamke, yuko kwenye nafasi kubwa ya kumuuwa mtoto wake wa kike kisaikolojia. Kuna wanawake ambao kwa kuudhiwa na waume zao au hata na wanawake wenzao huwa wanapenda sana kuropoka kauli za kudhalilisha jinsia ya kike.

"Mimi nakwambia sisi wanawake hatufai kabisa, kuzaliwa mwanamke ni jambo baya sana………ningekuwa naweza nimwombe Mungu anibadilishe niwe mwanaume …. Wanawake ni wajinga sana…." Kauli za aina hii zinaporudiwa mara mbili au tatu humfanya mtoto wa kike kuziamini na huanza kuwa na wasiwasi na jinsia yake. Hata watoto wa kuime nao huziamini kauli hizi na kuanza ‘ubabe' wa kiume kuanzia hapo.

Mtoto wa kike anapozisikia kauli hizi kutoka kwa mama yake na kwa sababu mama yake ndiye ‘shujaa' wake, huanza kujenga dhana kwamba, kama mama yake hapendi kuwa mwanamke, kwa sababu mwanamke ni mjinga na dhaifu, naye hana budi kuikimbia hali hiyo. Anaikimbiaje?Kuna njia nyingi za kukimbia hali hiyo, lakini kubwa na ya karibu ni kwa mtoto huyu kuanza kujibainisha na jinsia ya kiume. Kwa sababu akili ya mtoto haichuji, huanza kuhisi vibaya kuwa kwake mwanamke mbele ya wenzake, hasa wanaume.

Kujibainisha na jinsia ya kiume ni pamoja na kufuatana na wanaume, kuvaa kiume, kuongea kiume, kutembea kiume na kufanya kazi za kiume.
Siyo lazima, lakini mtoto huyu anaposhindwa kupata mahali ambapo atadondosha dhana au imani hii, ni wazi atakuja kujibainisha kimapenzi, atajibainisha kama mwanaume. Matokeo ya jambo kama hili ni kuwa na mwanamke ambaye anataka kuwa mwanaume kwa wanawake wenzake kimapenzi.Kama sio kauli za akina mama kujilaumu, kauli za akina baba kuwalaumu wanawake pia na akina mama kuzikubali kivitendo, zinaweza kuwaathiri watoto wa kike kimakuzi.

Baba anapokuwa na tabia ya kutoa kauli kali na chafu dhidi ya mama, na mama kuonyesha kukubaliana na kauli hizo kwa vitendo ni hatari sana.
Hebu sikia kauli kama hii kutoka kwa baba: "Mwanamke gani anayezaa mitoto ya kike tu, ni afadhali kuoa mke mwingine….." majibu ya mwanamke anayekashifiwa ni haya: "Kwani mimi nimetaka, si Mungu mwenyewe, kwani hata mimi si ninapenda watoto wa kiume……" Kwa mtoto wa kike majibu kama haya, huwa yanasikika masikioni mwake kama, "Hata mimi sitaki watoto wa kike kwa sababu hawana thamani, lakini sina uwezo wa kuwakataa.."

Akina mama, yawapasa kuelewa kwamba, kauli zao na kuzipa kauli za waume zao nguvu, huweza kuwaathiri sana watoto wao. Kila neno wanalotamka kwa watoto ni lazima walikague mara mbili. Waume zenu wanapotoa kauli zinazobagua watoto kijinsia mbele ya watoto hao ni lazima mzikanushe sawia na kuwaeleza watoto ukweli utakaowapa nguvu ya kufurahia jinsia waliyonayo.
 
Nafurahia kuzaliwa mwanamke, na pia natamani nizae watoto wa kike tupu na natumaini Mwenyezi Mungu atasikia ombi langu hili
 
Umeandika akila tupu hapa mkuu'watoto wengi wa kike wanakutana na matatzo kama haya'.
 
Hayo uliyoandika madhara yake ni kuwa na binti asiyejiamini na kuamini wanaume ni kila kitu.

La ulesbian halisababishwi na maneno. Sana sana kwa Tz ulesbian unachangiwa na watoto kusoma boarding schools za wanawake watupu. Wengi wanaoana huko na nilishasikia habari za ndoa za boarding school toka sijajua neno lesbian. Boarding zinaharibu watoto.
 
Hayo uliyoandika madhara yake ni kuwa na binti asiyejiamini na kuamini wanaume ni kila kitu.

La ulesbian halisababishwi na maneno. Sana sana kwa Tz ulesbian unachangiwa na watoto kusoma boarding schools za wanawake watupu. Wengi wanaoana huko na nilishasikia habari za ndoa za boarding school toka sijajua neno lesbian. Boarding zinaharibu watoto.

Nayo ni moja ya sababu...............
 
Hayo uliyoandika madhara yake ni kuwa na binti asiyejiamini na kuamini wanaume ni kila kitu.

La ulesbian halisababishwi na maneno. Sana sana kwa Tz ulesbian unachangiwa na watoto kusoma boarding schools za wanawake watupu. Wengi wanaoana huko na nilishasikia habari za ndoa za boarding school toka sijajua neno lesbian. Boarding zinaharibu watoto.

Ni kweli boarding school zinachangia sana kuharibu watoto iwe ni wa kike au kiume. Pili malezi ya wazazi, kuna dada mmoja tuko naye department moja ni lesbian asiyeficha hali yake na anakiri kufundishwa na shangazi yake tabia hii.
 
Si kusoma boarding school za wanawake pekee,bali pia hata hii tabia ya kutoka out na shost wako,then mnalewa kisha mnaenda kulala pamoja,coz kuna wanawake wengine wakilewa pombe inawatuma wafanye sex,we unafikiri hapo atafanyaje na ukiangalia boy wake yuko mbali? Wanaamua kujitibu na matokeo yake wanalewa na tabia hii.
 
Ingekuwa kuishi/kujiassociate/kuzungukwa na wanamme unakuwa lesbian?
Sijui wengine wangekuwa wapi, labda wangeshaota hata mshedede.

Kikubwa ni kumfunza mtoto kujitambua na kwa na values katika umri mdogo, huko aendako kwingine atakuwa keshajijengea mipaka yake.
 
Back
Top Bottom