Malecela: Tanzania itakuwa ya 11 kiuchumi duniani miaka 20 ijayo

Mzee malecela amesema kwa mujibu wa magazine moja linalochapishwa marekani, Tanzania itakuwa ya 11. Aliisoma magazine hii akiwa Marekani (hivi karibuni) hajasema lini.

Hiyo magazine ilisema miaka 20 ijayo, China itakuwa ya kwanza ikifuatiwa na India, ya tatu Marekani na Tanzania Ya 11. Amesema Tanzania ni ya 3 Africa kwa utoaji dhahabu, Soda ash ni ya pili Duniani baada ya Marekani, Makaa ya mawe tunayo mengi sana.

SISI SIYO MASKINI!..

Source: Dkk 45, ITV

Mkuu tenende, Comrade Mzee Malecela aidha hajui au amesahau kuwa hiki kizazi na vijavyo ni vya data/evidence...

1. Alipaswa kusema ni gazeti lipi, limesema hivyo kwa analysis gani, lini na wapi?

2. Yeye kwa mtazamo wake comrade, kwa uzoefu na haya anayoyaona,(60% of Tanzanian budget kutegemea donors) anakubali "analysis" yeyote?!!

3. Aidha anazeeka vibaya, au anauhakika hatakuwepo after ten years from now(AND am not sure af the later)..kwamba after 10years from now Tanzania ikimkumbusha maneno ya gazeti lake)!!!


POOR ANALYSIS OF THE CENTURY...Tusitegemee miujiza kutoka tulipo "na kuwa number 11"..eti tu kwa sababu "gazeti la marekani limesema"
 
Katika interview iliyokuwa inarushwa na ITV leo, Mzee Malecela aliulizwa na mtangazi kuhusu inflation inavyomgusa Mtanzania. Kwa kweli it was very poor analysis for a person with such extensive CV.




Hii elimu ya mwaka moja moja kila mahali ikaaje au kuna makosa?
 
Malecela once again has proved kwamba nje ya Sokoine na Nyerere, Tanzania haijawahi kuwa na Waziri mkuu mwingine mwenye uwezo wa kiuongozi kama mzee huyu; I remain to wonder mambo mawili:

1. Uhuni wake ambao tuliambiwa ndio ulipelekea ashinikizwe kujiuzulu ulikuwa ni uhuni wa namna gani? Wengine tulikuwa wadogo kuelewa mambo kwa undani;

2. Ingetokea Malecela akawa Rais wa tatu au wa nne wa Tanzania, angefanya kitu gani tofauti?

Well said ndugu yangu.

Kuhusu swali lako la kwanza, huyu Mzee Jumanne alikuwa mhuni literary.
Na moja ya uhuni wake aliwahi kuruka mpaka (cross the border) kwa kuwa na mahusiano na mtu fulani wa Mwalimu. Wengi waliduwazwa na ujasiri na wendawazimu huo (in one package). Alikuwa bingwa wa mikakati mibovu na ya kipuuzi ambayo haifai hata kutaja.

Pia nakumbuka baadhi ya watu wachache waliokuwa wanamfaham Malecela (kwa kufanya naye kazi) walikuwa wanamwita "hatabiriki". Of coz, unakumbuka pia kuna watu wachache walikuwa wanamwita Baba wa Taifa "haambiliki".....
 
Hebu tujiulize wanabodi; Watu wa jimbo lake la uchaguzi pale Dodoma waliona Livingstone Lusinde (Mbunge wa sasa Mtera) ni kichwa kuliko huyu Malecela....je hali ya huyu mzee ni ipi? Jaribu tu kupata picha status yake halisi ikoje.

Wengi wetu tunamwona Lusinde ni caliber ya Mirembe, a plain thug to be precise. Lakini kwa wana-Mtera Lusinde was/is some quantity.
 
kati ya watu walioongea bila point ni huyu mzee wangu. nilivumilia sana kuangalia kipindi chake tangu mwanzo hadi mwisho. hakuna hata point aisee, ndo maana tunasema hii nchi inatakiwa kuongozwa na vijana, wazee hawana kitu aisee, amekuja tu kuwaaibisha wazee wenzie kuwa ukizeeka mwili hata akili inazeeka.

hata kama lipo hilo gazeti au magazine navyosema, uchumi hautathminiwi kukua bila vichocheo vya uchumi kusitawi, kustawishwa ipasavyo katika sekta zote za uchumi.Ni ndoto kufikiria kuwa wa kumi na moja bila jitihada, hiyo ni financial mastabertion.Ni lazima kuhimiza jamii yetu kufanya kazi kwa bidii na maarifa, ni lazima kuwezesha kusitawisha nyanja zote za uchumi zikue ili kuleta usitawi wa uchumi mpevu, siyo kama sasa, kila sekta kivyake na zingine kusahaurika kama kilimo.Pia ni lazima kuwe na muunganiko wa shughuli za kiuchumi na uratibu wake.haya maneno ya blabla kujipendekeza wamkumbuke huyu mzee hayatatusaidia itakuwa kujidaganya.
 
ukiwa na rais kama huyu, nchi inaweza kurudi kwenye zama za ujima. hivi mzee kumbe huwa namheshimu nikijua kuwa anao uelewa wowote wa namna ya kuikomboa hii nchi, kumbe hamna kitu kabisa aisee, sijui uzoefu wake wote ni diplomasia za kirussia zinazowafanya watu wawe mambumbumbu kwa kudanganywa kwenye chama chake....nimepoteza muda kuangalia kipindi kile aisee.
KWELI HUYU MZEE ANA DISPLOMASIA ZA KIRRUSI NA mpambe WA NCHI ZA KIARABU. Si unajua Mama migiro alipokwenda kuwa Naibu katibu mkuu wa UN. Mzee malecela alimuaga na kusema " ukifika huko UN, kaseme, Tanzania haitaki majeshi ya Uvamizi Iraq! KUmbuka muda wote aliokaa madarakani kama vice president, hakuwahi kuilaani Uganda hata siku kwa kukalia ardhi ya Zaire.

