Malecela na Lowassa - Njia mbili tofauti?

kama mbunge wa muda mrefu na kiongozi wa serikali bungeni kwa kipindi cha miaka miwili el anajua fika kwamba alistahili kujitetea kwanza bungeni. kama bunge lingempiga mkwara hapo ndipo naamini angeweza kukimbilia kwa wananchi au vyombo vya sheria na kusema yale alozuiwa kusema bungeni.
 
ndugu zangu,

..kuna hali ya kuamini kwamba Bunge liko juu ya wananchi. Bunge ni mali ya wananchi--viongozi na wasio viongozi.

Sawa lakini Bunge linaongozwa kwa sheria za Bunge na nchi inatambua sheria hizo na hakuna mtu ambaye anaruhusiwa kuvunja sheria hizo kwa sababu ana uchungu au hisia ya kisasi.


..si makosa kuzungumzia uamuzi wowote ule wa Bunge, au kupingana nao mitaani. leo hii tukimzuia Lowassa kufanya hivyo, kesho yanaweza kumkuta mwananchi wa kawaida.

Ndiyo kuna makosa na mengine yanaweza kugongana na sheria. Tafadhali pitia sheria ya Haki, Madaraka na Kinga ya Bunge. Hata hivyo, raia wa kawaida anafungwa tofauti na sheria hizo au taratibu hizo za Bunge na hakuna anayemkataza Lowassa asizungumze isipokuwa hekima ingetawala kile anachotaka kusema maana kama ni kujitengenezea zaidi sidhani kama amefanikiwa. Wenyewe wanasema plan yake hiyo imebackfire!
..Lowassa analalamika wakati Bunge limeshafanya uamuzi wa kupitisha Ripoti ya Mwakyembe. Hii si sawa na kuzungumzia suala lililoko mbele ya Mahakama. Lowassa alieleza kinyongo chake ndani ya Bunge, ana haki ya kueleza kinyongo chake nje ya Bunge.

Hilo yaweza kuwa kweli lakini kama ni "kuweka rekodi sawasawa" kama alivyosema TVT basi mahali sahihi ni pale Bungeni. Kitendo cha kudai ameonewa ni kitendo kinachohusu haki. Kwa maneno mengine na yeye mwenyewe ameyatumia ni kuwa Lowassa hakutendewa haki. Sasa kama hakutendewa haki anazo sehemu kubwa tatu ambazo angeweza kutendewa haki.

a. Angetoa hoja Bungeni kuwa Bunge lisijadili ripoti hiyo na kumuomba Spika aongeze muda wa Kamati ili aweze kuzungumza nao kwa vile hakuhojiwa. Hoja yake angeijenga alivyoijenga siku ya kujiuzulu na kumuomba Spika badala ya kuendelea na Mjadala aiactivate Kamati tena ili apate kujiuleza ili kama Kamati ingefikia mahitimisho yale yale basi yaonekane yamefikiwa kwa haki. Hakufanya hivyo, yeye aliamua "kuweka manyanga chini".

b. Lowassa wakati wa kujiuzulu na baada ya kuona mapungufu kwenye ripoti angemuomba Spika Bunge liahirishwe kwa muda ili yeye na wenzake waweze kupitia ripoti hiyo badala ya kuendelea kuchambuliwa ili waweze kupatiwa nafasi ya kutolea maelezo kuliko ilivyofanywa. Hakufanya hivyo; aliweka manyanga chini.

c. Lowassa hakuwa na sababu ya kuwahi kuzungumza siku ile ya pili na "kususa uwaziri Mkuu" alivyofanya. Angeweza kukaa kimya na kuwaacha waliokasirika wapige kelele na kuzungumza na hatimaye mwishoni kama alivyofanya kwenye hoja ya "kupaa" kwa ndege angeanza kujibu hoja kwa hoja na kuwaonesha udhaifu wa hoja za Dr. Mwakyembe hakufanya hivyo. Alizira Uwaziri Mkuu.


