Malecela apinga pendekezo la wazee kuenguliwa NEC

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Malecela ambaye amepata kuwa waziri mkuu, alisema haoni sababu ya wazee kuwa nje ya vikao vya NEC na CC kwani busara zao bado zinahitajika kwa ajili ya ujenzi wa chama chao.Wakati Malecela akipingana na mapendekezo hayo, habari zinasema kuwa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, mzee Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa wa Awamu ya Nne, wamefurahia mapendekezo hayo.

CCM ina mpango wa kuwaondoa marais wataafu na viongozi wengine waliowahi kushika nyadhifa za juu serikalini kuwa wajumbe wa kudumu wa NEC na CC.Lengo la kufanya hivyo inadaiwa ni kutaka kuwapumzisha kwani kuna wakati hujikuta wakikaa muda mrefu kwenye vikao vya chama, hali ambayo huwaathiri kiafya.Pamoja na kuwaengua kwenye NEC na CC, chama hicho kimepanga kuanzisha Baraza la Wazee ambapo wastaafu hao na wengine watapata fursa ya kutoa mawazo yao ya kujenga na kukiimarisha chama.

::Tanzania Daima::
 
hapa nahisi tayari jamaa wameshaandaa mipango yao ya kishenzi ambayo wanahisi itakwamishwa na wazee hivyo dawa ni kuwaondoa.ukishafikia stage ya kumkataa mzazi wako basi ujue kuwa laana haiko mbali.hizi ni dalili za kusambaratika kwa chama tawala!!! mwanzoni walitaka kuwatosa uvccm na sasa wanawatosa wazee.hiyo dhambi itawatafuna
 
Back
Top Bottom