Mwakalinga Bujo
JF-Expert Member
- Oct 22, 2008
- 2,719
- 1,440
- Ha! ha! ha! ha! Great Thinker bwana unanivunja mbavu sana, yaani unataka nivae gwanda level ya nyumba kumi kumi? ha! ha! ha! ha!
- HUKU BONGO USIKU SAA IZI, USIKU MWEMA SANA MKUU WANGU!
William.
Mkuu wa kazi aka Le Mutuz siasa wewe huiwezi kwasababu una upeo mdogo sana wa kufikiri kama sio uvivu wa kufikiri.Huwa hujiamini kwa kile unachofanya hata siku moja,ungekuwa unajiamini usingetoa post na pics kwa wall yako ya fb kipindi cha mchakato wa kugombea uwakilishi kwenye bunge la Afrika mashariki.Jipange kamanda safari yako bado ni ndefu sana.
Ungekuwa unasoma alama za nyakati kipindi hichi ungekaa sana karibu na baba yako akupe mbini za kushinda/kukabiliana na baadhi ya wanafiki wa magamba, kwani hata yeye na unguli wake kwenye medani ya siasa walimuadhibu.Ila kama hujaamua kubadilisha maisha yako ya kuigiza hata hizo pesa kidogo ulizozichanga kipindi hicho unazunguka 90% ya dunia (kama unavyojitapa kila kukicha) zitaisha na watakutungia nyimbo kama Mac Muga.
Binadamu huwa anatabia ya kuunganisha matukio pindi anapotaka kumtafutia makosa adui/mpinzani/mshindani wake.Jifunze zaidi kuliko kujiona unajua mengi,kwa exposure unayojigamba nayo ,wewe sio mtu wa kufungua blog na kuanza kuwasifu kina Sinta/Jokete.Kuna mambo mengi sana ambayo unaweza ukatufundisha kwa njia ya blog ikiwa ni pamoja na kutoa burudani lakini si kwa hicho unachokifanya.Ukweli ni kwamba wewe maisha yako halisi huwezi yaacha,hivyo endelea na ndoto zako ulizokuwa nazo tokea utotoni acha kupoteza muda kunye mambo ambayo ni magumu kulingana na upeo wako hususani Siasa.