..Hii si mara ya kwanza uamuzi wa Bunge kupingwa nje ya vikao vya Bunge. Sote tunakumbuka jinsi Baba wa Taifa alivyopinga Azimio la kuundwa kwa serikali ya Tanganyika. Tena aliandika mpaka Utenzi, na kitabu. Je, alikuwa akifanya makosa? sidhani
.

Wakati Nyerere anafanya hivyo alikuwa Mbunge wa Jimbo gani?

..pia naomba tuelewane hapa kwamba yanayotokea ndani ya vyama vya siasa yanatuhusu Watanzania wote. Vyama vya siasa vinapokea mabilioni ya ruzuku kutokana na kodi yetu wananchi.

Agree!
..Yaliyomtokea Malecela ndani ya vikao vya CCM yanalihusu Taifa zima. Suala lililokuwa mbele ya vikao vya CCM lilikuwa uteuzi wa mgombea Uraisi wa Tanzania. Maamuzi ya vikao vile yana athari kwa Taifa. Yanatuhusu Watanzania wote.

Agree

..Naamini katika busara ya Watanzania ktk ujumla wetu. We can be fooled for sometime but not all the time. Sina wasiwasi na wananchi wa Monduli kwamba at the end of the day watang'amua kwamba Lowassa.

I doubt it!
 
Hata hivyo, kwa upande wa Lowassa hilo ni kinyume naye. Matukio yaliyofuatia kujiuzulu kwake yamethibitisha kitu kimoja; Lowassa anaamini kuwa anastahili kuwa kiongozi wa ngazi za juu na ya kuwa hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kumzuia na yuko tayari kufanya lolote lile kujijengea jukwaa la kujisafisha.

Lowassa siyo tu ameamua kujisafisha lakini ni wazi kabisa ameamua kuchallenge siyo tu nguvu ya Rais bali pia chama chake na kwa hakika Bunge la Jamhuri ya Muungano. Kwa mtu mwenye jazba kama Lowassa neno hekima na busara viko mbali naye na hisia za kisasi na kustahili zinamuongoza.

Ni kwa sababu hiyo kabla ya kutumiwa ujumbe hivi juzi, ujumbe uliokuwa loud and clear alikuwa ameaanda mkakati wa "full throttle" wa kuchallenge maamuzi ya Bunge, ukimya wa Rais kumtetea n.k Na zaidi alifikia uamuzi huo baada ya kuamua kutomjulisha Rais kuwa anaenda kujiuzulu hadi pale Rais aliposikia kwenye TV kama Watanzania wengine.

Lowassa siyo tu anataka kurudi katika uongozi bali pia anaandaa kisasi; kisasi ambacho kitaonekana zaidi siku zijazo ambapo Rais Kikwete anatarajiwa kufanya mabadiliko makubwa ya wakuu wa mikoa na wilaya akizingatia kile kinachofanyika Kyela kuhusu Mwakyembe.

Endapo Lowassa hataweza kukaa chini na kutulia busara na hekima katika kushughulikia mgongano wake na JK ajue kabisa kuwa anajitengenezea mazingira siyo tu ya kukataliwa na wana CCM wenzake bali pia kuonekana mbele ya wananchi kama adui wa Rais. Sidhani kama anataka hilo la pili kwani licha ya matatizo mengi yaliyopo Tanzania watu wengi bado wanamhusudu na kumheshimu Rais Kikwete (licha ya madhaifu yake mengi ya kiuongozi)kama Rais Halali wa Jamhuri yetu.

Jamani, Mwenzetu Lowassa amekula "Kloriti" ya nguvu kama Viagra au Ciallis, hivyo atafoka na kuchemka mpaka sumu ya "Kloriti" iishe. Labda mtu ampe "Loshoroo" ya nguvu kukata hiyo sumu kwenye "Kloriti" iliyompa mori kupita kiasi!

He has a 36 hours side effects of Ciallis! He still has an erection!;):rolleyes:
 
hey... mchungaji!! mtu mwenye mori ukimuongezea hiyo cialis si ndo itakuwa matatizo?
 
