Kuna taarifa kwamba wakati wowote ndani ya siku mbili hizi Mzee John Malecela anatarajiwa kutoa tamko zito ambalo linaweza kutikisa nchi na Chama cha Mapinduzi (CCM). Lakini pia tamko lake linaweza kuweka mambo sawa na kutoa mwelekeo.
Tunafuatilia.
Malecela alifanya kosa fulani baada ya mchakato wa 2005; alikuwa too royal kwa CCM. Mzee wa watu alifanyiwa mizengwe ya ajabu na CCM wakati ule huku akiwa ndiye mtu pekee aliyekuwa kaijenga CCM ile kwa mikono yake kuliko mtu mwingine yeyote aliyetaka kiti cha urais wakati ule. Jampo alilotakiwa kufanya wakati huo ni kuacha partisanship na kuchukua statesmanship roles zaidi. Leo hii angekuwa anaogopwa na hata akina JK.
CCM walifanya kosa kubwa sana kumwachia Malecela asiendelee kuwa Makamu mwenyekiti wa CCM.
Msekwa naona anayumba kweli kweli. Wewe angalia CCM hii, juu JK, kushoto Msekwa na kulia Makamba. Hakuna mtu hapo, bora wamrudishe tingatinga aanze kuswaga takataka zozote.
Uhuru wa maoni ni ibara namba ngapi vile?
Malecela ni yule aliyewahi kubadili jina na kuitwa jumanne akapewa magari zaidi ya 64 kwa ajili ya kampeni na waarabu. nakumbuka nyerere alimwambia John ukisha kuwa raisi utalipajie hiyo mali. Mwalimu akamwambia Ali akimpitisha Jumanne atampigia mrema debe.
CCM ni dampo kweli hata aongee nani dampo limeoza linatoa funza hakuna wa kumsikiliza.Hana jipya ana hasira ya kunyimwa ulaji yeye na kilango.
Mtanzania, Malecela ni Mgogo. Ili uweze kuishi Dodoma, inabidi uwe Mvumilivu sana. Wagoggo AKA AGWE, wana kauvimilivu sana. Wao huwa hawana maneno maneno kama sisi/nyinyi. Hata wakoloni hapo walipita tu bila kupata matatizo yoyote. Ukichunguza sana unakubali kuwa Wagogo ni Wazaramo walioenda Dodoma kuchukua Mbuzi wa Arobaini........ mengine yatakuja endelea.
This country has gone to the DOGS believe me my Dear Wadanganyika
Mzee Malecela kama kawaida yake atakuwa katikati kujaribu kuweka mambo sawa.
Huyu mzee pamoja na kufanyiwa fouls zote na CCM lakini hakupiga kelele za kuonewa.
Which reminds me, aliwahi kuwajibu watu waliokuwa wanalalamikIa usafiri wa kwenda Kigoma miaka ya 80 alipokuwa waziri wa mawasiliano kwamba "THEY CAN GO TO HELL", na sisi tumjibu hivyohivyo ?
KLHN Wire
Alipoulizwa kuhusu mipango yake ya kisiasa ya baadaye na hasa kama ataingia tena katika kinyang'anyiro cha kugombea Urais Mzee Malecela alisema kuwa imekuwa ni utamaduni ndani ya CCM kwa Rais aliyeko madarakani kuachwa kukamilisha vipindi viwili vinavyoruhusiwa kikatiba na hivyo mpango huo kwake kwa mwakani haupo. Hata hivyo alionesha kuwa ana mpango wa kuendelea kulitetea jimbo lake la Mtera ambalo ameliongoza kwa karibu miaka 40 sasa.