Hawa ndio watu waliotufisha hapa tulipo katika umasikini mkubwa sana ingawa tuna mali. Kashika posts mbali mbali nyingi sana na nyeti serikalini, lakini hajawahi hata siku moja kutatua kero ya masikini! Ni mtu aliyejitenga sana na jamii na alikuwa mbali sana na matatizo ya watu.
 
tuache ndoto za asubuhi. hatuwezi kupata maendeleo ya kiuchumi kwa kuandikwa kwenye magazine. tufanye kazi na tukatae rushwa. plus siasa safi. period
 
Hii elimu ya mwaka moja moja kila mahali ikaaje au kuna makosa?

Fast track, courtesy of Chief Mazengo. Matokeo yake ndo hayo, mtu hata debate club hakupita anaenda kuwa kiongozi.

Uzeeni anasema mambo kijumla jumla "kuna gazeti moja nimesoma linasema Tanzania itakuwa ya 11 kwa uchumi in 20 years".

Magazeti yanatakiwa kuku quote wewe mzee wa nchi, sio wewe una quote magazeti bila hata ya kutaja details za jina la gazeti tulichunguze vizuri.
 
uyu mzee amnazo kabsa!....mfo, china,usa,korea,india,japan,southafrca,franc,uk,kenya,brazl,german,canada,saud arbia,iran, watakuwa wap? Wakat sisi rwanda,botwana,kenya wame2acha mbal?..hii michozo michafu ya ccm ya kuwadaa watz cjui itaisha ln! Jaman sis sio wafu 2naona 2natambua na 2naelewa
 
Wakuu,
Nawakubali wana- Jamiiforums kwa maswali muhimu juu ya linki na jina la 'magazine' , maana hata Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alipata kusema namnukuu
"mtu mwenye akili akikupa mawazo ya kipumbavu halafu
anajua unajua ni ... ukiyakubali anakudharau" J.K Nyerere.

Sasa hawa CCM na wazungu wao tumewastukia, lazima walete linki tupitie jarida (magazine) tuone mbinu gani chini ya CCM wanaweza kufikia lengo la kuwa nchi ya 11 kubwa kiuchumi duniani.
 
Lakini Ametaja tu MAGNITUDE ni 11 hajatoa DIRECTION may be ni ya 11 tokea Nkian. Nasikia sasa hivi Ni Ya 3 tokea Nkiani sasa tukifika 11 in 20 years yeye kaona ni poa! The the the! Ukiona mahali wameona Lusinde ni jembe ujue pagumu.
 
N i ajabu kusikia comments za mzee Malecela. Ni msomi wa haja na mkongwe wa siasa za fitna tangu enzi za Mwl. Aliyeyuandikia CV yake kaacha mengi na amekosea miaka sana. Kifupi huyu ni moja ya wasomi kumi wenye shahada nchini hadi wakati wa uhuru. Anaongoza kwa vyeo kuliko mwana CCM yeyote yule.

Marekebisho machache ni haya hapa.

1949-1952-Alliance Sec School(Mazengo Sec/ St John's University)
1953-1954-St Andrews College(Minaki Sec School)
1954-1959-The University of Bombay in India(B.Com Degree)
1961-1962-Cambridge University

Vyeo inaweza kuwa page nne. Lakini kwa point zile kweli mzee amezeeka sana. Lakini mbona kaka yake (Hon Balozi, Job Lusinde) yuko fiti hata kwa hoja?
 
Mimi naona mnapoteza muda kujadili mada za Mzee Malecela! Huyu mzee kwa sasa anatakiwa apumzike, amechoka na kwa kweli amechoka kisawasawa!

Siwezi hangaika kujadili wakati hakutoa source! Haya ndo mambo waliyokuwa wantudanganya nayo wakati wa siasa za cham kimoja!!!
 
KWELI HUYU MZEE ANA DISPLOMASIA ZA KIRRUSI NA mpambe WA NCHI ZA KIARABU. Si unajua Mama migiro alipokwenda kuwa Naibu katibu mkuu wa UN. Mzee malecela alimuaga na kusema " ukifika huko UN, kaseme, Tanzania haitaki majeshi ya Uvamizi Iraq! KUmbuka muda wote aliokaa madarakani kama vice president, hakuwahi kuilaani Uganda hata siku kwa kukalia ardhi ya Zaire.

Hawa ndio watu waliotufisha hapa tulipo katika umasikini mkubwa sana ingawa tuna mali. Kashika posts mbali mbali nyingi sana na nyeti serikalini, lakini hajawahi hata siku moja kutatua kero ya masikini! Ni mtu aliyejitenga sana na jamii na alikuwa mbali sana na matatizo ya watu.

Huyu mzee angelikuwa rais 2005, sijui hii nchi ingelikuwa wapi?!!!:nerd:
 
Back
Top Bottom