Still moving!

Watz na tafsiri za ajabu

1. Wao wakistarehe ukafanye kaxi ukipata ni mwizi

2.ukiwa na vision unataka kuitekeleza unaitwa una tamaa ya madaraka

3.mjasiriamali mzalendo ni adui na hatari, mjasiriamali mgeni ni Rafiki na mwema

4. Huna ulilomkosea mtu, kutwa kucha unalalamika uluowatendea mazuri wanataka kulipa kisasi badala ya kuwazawadia

5. Unakesha kusema watu Wa kanda Fulani hawajui na hawastahili uongozi, wakikubalika na umma unalalamika wanaleta ukanda...

6.wakiamini unachoamini ni magenious na wenye maarifa, wakiamini kinyume ni wapumbavu na malofa

7.tunaamini paka ni paka na wote ni sawa, paka mweupe ruksa kujikamatia panya atakavyo, paka mweusi afungiwe kwenye wavu akimwangalia paka mweupe akiua mapanya kwa kujifurahisha.

8. Tunauthamini na kuuhitaji mchango wako kiuchumi na kimawazo....hats hivyo hatukuhitaji uwe kongozi..iow, tunahitaji kodi zako, hatuhitaji usimamie zinavyotumika

Tuendelee.....
 
After all, Malecela is a just a common person - non visionary- a wise man, and groomed during the period of fear, follower to prophet nyerere....rendered docile.

Lowassa is a visionary, leader, younger, asiyeogopa mtu....ana ndoto.asiye mwanasiasa sana, anaeamini katika matokeo sio hadithi....

So, kuwafananisha Hawa so sawa....after all kwa ccm kibajaj so ni Wa maana kuliko cigwiyemisi?
 
Watz na tafsiri za ajabu

1. Wao wakistarehe ukafanye kaxi ukipata ni mwizi

2.ukiwa na vision unataka kuitekeleza unaitwa una tamaa ya madaraka

3.mjasiriamali mzalendo ni adui na hatari, mjasiriamali mgeni ni Rafiki na mwema

4. Huna ulilomkosea mtu, kutwa kucha unalalamika uluowatendea mazuri wanataka kulipa kisasi badala ya kuwazawadia

5. Unakesha kusema watu Wa kanda Fulani hawajui na hawastahili uongozi, wakikubalika na umma unalalamika wanaleta ukanda...

6.wakiamini unachoamini ni magenious na wenye maarifa, wakiamini kinyume ni wapumbavu na malofa

7.tunaamini paka ni paka na wote ni sawa, paka mweupe ruksa kujikamatia panya atakavyo, paka mweusi afungiwe kwenye wavu akimwangalia paka mweupe akiua mapanya kwa kujifurahisha.

8. Tunauthamini na kuuhitaji mchango wako kiuchumi na kimawazo....hats hivyo hatukuhitaji uwe kongozi..iow, tunahitaji kodi zako, hatuhitaji usimamie zinavyotumika

Tuendelee.....

UK poa sana.....
 
Lowassa ni mtu wa watu pia ana vision Malecela hakuwa nazo.Acha mwanaume apigane kiume...
 
This time wala sina muda wakubishana na wewe.najua imekuchukua sana muda kubadili twist>>na sasa ni bor anikuachie upate hasara mbaya peke yako km mkapa.
 
Mwanakijiji naona Lowamaniac wanaendelea kukushambulia na zile akili zao za Kipumbavu na Kilofa hawaoni Logic ndani ya uzi wako ...sasa wataisoma namba kwenye matobo na kanzu...washanza kulalama baaada ya kuiona nyomi ya Dar es Salaam na Katavi.Wametunga mambo ya ajabu mara NEC mara ooohhoo karatasi za kupigia kura Mara Cha wapumbavu na Malofa wao wameenda kupanda Daladala kuwakejeri raia wa chini.
 
Back
Top Bottom