Malecela, Diallo, Bashe, Nape ni wanachama hai wa JF- Gazeti la Mwanahalisi lasema

Status
Not open for further replies.

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,239
24,099
Gazeti la Mwanahalisi Tarehe 27/04/2011:

Gazeti hili lilipomtafuta William Malecela anayeishi New York, Marekani, kujua iwapo ni mwanachama wa Chadema alisema, “Si kweli hata kidogo.”

Alisema yeye ni mwanachama mwaminifu wa CCM, na kwamba hivi sasa yuko mbioni kufungua tawi la chama hicho mjini New York Marekani.

Alisema, “Tatizo la watu wa CCM hawataki kusoma, badala yake wanakuja na ripoti za kuokoteza mitaani. Mimi ni mwanzilishi wa JF, nimekuwa huko tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006.”

Kwa upande wake Maxence Melo, anasema wakati mtandao huo unaanzishwa mwaka 2006 kabla ya kampuni kusajiliwa mwaka 2008, kulikuwa na watu wengi sana, wakiwamo vigogo wa CCM.

Anasema miongoni mwa wanachama wa mtandao huo, ni Nape Nnauye, Hussen Bashe na Khamisi Kigwangala.

Anasema mbali na wanachama hao wanaofahamika kwa majina yao, wapo wanachama na viongozi wengi wa CCM, wanaotumia majina bandia.

Soma zaidi : Mukama amdanganya Kikwete | Gazeti la MwanaHalisi
 
Sasa wao kuwepo hapa ni tatizo gani? Mbona kuna vibaraka wengi wa chadema humu lakini hamna aliesema kitu.
 
jamani huu ni mtandao usiojihusisha na chama chochote kile,ingawaje waumini wake ndio wenye uhuru wa kuamini vyama,kwa mtindo huu yeyote yule awe na chama ama hana chama ni ruksa ktk huu mtandao JF,sasa wale wanaowatuhumu baadhi ya wanachama wao kuwa wapo tofauti na wao eti kwa kuwa wapo JF nadhani hawawatendei haki wahusika

ikiwezekana na wao tunawakaribisha kama bado hawajajiunga kwa majina bandia
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom