Malezi ya DADA WA KAZI.

Luvvy

Member
Apr 23, 2012
16
0
Nna jirani yangu mwenye mtoto wa mwaka mmoja. Ye na mume wake wote wameajiriwa kwahiyo huwa wanamuacha mtoto na dada wa kazi.

Kitu cha kwanza kunotice ni kwamba siku mmoja wao akiwepo nyumbani mtoto halii lii sana.Mpaka kuna wakati hua nadhani labda wametoka kwa ukimya kumbe wapo. Ila wakiwa hawapo mtoto analia kila saa, na dada wa kazi full kumfokea na kumtisha kumpiga(pengine hua anafanya kweli).

Sasa juzi ndio alinichosha kabisa. Nilimkuta kakaa barazani alafu kamlaza yule mtoto juu ya miguu yake, kichwa kimegusa sakafu alafu anamnywesha uji. Uji mwingi unaishia chini na puani, mtoto analia, dada ni kelele tu "ntakupiga!!!"kwa wingi na kulalama kuhusu uji unaomwagika.

Sikusema neno ila leo nimefikiria weee nikaona kuwa mimi nisingependa mtoto wangu awe analishwa kwa style hiyo au kupigwa hata kufinywa na mtu yeyote yule katika umri huo. Sasa najiuliza kama nimweleze jirani namna mwanawe anavyokuwa treated akiwa hayupo au la. Kama jibu ni ndio, nianzeje????

Maoni tafadhali.
 
nakuomba umweleze please nasikia uchungu nahisi kama wangu ndo anafanyiwa hivyo. ongea na mama mtoto au baba avizie siku washuhudie afu atafute alternative..... Jaman hawa wadada unaweza ukauwa!
 
Nakuomba umueleze haraka tena umechelewa nakumbuka wakati tunakua tulelewa na jamii yote inayotuzunguka jirani akiona kosa tu jiandae siku haiishi halijafika nyumbani sijui nini kimetubadilisha sasa.
 
wewe ulitakiwa pale pale umsaidie yule binti namna nzuri ya kumlisha mtoto pengine ni uelewa wake mdogo ktk jamii wote ni wazazi yule sawa na mtoto wako
 
Mueleze bana!!! kabla hali haijawa mbaya zaidi...Huo ndio tunaita ujirani mwema...Ingekuwa ni mwanao anatendewa hivyo ungependa jirani akutaarifu kinachojiri unapokuwa hauko nyumbani...ukija kusikia huyo mtoto amefariki labda kwa mateso ayapatayo kwa huyo binti utajilaumu sana.

Nna jirani yangu mwenye mtoto wa mwaka mmoja. Ye na mume wake wote wameajiriwa kwahiyo huwa wanamuacha mtoto na dada wa kazi.

Kitu cha kwanza kunotice ni kwamba siku mmoja wao akiwepo nyumbani mtoto halii lii sana.Mpaka kuna wakati hua nadhani labda wametoka kwa ukimya kumbe wapo. Ila wakiwa hawapo mtoto analia kila saa, na dada wa kazi full kumfokea na kumtisha kumpiga(pengine hua anafanya kweli).

Sasa juzi ndio alinichosha kabisa. Nilimkuta kakaa barazani alafu kamlaza yule mtoto juu ya miguu yake, kichwa kimegusa sakafu alafu anamnywesha uji. Uji mwingi unaishia chini na puani, mtoto analia, dada ni kelele tu "ntakupiga!!!"kwa wingi na kulalama kuhusu uji unaomwagika.

Sikusema neno ila leo nimefikiria weee nikaona kuwa mimi nisingependa mtoto wangu awe analishwa kwa style hiyo au kupigwa hata kufinywa na mtu yeyote yule katika umri huo. Sasa najiuliza kama nimweleze jirani namna mwanawe anavyokuwa treated akiwa hayupo au la. Kama jibu ni ndio, nianzeje????

Maoni tafadhali.
 
Hao ndio ''HOUSE MANAGERS'' !

Mweleze kesho mbele ya house manager akiwepo ili kukata mzizi wa fitina
 
Nna jirani yangu mwenye mtoto wa mwaka mmoja. Ye na mume wake wote wameajiriwa kwahiyo huwa wanamuacha mtoto na dada wa kazi.

Kitu cha kwanza kunotice ni kwamba siku mmoja wao akiwepo nyumbani mtoto halii lii sana.Mpaka kuna wakati hua nadhani labda wametoka kwa ukimya kumbe wapo. Ila wakiwa hawapo mtoto analia kila saa, na dada wa kazi full kumfokea na kumtisha kumpiga(pengine hua anafanya kweli).

Sasa juzi ndio alinichosha kabisa. Nilimkuta kakaa barazani alafu kamlaza yule mtoto juu ya miguu yake, kichwa kimegusa sakafu alafu anamnywesha uji. Uji mwingi unaishia chini na puani, mtoto analia, dada ni kelele tu "ntakupiga!!!"kwa wingi na kulalama kuhusu uji unaomwagika.

Sikusema neno ila leo nimefikiria weee nikaona kuwa mimi nisingependa mtoto wangu awe analishwa kwa style hiyo au kupigwa hata kufinywa na mtu yeyote yule katika umri huo. Sasa najiuliza kama nimweleze jirani namna mwanawe anavyokuwa treated akiwa hayupo au la. Kama jibu ni ndio, nianzeje????

Maoni tafadhali.

Mwambie, jamani. Utakuwa umesaidia mtoto na jambo la kujivunia. Mimi hapa nilipo niliwahi kufanya hivyo, walipogundua walinipa zawadi kwa kunusuru mtoto wao maana waligundua mengi ya kifo kilichokuwa kinamsubiri mtoto
 
ndugu mweleze mapema tena hata usiku huu next time anaweza kumuua jamani si mnakumbuka yule binti aliye muua mtoto wazazi wa mtoto wakiwa kazin kisha yeye kuondoka? jamani niliskia ushuhuda huu nilichanganyikiwa kiukweli dont wait for a second to pass my dear the kid is innocent mweleze huyo mama tena akiwa na mumewe ili wajue na waamue kwa busara. pse usilale nacho kamwe.
 
wewe ulitakiwa pale pale umsaidie yule binti namna nzuri ya kumlisha mtoto pengine ni uelewa wake mdogo ktk jamii wote ni wazazi yule sawa na mtoto wako
mkuu uko sahihi but kama ni outsider kisha ukamwambia ndo kabisa atamkomoa mtoto huko ndani, achana na binti akisha kuwa na moyo wa unyama yaani kama anaweza kumfinya mtoto what do u expect? ni waz kwamba ni kifo ndicho anachosubiri tu.
 
Mueleze bwana, hata kama unaogopa, fanya maarifa upate japo namba ya huyo jirani UNTUMIE SMS KALI ya kuelezea ukweli wa tukio. Hapo utaepuka kusutwa na mdundiko!!! Wadada wa shida mjini basi mtu unaweza kumwambia akamkanya tu dada wake, alafu ukawa unajistukia, wamaza wengine choka mbayaa! Ila hiyo ya SMS itakulinda alafu ataogopa sana hadi mtu wa mbali kasema, atawalaumuje majirani? Tena kwenye sms unashauri ACHUNGUZE MWENYEWE ULE MDA MTOTO ANAOPEWA UJI!!!!!
 
Unasubiri nini? Jaribu kugeuza mkanda kwako, Je ingekuwa mwanao ungependa uelezwe anayofanyiwa kwa wakati gani? Bila shaka ni mapema kabla hajaumia!
 
huo ndo ujinga wa wazazi wengi wanaoelekeza akili zao katika kusako shekeli halafu wanasahu kama wanawatoto home
usilete za uswazi, acha familia zijilee, we utamtafutia msichana mwingine?
lea familia yako, achana na familia za watu
 
Mweleze haraka sana, tena mwambie ategeshee aisende kazini ina na muda huo huo amfukuze maana akimwacha na mtoto atamfanyia unyama.
 
Ooh my God 2mbo linankata, yan kama naona vile mwanangu anafanyiwa hvy! Ma hg jaman hawa wa2 cjui wakoje? Weng hawajali kaz ilowapeleka af midomo juu kulalamika wanateswa. Ningekua mimi ningemtandika 4 sure. Waeleze pls ikiwezekana ajifanye kenda kazn ili amfume.
 
Acha roho mbaya, huyu mtoto akipata tatizo na we ujue umehusika, uwezi kuona mtoto analelewa ndivo sivyo na we ukakaa kimya. Acha wakuite mbeya lakini kawaeleze wazazi wake
 
Natumaini mpaka muda huu utakuwa umemueleza. Maana wote wamekushauri hivyo!

Ubarikiwe.
 
mueleze, tena mueleze mbele ya huyo binti, ili siku nyingine ajue hata majirani wanaona na hawafurahishwi na matendo yake, atabadilika
 
nadhan anatakiwa kufahamu hilo lakini ili kujitoa katika neno mbea mwombe afanyie uchunguz hilo, ajue kwa ushahidi kamili, pengine mama akiwepo home, dada anamlisha vizuri n ukienda kichwa kichwa kumwambia mama atakushangaa na anaweza asikuamini. hayo ni mawazo yangu tu
 
Back
Top Bottom